Al-Qiyamah

سورة القيامة

Sura 75 · Makki · 40 aya

75:1Juzuu 29 · uk. 577

لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ1

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Hesabu na Malipo,
75:2Juzuu 29 · uk. 577

وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ2

na Anaapa kwa nafsi yenye kuamini na kuchamungu, inayomlaumu mwenyewe kwa kuacha matendo ya utiifu na kufanya matendo yenye kuangamiza, kwamba watu watafufuliwa.
75:3Juzuu 29 · uk. 577

أَيَحْسَبُ الْإِنْسَانُ أَلَّنْ نَجْمَعَ عِظَامَهُ3

Je anadhanihuyu binadamu kafiri kuwa sisi hatutaweza kuikusanya mifupa yake baada ya kuwa mbalimbali.?
75:4Juzuu 29 · uk. 577

بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَنْ نُسَوِّيَ بَنَانَهُ4

Ndio! Tutaikusanya na tunaweza kufanya vidole vyake au ncha za vidole vyake- baada ya kuvikusanya na kuzioanisha- viwe kwenye umbo la sawasawa, kama vilivyokuwa kabla ya kufa.
75:5Juzuu 29 · uk. 577

بَلْ يُرِيدُ الْإِنْسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ5

Bali binadamu anakanusha kufufuliwa, anataka asalie kwenye kufanya ubaya kwa siku za mbeleni za maisha yake.
75:6Juzuu 29 · uk. 577

يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ6

Kafiri huyu huwa akiuliza, akiliona jambo la kusimama Kiyama kuwa liko mbali, «Ni lini Siku ya Kiyama?’
75:7Juzuu 29 · uk. 577

فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ7

Basi macho yatakapoduwaa na yakashituka kwa kutishika na kile yalichokiona cha vituko vya Siku ya Kiyama,
75:8Juzuu 29 · uk. 577

وَخَسَفَ الْقَمَرُ8

na ukafutika mwangaza wa mwezi,
75:9Juzuu 29 · uk. 577

وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ9

na vikakusanywa jua na mwezi katika kukosa mwangaza, kikawa kila mojawapo ya hivyo viwili hakina mwangaza,
75:10Juzuu 29 · uk. 577

يَقُولُ الْإِنْسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ10

wakati huo binadamu atasema, «Pa kukimbilia ni wapi kuiepuka adhabu?»
75:11Juzuu 29 · uk. 577

كَلَّا لَا وَزَرَ11

Mambo sivyo kama unavyotamani yawe, ewe binadamu, ya kutaka kukimbia. Huna mahali pa kukimbilia wala pa kupata uokozinfsi yake.
75:12Juzuu 29 · uk. 577

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ12

Kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake ndio mwisho wa viumbe Siku ya Kiyama na ndipo mahali pao pa kutulia, na hapo Amlipe kila mtu kwa kile alichostahiki.
75:13Juzuu 29 · uk. 577

يُنَبَّأُ الْإِنْسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ13

Atapashwa habari binadamu Siku hiyo kwa matendo yake yote, mema na mabaya, aliyoyatanguliza miongoni mwa hayo katika maisha yake na aliyoyachelewesha.
75:14Juzuu 29 · uk. 577

بَلِ الْإِنْسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ14

Bali binadamu ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake, yenye kumfuata kwa alichokitenda na alichokiacha,
75:15Juzuu 29 · uk. 577

وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ15

hata kama atakuja na kila udhuru wa kuelezea sababu ya uhalifu wake, hilo halitamfaa.
75:16Juzuu 29 · uk. 577

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ16

Usitikise, ewe Nabii, ulimi wako kwa Qur’ani wakati wahyi unapoteremka ili ufanye haraka kuihifadhi kwa kuogopa isikuponyoke.
75:17Juzuu 29 · uk. 577

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ17

Kwani ni juu yetu sisi kuikusanya kwenye kifua chako kisha uisome kwa ulimi wako wakati utakapo. Mjumbe wetu Jibrili akikusomea,
75:18Juzuu 29 · uk. 577

فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ18

basi kisikilize kisomo chake na umpulikize. Kisha isome kama alivyokusomea,
75:19Juzuu 29 · uk. 577

