Al-Fajr

سورة الفجر

Sura 89 · Makki · 30 aya

89:1Juzuu 30 · uk. 593

وَالْفَجْرِ1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa alfajiri
89:2Juzuu 30 · uk. 593

وَلَيَالٍ عَشْرٍ2

na masiku kumi ya kwanza ya Mfungotatu na kwa kile kilichoyafanya yawe matukufu,
89:3Juzuu 30 · uk. 593

وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ3

kwa kila idadi igawanyikayo na isiyogawanyika,
89:4Juzuu 30 · uk. 593

وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ4

kwa usiku upitapo na giza lake.
89:5Juzuu 30 · uk. 593

هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِذِي حِجْرٍ5

Kwani hakuna katika kiapo kiliyotajwa chenye kukinaisha kwa mwenye akili?
89:6Juzuu 30 · uk. 593

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ6

Huoni, ewe Mtume, vipi Mola wako
89:7Juzuu 30 · uk. 593

إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ7

Alivyoiangamiza kaumu ya Ād'. kabila la Irama lenye nguvu na majengo yaliyoinuliwa juu ya vipia,
89:8Juzuu 30 · uk. 593

الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ8

ambalo hakukuumbwa mfano wake katika miji, kwa ukubwa wa miili na wingi wa nguvu?
89:9Juzuu 30 · uk. 593

وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ9

Na vipi Alivyowafanya Thamūd, kaumu ya Ṣāliḥ, ambao waliweza kuchonga jabali na kufanya nyumba ndani yake?
89:10Juzuu 30 · uk. 593

وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ10

Na vipi Alivyomfanya Firauni, mfalme wa Misri, aliyekuwa na askari waliouhami ufalme wake na kuutilia nguvu.
89:11Juzuu 30 · uk. 593

الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ11

Hawa ndio waliokitumia nguvu na kudhulumu mijini.
89:12Juzuu 30 · uk. 593

فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ12

Wakaeneza humo, kwa dhuluma zao, uharibifu.
89:13Juzuu 30 · uk. 593

فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ13

Mwenyezi Mungu Akawamiminia adhabu kali.
89:14Juzuu 30 · uk. 593

إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ14

Hakika Mola wako,ewe Mtume, Anamwangalia mwenye kumuasi kwa kumpa muhula kidogo, kisha Humpatiliza kwa uwezo na ushindi..
89:15Juzuu 30 · uk. 593

فَأَمَّا الْإِنْسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ15

Huyu binadamu, Mola wake Anapompa mtihani wa neema, Anapomkunjulia riziki yake na kumpa maisha mazuri, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye ana cheo kwa Mola wake na huwa akisema :»Mola wangu Amenitukuza.»
89:16Juzuu 30 · uk. 593

وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ16

Na Anapomuonja na Akambania riziki yake, huwa akidhani kuwa hayo ni kwa kuwa yeye amefanywa mnyonge na Mwenyezi Mungu na huwa akisema: «Mola wangu Amenifanya mnyonge.».
89:17Juzuu 30 · uk. 593

كَلَّا ۖ بَلْ لَا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ17

Hali ya mambo si kama anavyodhania binadamu huyu, kwani mtu hutukuzwa kwa kumtii Mwenyzi Mungu na hufanywa mnyonge kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamwakirimu mayatima na kuwatendea wema.
89:18Juzuu 30 · uk. 593

وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ18

Wala hamhimizani kulisha maskini.
89:19Juzuu 30 · uk. 593

وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَمًّا19

Na mnakula haki za watu, katika kurithi, kwa pupa.
89:20Juzuu 30 · uk. 593

وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا20

Na mnapenda mali kupita kiasi.
89:21Juzuu 30 · uk. 593

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا21

Basi hali zenu zisiwe namna hiyo. Kumbukeni pindi ardhi itakapotikiswa na kuvunjwavunjwa.
89:22Juzuu 30 · uk. 593

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا22

Na Akaja Mola wako kutoa uamuzi kwa waja Wake hali Malaika wamepiga safu.
89:23Juzuu 30 · uk. 594

وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنْسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ23

Na ukaletwa, Siku Hiyo kubwa, moto wa Jahanamu. Hiyo ndiyo Siku kafiri atakumbuka na kutubia. Kutamfalia nini sasa kukumbuka kwake na kutubia, na yeye katika ulimwengu alikuwa ameyapuuza hayo, na wakati wake umekwisha kupita?
89:24Juzuu 30 · uk. 594

يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي24

Atakuwa akisema: ‘Laiti mimi nilitanguliza ulimwenguni amali zenye kunifaa katika maisha yangu ya Akhera’.
89:25Juzuu 30 · uk. 594

فَيَوْمَئِذٍ لَا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ25

Katika Siku Hiyo ngumu yenye vituko, hakuna atakaye kuweza kuadhibu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa anayemuasi.
89:26Juzuu 30 · uk. 594

وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ26

Na hakuna atakaye kuweza kufunga kama kifungo Chake wala kufikia hadi yake.
89:27Juzuu 30 · uk. 594

يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ27

Ewe nafsi iliyotulia kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, kumwamini Yeye na kuamini starehe ya Pepo Aliyowaandalia waumini!
89:28Juzuu 30 · uk. 594

ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَرْضِيَّةً28

Rudi kwa Mola wako hali ya kuridhika na takrima ya Mwenyezi Mungu kwako na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ameridhika na wewe.
89:29Juzuu 30 · uk. 594

فَادْخُلِي فِي عِبَادِي29

Ingia miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu walio wema
89:30Juzuu 30 · uk. 594

وَادْخُلِي جَنَّتِي30

na ingia kwenye Pepo yangu.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Jibreel - Al-Fajr · Tlawati