At-Tariq

سورة الطارق

Sura 86 · Makki · 17 aya

86:1Juzuu 30 · uk. 591

وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu na nyota yenye kuchomoza usiku.
86:2Juzuu 30 · uk. 591

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ2

Na ni lipi lilokujulisha ni ukubwa gani wa nyota hiyo?
86:3Juzuu 30 · uk. 591

النَّجْمُ الثَّاقِبُ3

Hiyo ni nyota ing’arao na kuzagaa.
86:4Juzuu 30 · uk. 591

إِنْ كُلُّ نَفْسٍ لَمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ4

Hakuna nafsi yoyote isipokuwa amewakilishwa kwayo Malaika mwenye kuchunguza na kusjili amali zake ili ihesabiwe Siku ya Kiyama.
86:5Juzuu 30 · uk. 591

فَلْيَنْظُرِ الْإِنْسَانُ مِمَّ خُلِقَ5

Basi aangalie binadamu mwenye kukanusha kufufuliwa ameumbwa kwa kitu gani? Ili ajue kuwa kurudisha umbo lake mara ya pili si vigumu kama kuumbwa mara ya kwanza.
86:6Juzuu 30 · uk. 591

خُلِقَ مِنْ مَاءٍ دَافِقٍ6

Aliumbwa kwa manii yenye kupenyeza ndani ya uzao kwa haraka.
86:7Juzuu 30 · uk. 591

يَخْرُجُ مِنْ بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ7

Yatokayo kwenye mgongo wa mwnamume na kifua cha mwanamke.
86:8Juzuu 30 · uk. 591

إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ8

Hakika yule Aliyemuumba binadamu kwa maji haya ni muweza wa kumrudisha kwenye uhai baada ya kufa.
86:9Juzuu 30 · uk. 591

يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ9

Siku zitakapofunuliwa wazi siri ziliofichwa na nafsi na kupambanuliwa njema na mbovu.
86:10Juzuu 30 · uk. 591

فَمَا لَهُ مِنْ قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ10

Binadamu hatakuwa na nguvu ya kuitetea nafsi yake wala hatakuwa na mtetezi wa kumwepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu.
86:11Juzuu 30 · uk. 591

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ11

Na Anaapa kwa mbingu yenye mvua ya kukaririka.
86:12Juzuu 30 · uk. 591

وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ12

Na ardhi yenye pasuko za kufanya mimea ichipuke.
86:13Juzuu 30 · uk. 591

إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ13

Hakika Qur’ani ni neno lenye kupambanua baina ya haki na batili.
86:14Juzuu 30 · uk. 591

وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ14

Na si upuuzi. Haifai kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Akifanya hivyo atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu.
86:15Juzuu 30 · uk. 591

إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا15

Hakika wenye kumkanusha Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani wanafanya vitimbi na mipango ili kuipinga haki na kuitilia nguvu batili.
86:16Juzuu 30 · uk. 591

وَأَكِيدُ كَيْدًا16

Na Mimi nafanya vitimbi kuidhihirisha haki ingawa makafiri wanatukia.Usiwe na haraka nao, ewe Mtume, kutaka wateremshiwe adhabu.
86:17Juzuu 30 · uk. 591

فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا17

Wape muhula uwangojee muda mchache wala usiwafanyie haraka, utaona adhabu itakayowafikia, mateso na maangamivu.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Ayyub - At-Tariq · Tlawati