Al-Alaq

سورة العلق

Sura 96 · Makki · 19 aya

96:1Juzuu 30 · uk. 597

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ1

Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba.
96:2Juzuu 30 · uk. 597

خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ2

Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu.
96:3Juzuu 30 · uk. 597

اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ3

Soma, ewe Nabii, kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu.
96:4Juzuu 30 · uk. 597

الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ4

Aliyewafundisha viumbe vyake kuandika kwa kalamu.
96:5Juzuu 30 · uk. 597

عَلَّمَ الْإِنْسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ5

Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu.
96:6Juzuu 30 · uk. 597

كَلَّا إِنَّ الْإِنْسَانَ لَيَطْغَىٰ6

Kweli, binadamu hukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu
96:7Juzuu 30 · uk. 597

أَنْ رَآهُ اسْتَغْنَىٰ7

akijiona ametosheka kwa utajiri wake.
96:8Juzuu 30 · uk. 597

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ8

Basi, ajue kila mwenye kutupa mipaka kuwa mwisho atarudi kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Atamlipa kila binadamu kwa alilolitenda.
96:9Juzuu 30 · uk. 597

أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ9

Je, umeona ujeuri wa ajabu zaidi kuliko wa mtu huyu, Abu jahl,
96:10Juzuu 30 · uk. 597

عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ10

Anayemkataza mja wetu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, anapomsalia Mola wake?
96:11Juzuu 30 · uk. 597

أَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ11

Waonaje iwapo mwenye kukatazwa kusali yuko uongofuni, vipi anamkataza?
96:12Juzuu 30 · uk. 597

أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ12

Au iwapo anaamrisha mwigine kumcha Mungu, vipi anamkataza hilo?
96:13Juzuu 30 · uk. 598

أَرَأَيْتَ إِنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ13

Waonaje iwapo huyu mwenye kukataza anakanusha lile alinganiwalo kwalo na kulipa mgongo,
96:14Juzuu 30 · uk. 598

أَلَمْ يَعْلَمْ بِأَنَّ اللَّهَ يَرَىٰ14

hajui kuwa Mwenyezi Mungu anaona kila analolifanya?
96:15Juzuu 30 · uk. 598

كَلَّا لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ15

Basi mambo si kama anvyodai Abu Jahl. Na asipokomeka na ushindani alionao na udhia wake, Tutamshika upaa wake kwa nguvu na kumtia Motoni.
96:16Juzuu 30 · uk. 598

نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ16

Upaa wake ni upaa wenye maneno ya urongo na vitendo vya makosa.
96:17Juzuu 30 · uk. 598

فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ17

Basi na awalete, mtupaji mipaka huyu, watu wa baraza ili wamsaidiye.
96:18Juzuu 30 · uk. 598

سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ18

Sisi Tutawaita Malaika wa adhabu.
96:19Juzuu 30 · uk. 598

كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِبْ ۩19

Mambo si kama Abu Jahl anavyoyadhania. Yeye, ewe Mtume, hawezi kukufanya lolote la kukudhuru Usimfuate kwa lile alilokuitia la kuwa uache Swala, bali msujudie Mola wako na uwe karibu na Yeye kwa kujipendekeza Kwake kwa kumtii.

Cheza kutoka mwanzo wa sura