At-Tin

سورة التين

Sura 95 · Makki · 8 aya

95:1Juzuu 30 · uk. 597

وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa tini na zaituni, nayo ni miongoni mwa matunda yanayojulikana.
95:2Juzuu 30 · uk. 597

وَطُورِ سِينِينَ2

Na Anaapa kwa jabali la Ṭūr Sīnā’ ambalo Mwenyezi Mungu Alisema na Mūsā juu yake.
95:3Juzuu 30 · uk. 597

وَهَٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ3

Na Anaapa kwa Mji huu wa amani, usiokuwa na mambo ya kutisha. Nao ni mji wa Makkah, chimbuko la Uislamu.
95:4Juzuu 30 · uk. 597

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ4

Hakika Tumemuumba binadamu katika sura nzuri.
95:5Juzuu 30 · uk. 597

ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ5

Kisha Tutampeleka Motoni akiwa hakumtii Mweyezi Mungu na hakuwafuata Mitume.
95:6Juzuu 30 · uk. 597

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ6

Isipokuwa wale walioamini na wakafanya amali njema; wao watakuwa na malipo makubwa yasiyokatika wala kupungua.
95:7Juzuu 30 · uk. 597

فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ7

Ni lipi linalokupelekea wewe, ewe binadamu, kukanusha kufufuliwa na kulipwa, hali ya kuwa kuna dalili wazi kwamba Mwenyezi Mungu Ana uweza wa kufanya hayo?
95:8Juzuu 30 · uk. 597

أَلَيْسَ اللَّهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ8

Je, Hakuwa Mwenyezi Mungu , Ambaye Ameiweka Siku hii kutoa uamuzi baina ya watu, ni muadilifu zaidi ya wanaosifika kuwa ni waadilifu katika kila Alichokiumba? Kwani? Alikuwa. Basi wataachwa viumbe rebe: hawaamrishwi wala hawakatazwi wala hawalipwi kwa mema wala hawateswi kwa mabaya? Hilo si sahihi wala haliwi.

Cheza kutoka mwanzo wa sura