Ash-Shams

سورة الشمس

Sura 91 · Makki · 15 aya

91:1Juzuu 30 · uk. 595

وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa jua na mchana wake na mwangaza wake wa asubuhi.
91:2Juzuu 30 · uk. 595

وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا2

Na kwa mwezi unapolifuata wakati wa kucha na kutwa.
91:3Juzuu 30 · uk. 595

وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا3

Na kwa mchana unapoliondoa giza na kulifunua.
91:4Juzuu 30 · uk. 595

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا4

Na kwa usiku unapoifinika ardhi ikawa giza.
91:5Juzuu 30 · uk. 595

وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا5

Na kwa mbingu na kujengeka kwake kiimara.
91:6Juzuu 30 · uk. 595

وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا6

Na kwa ardhi na kutandikika kwake.
91:7Juzuu 30 · uk. 595

وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا7

Na kwa kila nafsi na namna Mwenyezi Mungu alivyoikamilisha umbo lake ili itekeleze kazi iliyoumbiwa nayo.
91:8Juzuu 30 · uk. 595

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا8

Akaibainishia njia ya shari na njia ya kheri.
91:9Juzuu 30 · uk. 595

قَدْ أَفْلَحَ مَنْ زَكَّاهَا9

Amefaulu mwenye kuisafisha na kuikuza kwa kheri.
91:10Juzuu 30 · uk. 595

وَقَدْ خَابَ مَنْ دَسَّاهَا10

Na ameingia kwenye hasara mwenye kuitia nafsi yake kwenye maasia.
91:11Juzuu 30 · uk. 595

كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا11

Kabila la Thamūd lilimkanusha Nabii wake kwa kuvama kwenye uasi.
91:12Juzuu 30 · uk. 595

إِذِ انْبَعَثَ أَشْقَاهَا12

Pindi walipotoka wabaya zaidi wa kabila hilo kumchinja Ngamia. Mtume wa Mwenyezi Mungu’ Ṣāliḥ, amani imshukie,
91:13Juzuu 30 · uk. 595

فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ نَاقَةَ اللَّهِ وَسُقْيَاهَا13

akawaambia: «Tahadharini kumgusa kwa ubaya ngamia ambaye ni miujiza ilioletwa na Mwenyezi Mungu kwenu inayoonyesha ukweli wa Nabii wenu, na msizuie kinywaji chake. Yeye ana siku yake ya kunywa na nyinyi mna siku yenu maalumu ya kunywa.» Hilo likawa zito kwao.
91:14Juzuu 30 · uk. 595

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُمْ بِذَنْبِهِمْ فَسَوَّاهَا14

Wakamkanusha na kulipuza onyo lake wakamchinja.Mola wao Akawafinika kwa adhabu, akaisawazisha juu yao na hakuna aliyeweza kuponyoka.
91:15Juzuu 30 · uk. 595

وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا15

Wala Haogopi, Mwenye uwezo uliotukuka, athari ya adhabu kali Aliywateremshia.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Yasser Salama - Ash-Shams · Tlawati