Az-Zalzalah

سورة الزلزلة

Sura 99 · Madani · 8 aya

99:1Juzuu 30 · uk. 599

إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا1

Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.
99:2Juzuu 30 · uk. 599

وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا2

Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandi.
99:3Juzuu 30 · uk. 599

وَقَالَ الْإِنْسَانُ مَا لَهَا3

Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?»
99:4Juzuu 30 · uk. 599

يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا4

Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya.
99:5Juzuu 30 · uk. 599

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا5

kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa.
99:6Juzuu 30 · uk. 599

يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ6

Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo.
99:7Juzuu 30 · uk. 599

فَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ7

Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera.
99:8Juzuu 30 · uk. 599

وَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ8

Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Ayyub - Az-Zalzalah · Tlawati