Al-Infitar

سورة الإنفطار

Sura 82 · Makki · 19 aya

82:1Juzuu 30 · uk. 587

إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ1

Pindi mbingu zitakapopasuka na ukaharibika mpango wake.
82:2Juzuu 30 · uk. 587

وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انْتَثَرَتْ2

Na pindi nyota zitakapoangukiana.
82:3Juzuu 30 · uk. 587

وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ3

Na pindi Mwenyezi Mungu Atakapozifanya bahari kulipuka na maji yake kutoweka.
82:4Juzuu 30 · uk. 587

وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ4

Na pindi makaburi yatakapogeuzwa kwa kufufuliwa waliokuwamo ndani yake.
82:5Juzuu 30 · uk. 587

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ5

Wakati huo itajua kila nafsi vitendo vyake vyote ilivyovifanya, vilivyotangulia na vilivyoahirika na italipwa kwa vitendo hivyo.
82:6Juzuu 30 · uk. 587

يَا أَيُّهَا الْإِنْسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ6

Ewe binadamu unayekanusha kufufuliwa! Ni kipi kilichokufanya uhadaike na ughurike kuhusu Mola wako Mpaji Mwenye kheri nyingi, Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa?
82:7Juzuu 30 · uk. 587

الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ7

Kwani si Yeye Aliyekuumba, Akalisawazisha umbo lako, Akakuweka katika hali ya sawa na Akakurekibisha ili uweze kutekeleza nyadhifa zako,
82:8Juzuu 30 · uk. 587

فِي أَيِّ صُورَةٍ مَا شَاءَ رَكَّبَكَ8

katika sura yoyote ile Aliyoitaka Akakuumba?
82:9Juzuu 30 · uk. 587

كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ9

Mambo hayako kama vile mnavyosema kwamba nyinyi mna haki ya kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Hesabu na Malipo.
82:10Juzuu 30 · uk. 587

وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ10

Na mjue kuwa wako na nyinyi Malaika wachunguzi,
82:11Juzuu 30 · uk. 587

كِرَامًا كَاتِبِينَ11

watukufu kwa Mwenyezi Mungu, waandishi wa yale waliyowakilishwa kuyadhibiti. Hakiwapiti, katika vitendo vyenu na siri zenu, chochote.
82:12Juzuu 30 · uk. 587

يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ12

Wanayajua mnayoyafanya, ya kheri au ya shari.
82:13Juzuu 30 · uk. 587

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ13

Hakika wachamungu wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa kwenye neema.
82:14Juzuu 30 · uk. 587

وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ14

Hakika watu waovu waliopuuza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake watakuwa katika Moto mkali.
82:15Juzuu 30 · uk. 587

يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ15

Ukali wake, Moto huo, utawapata Siku ya Malipo.Na wala wao hawatakuwa ni wenye kughibu,
82:16Juzuu 30 · uk. 587

وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ16

wakawa hawamo ndani ya Moto wa Jahanamu, si kwa kutoka wala kwa kufa.
82:17Juzuu 30 · uk. 587

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ17

Ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu?
82:18Juzuu 30 · uk. 587

ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ18

Kisha ni kipi kinachokujuza ni upi utukufu wa Siku ya Hesabu?
82:19Juzuu 30 · uk. 587

يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِنَفْسٍ شَيْئًا ۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِلَّهِ19

Siku ya Hesabu, hataweza yoyote kumnufaisha yoyote. Na amri zote Siku Hiyo ni za Mwenyezi Mungu Peke yake Ambaye hakuna mwenye kumshinda, wala hakuna mwenye kumtendesha nguvu, wala hakuna mwenye kushindana na Yeye.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Ayyub - Al-Infitar · Tlawati