Al-Inshiqaq

سورة الإنشقاق

Sura 84 · Makki · 25 aya

84:1Juzuu 30 · uk. 589

إِذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ1

Pindi mbingu itakapopasuka na kudhihiri mawingu katika pasuko zake Siku ya Kiyama.
84:2Juzuu 30 · uk. 589

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ2

Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ipasuke, na inastahili kufuata amri hiyo.
84:3Juzuu 30 · uk. 589

وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ3

Na pindi ardhi itakapotandikwa na kukunjuliwa.
84:4Juzuu 30 · uk. 589

وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ4

Na milima yake kuvunjwa-vunjwa Siku hiyo.
84:5Juzuu 30 · uk. 589

وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ5

Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ifanye hivyo, na inastahili kufuata amri hiyo.
84:6Juzuu 30 · uk. 589

يَا أَيُّهَا الْإِنْسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ6

Ewe binadamu, wewe unaenda kwa Mwenyezi Mungu na unafanya amali nzuri na mbaya, kisha utakutana na Yeye Siku ya Kiyama. Na huna budi kupata kutoka Kwake malipo mazuri zaidi ya amali yako njema au yanayolingana na amali yako mbaya.
84:7Juzuu 30 · uk. 589

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ7

Yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa mkono wake wa kulia,
84:8Juzuu 30 · uk. 589

فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا8

naye ni yule aliyemuamini Mola wake, atahesabiwa hesabu pesi.
84:9Juzuu 30 · uk. 589

وَيَنْقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا9

Na atarudi kwa watu wake Peponi akiwa ni mwenye furaha.
84:10Juzuu 30 · uk. 589

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ10

Na yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa nyuma ya mgongo wake,
84:11Juzuu 30 · uk. 589

فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا11

naye ni yule aliyemkanusha Mwenyezi Mungu, ataita maangamvu na hasara,
84:12Juzuu 30 · uk. 589

وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا12

na ataingia Motoni.
84:13Juzuu 30 · uk. 589

إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا13

Hakika yeye alikuwa kwa watu wake ulimwenguni ni mwenye furaha na majivuno, hafikirii mwisho wake utakuwa namna gani.
84:14Juzuu 30 · uk. 589

إِنَّهُ ظَنَّ أَنْ لَنْ يَحُورَ14

Alidhani hatarudi kwa Muumba wake, akiwa hai, kwa kuhesabiwa.
84:15Juzuu 30 · uk. 589

بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا15

Sivyo hivyo! Mwenyezi Mungu Atamrudisha kama alivomuumba na kumlipa kwa amali zake. Kwani Yeye kwake ni Mtambuzi na kwa hali yake ni Mjuzi kuanzia Alipomuumba mpaka kumfufua.
84:16Juzuu 30 · uk. 589

فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ16

Mwenyezi Mungu Ameapa kwa wekundu wa pambizo za mbingu wakati wa kutwa jua.
84:17Juzuu 30 · uk. 589

وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ17

Na kwa usiku na viunbe tofauti - tofauti vya kutambaa, kuruka na kutembea kwa miguu, uliokusanya.
84:18Juzuu 30 · uk. 589

وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ18

Na kwa mwezi ukamilikapo mwangaza wake.
84:19Juzuu 30 · uk. 589

لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَنْ طَبَقٍ19

Mtapitia, enyi watu, miongo mbalimbali na hali tofauti :kutoka kwenye tone la manii, kuptia pande la damu, nofu la nyama hadi kutiwa roho, mpaka kufa na mpaka kufufuliwa. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, afanyapo hilo atakuwa ameingia kwenye ushirikina.
84:20Juzuu 30 · uk. 589

فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ20

Ni kitu gani kinachowazuia kumwamini baada ya aya zake kufafanuliwa kwao?
84:21Juzuu 30 · uk. 589

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩21

Na wana nini wao wanaposomewa Qur’ani hawamsujudii Mwenyezi Mungu wala hawajisalimishi kufuata yaliyokuja ndani yake?
84:22Juzuu 30 · uk. 589

بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ22

Hakika tabia ya waliokufuru ni kuikanusha na kuikataa haki.
84:23Juzuu 30 · uk. 589

وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ23

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa ukaidi wao wanaouficha kwenye nyoyo zao hali wao wanajua kuwa yale yaliyoletwa na Qur’ani ni kweli.
84:24Juzuu 30 · uk. 589

فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ24

Basi wape bishara, ewe Mtume, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Amewaandalia adhabu yenye uchungu.
84:25Juzuu 30 · uk. 590

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ25

Lakini wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakatekeleza amri waliyofaradhiwa na Mwenyezi Mungu watakuwa na malipo, Siku ya Akhera, yasiyokatika wala kupungua.

Cheza kutoka mwanzo wa sura