Al-A'la

سورة الأعلى

Sura 87 · Makki · 19 aya

87:1Juzuu 30 · uk. 591

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى1

Takasa Jina la Mola wako Aliyetukuka na kuepukana na mshirika na kila sifa pungufu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na utakatifu Wake.
87:2Juzuu 30 · uk. 591

الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ2

Aliyeumba viumbe Akalitengeneza umbo lao na kulifanya zuri.
87:3Juzuu 30 · uk. 591

وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ3

Na Aliyekadiria kila kitu na kukipeleka njia inayonasibiana nacho.
87:4Juzuu 30 · uk. 591

وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ4

Na Aliyeotesha nyasi mbiti zenye rangi ya kijani,
87:5Juzuu 30 · uk. 591

فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ5

Akazifanya baadaye kuwa kavu zilizobadilika rangi.
87:6Juzuu 30 · uk. 591

سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنْسَىٰ6

Tutakusomea, ewe Mtume, hii Qur’ani kisomo ambacho hutakisahau.
87:7Juzuu 30 · uk. 591

إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ7

Isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Ataka usahau kwa hekima na maslahi anayoyajua Yeye. Kwani Yeye ni Mjuzi wa yaliyo wazi na yaliyofichika, ya maneno na ya vitendo.
87:8Juzuu 30 · uk. 591

وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ8

Tutakufanyia mapesi mambo yako yote; miongoni mwayo ni kukusahilishia kubeba majukumu ya utume na kuifanya nyepesi Dini uliyokuja nayo.
87:9Juzuu 30 · uk. 591

فَذَكِّرْ إِنْ نَفَعَتِ الذِّكْرَىٰ9

Basi wawaidhie kaumu zako, ewe Mtume, kwa namna tulivyokutayarishia ufanye kwenye wahyi ulioletewa, uwaongoze njia yenye kheri na wao na uwahusu kwa mawaidha yako wale wanaotarajiwa kuwaidhika nayo. Wala usijisumbue kuwashauri wale ambao mawidha hayawaathiri isipokuwa kuwatia ujeuri na kuwafanya wayakimbie.
87:10Juzuu 30 · uk. 591

سَيَذَّكَّرُ مَنْ يَخْشَىٰ10

Atanufaika kwa mawaidha anayemcha Mola wke,
87:11Juzuu 30 · uk. 592

وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى11

na atajiepusha na mawaidha aliye mbaya asiyemuogopa Mola wake
87:12Juzuu 30 · uk. 592

الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ12

atakayeingia kwenye Moto wa Jahanamu akiadhibika kwa ukali wake.
87:13Juzuu 30 · uk. 592

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ13

Kisha hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika wala ni mwenye kuishi akanufaika.
87:14Juzuu 30 · uk. 592

قَدْ أَفْلَحَ مَنْ تَزَكَّىٰ14

Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake na tabia mbovu,
87:15Juzuu 30 · uk. 592

وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ15

na akamtaja Mwenyezi Mungu, akampwekesha, akamuomba, akafanya vitendo vya kumridhisha na akasimamisha Swala kwa nyakati zake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kufuata sheria Aliyoiweka.
87:16Juzuu 30 · uk. 592

بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا16

Hakika yenu, nyinyi watu, mnafadhilisha pambo la maisha ya kilimwengu juu ya starehe za Akhera.
87:17Juzuu 30 · uk. 592

وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ17

Na hakika ya mambo ni kuwa nyumba ya Akhera na starehe zake ni bora zaidi kuliko ulimwngu na ni yenye kusalia zaidi.
87:18Juzuu 30 · uk. 592

إِنَّ هَٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ18

Haya mlioosimuliwa ndani ya Sura hii ni miongoni mwa yaliyotajwa kimaana katika Kurasa zilizotangulia kuteremshwa kabla ya Qur’ani.
87:19Juzuu 30 · uk. 592

صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ19

Nazo ni Kurasa za Ibrāhīm na Mūsā, amani ziwashukie.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Abdulkarim - Al-A'la · Tlawati