Al-Qari'ah

سورة القارعة

Sura 101 · Makki · 11 aya

101:1Juzuu 30 · uk. 600

الْقَارِعَةُ1

Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vituko vyake.
101:2Juzuu 30 · uk. 600

مَا الْقَارِعَةُ2

Ni kitu gani hiko chenye kugonga?
101:3Juzuu 30 · uk. 600

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ3

Na ni lipi lililokujulisha ni kipi hiko chenye kugonga?
101:4Juzuu 30 · uk. 600

يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ4

Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama pandzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni.
101:5Juzuu 30 · uk. 600

وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنْفُوشِ5

Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika.
101:6Juzuu 30 · uk. 600

فَأَمَّا مَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ6

Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito,
101:7Juzuu 30 · uk. 600

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَاضِيَةٍ7

atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi.
101:8Juzuu 30 · uk. 600

وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ8

Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito,
101:9Juzuu 30 · uk. 600

فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ9

makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu.
101:10Juzuu 30 · uk. 600

وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ10

Ni lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah»?
101:11Juzuu 30 · uk. 600

نَارٌ حَامِيَةٌ11

Ni Moto unaowaka sana kwa kuni ziliomo ndani yake.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Ayyub - Al-Qari'ah · Tlawati