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ19

kisha ni juu yetu kukuelezea kilichokutatiza kukifahamu katika maana yake na hukumu zake.
75:20Juzuu 29 · uk. 578

كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ20

Mambo sivyo kama mlivyodai, enyi mkusanyiko wa washirikina, kuwa hakuna kufufuliwa wala kulipwa.
75:21Juzuu 29 · uk. 578

وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ21

Bali nyinyi ni watu mnaopenda dunia na pambo lake na mnaacha Akhera na starehe zake.
75:22Juzuu 29 · uk. 578

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَاضِرَةٌ22

Nyuso za watu wema Siku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kung’ara, nzuri na zenye furaha,
75:23Juzuu 29 · uk. 578

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ23

zitamuona Mola Aliyeziumba na Anayezimiliki, na zitastarehe kwa hilo.
75:24Juzuu 29 · uk. 578

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ24

Nyuso za watu wabaya Silku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kukunjana na kusinyaa,
75:25Juzuu 29 · uk. 578

تَظُنُّ أَنْ يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ25

zinatazamia kushukiwa na msiba mkubwa wenye kuvunja.
75:26Juzuu 29 · uk. 578

كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ26

Ni kweli! Pindi roho itakapofika sehemu za juu za kifua,
75:27Juzuu 29 · uk. 578

وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ27

na wakasema baadhi ya waliohudhuria kuwaambia wengine, «Je kuna mtu wa kumzungua na kumpoza kutokana na hali hii aliyonayo?»
75:28Juzuu 29 · uk. 578

وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ28

Na yule ambaye yuko katika hali ya kufa akajua kwamba lile lililomshukia ni kuaga dunia, kwa kuwa anawaona Malaika wa mauti.
75:29Juzuu 29 · uk. 578

وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ29

Na ikashikana shida ya mwisho wa duniani na shida ya mwanzo wa Akhera. Kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka.
75:30Juzuu 29 · uk. 578

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ30

Watu watapelekwa Siku ya Kiyama: ima Peponi au Motoni.
75:31Juzuu 29 · uk. 578

فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ31

Hakuwa kafiri ni mwenye kumuamini Mtume na Qur’ani, wala hakuwa ni mwenye kumtekelezea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Swala za faradhi.
75:32Juzuu 29 · uk. 578

وَلَٰكِنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ32

Lakini aliikanusha Qur’ani na akaipa mgongo Imani,
75:33Juzuu 29 · uk. 578

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ33

kisha akaenda kwa watu wake akijiona hali ya kujigamba katika kutembea kwake. Basi maangamivu
75:34Juzuu 29 · uk. 578

أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ34

ni yako baada ya maangamivu!
75:35Juzuu 29 · uk. 578

ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ35

Kisha maangamivu ni yako baada ya maangamivu!
75:36Juzuu 29 · uk. 578

أَيَحْسَبُ الْإِنْسَانُ أَنْ يُتْرَكَ سُدًى36

Je anadhani huyu binadamu anayekanusha kufufuliwa kuwa ataachwa bure: haamrishwi wala hakatazwi, hahesabiwi wala hateswi?
75:37Juzuu 29 · uk. 578

أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِنْ مَنِيٍّ يُمْنَىٰ37

Kwani hakuwa binadamu huyu ni tone la manii dhaifu linalotokana na maji matwevu yanayomwagwa na kumiminwa kwenye kizazi,
75:38Juzuu 29 · uk. 578

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ38

kisha yakawa ni kipande cha damu iliyo kavu. Mwenyezi Mungu Akaliumba kwa uweza Wake na Akazilinganisha sura zake katika umbo la mwili lililo zuri kabisa?
75:39Juzuu 29 · uk. 578

فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنْثَىٰ39

Akafanya kutokana na binadamu huyu jinsi mbili: ya kiume na ya kike. Je kwani hakuwa Mola huyo Muumba wa vitu hivyo ni Muweza wa kuwarudisha viumbe wakiwa hai baada ya kutoweka kwao.
75:40Juzuu 29 · uk. 578

أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَنْ يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ40

Ndio! Anaweza. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hakika ni Muweza wa hilo.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Ayyub - Al-Qiyamah · Tlawati