Al-Haqqah

سورة الحاقة

Sura 69 · Makki · 52 aya

69:1Juzuu 29 · uk. 566

الْحَاقَّةُ1

Kiyama chenye kutukia kikweli ambacho ndani yake inahakikika ahadi ya Mwenyezi Mungu na onyo Lake.
69:2Juzuu 29 · uk. 566

مَا الْحَاقَّةُ2

Kiyama chenye kutukia kikweli ni zipi sifa zake na hali zake?
69:3Juzuu 29 · uk. 566

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحَاقَّةُ3

Na kitu gani kilichokujulisha wewe, ewe Mtume, na kukueleza uhakika wa Kiyama na kikakupa wewe picha ya janga lake na shida zake?
69:4Juzuu 29 · uk. 566

كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌ بِالْقَارِعَةِ4

Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, na ‘Ād, nao ni watu wa Hūd, walikikanusha Kiyama ambacho kinagonga nyoyo kwa vituko janga lake.
69:5Juzuu 29 · uk. 566

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ5

Ama hao Thamūd waliangamizwa kwa ukelele mkubwa uliopita kiasi ukali wake,
69:6Juzuu 29 · uk. 566

وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ6

na ama‘Ād waliangamizwa kwa upepo baridi unaovuma kwa nguvu.
69:7Juzuu 29 · uk. 566

سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَانِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى الْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ7

Mwenyezi Mungu Aliwasaliti nao masiku saba na michana minane yenye kufuatana, isiyokatika wala kusimama. Utawaona watu katika masiku hayo na michana wamekufa, kama kwamba wao ni vigogo mitende iliyo mibovu iliyolika ndani.
69:8Juzuu 29 · uk. 566

فَهَلْ تَرَىٰ لَهُمْ مِنْ بَاقِيَةٍ8

Basi je utamuona mtu yoyote miongoni mwao mwenye kusalia bila kuangamia?
69:9Juzuu 29 · uk. 567

وَجَاءَ فِرْعَوْنُ وَمَنْ قَبْلَهُ وَالْمُؤْتَفِكَاتُ بِالْخَاطِئَةِ9

Na akaja mpita kiasi katika uasi Fir’awn na ummah waliomtangulia waliokanusha Mitume wao, na watu wakazi wa vijiji vya watu wa Lūṭ ambao majumba yao yaliwapindukia kwa sababu ya kitendo kibaya walichokifanya, cha ukafiri, ushirikina na mambo machafu.
69:10Juzuu 29 · uk. 567

فَعَصَوْا رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَابِيَةً10

Kila ummah kati yao walimuasi mjumbe wa Mola wao ambaye alitumwa kwao, basi Mwenyezi Mungu Akawashika mshiko mkali mno.
69:11Juzuu 29 · uk. 567

إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ11

Sisi, maji yalipopita kipimo chake, mpaka yakawa juu na kuangatika juu ya kila kitu, tuliwabeba watu wa asili zenu pamoja na Nūḥ ndani ya jahazi ambayo ilikuwa ndio sababu ya kuokoka Waumini na kuzamishwa makafiri,
69:12Juzuu 29 · uk. 567

لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَا أُذُنٌ وَاعِيَةٌ12

hili likiwa ni mazingatio na mawaidha, na lipate kulihifadhi tukio hilo kila shikio ambalo kazi yake ni kuhifadhi, na lielewe kile ambacho limekisikia.
69:13Juzuu 29 · uk. 567

فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ نَفْخَةٌ وَاحِدَةٌ13

Pindi Malaika atakapopuliza kwenye barugumu mpulizo mmoja, nao ni mpulizo wa kwanza ambao hapo patapatikana maangamivu ya ulimwengu,.
69:14Juzuu 29 · uk. 567

وَحُمِلَتِ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَاحِدَةً14

Na pindi ardhi na milima itakapoinuliwa kutoka mahali ilipo ikavunjwavunjwa na kugongwagongwa mara moja,
69:15Juzuu 29 · uk. 567

فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ15

Wakati huo Kiyama kitasimama.
69:16Juzuu 29 · uk. 567

وَانْشَقَّتِ السَّمَاءُ فَهِيَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ16

Na mbingu zitafanya ufa na ziwe dhaifu na kulegea Siku hiyo, hazitakuwa na mshikamano wala ugumu.
69:17Juzuu 29 · uk. 567

وَالْمَلَكُ عَلَىٰ أَرْجَائِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ17

Na Malaika watakuwa kwenye pambizo na pande zake, na wataibeba «Arshi ya Mola wako juu yao Siku ya Kiyama Malaika wanane miongoni mwa Malaika wakubwa.
69:18Juzuu 29 · uk. 567

يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنْكُمْ خَافِيَةٌ18

Katika Siku hiyo, mtaorodheshwa kwa Mwenyezi Mungu, enyi wat, ili mhesabiwe na mlipwe, hakuna chochote kitakachofichamana kwa Mwenyewzi Mungu miongoni mwa siri zenu.
69:19Juzuu 29 · uk. 567

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ19

Ama yule Atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwa katika hali ya ubashasha na furaha, ‘Chukueni kitabu changu mkisome!
69:20Juzuu 29 · uk. 567

إِنِّي ظَنَنْتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ20

Mimi nilikuwa na yakini duniani kuwa nitapata malipo yangu Siku ya Kiyama, nikajiandalia nayo kwa matayarisho ya Imani na matendo mema.»
69:21Juzuu 29 · uk. 567

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَاضِيَةٍ21

Basi yeye atakuwa kwenye maisha ya furaha ya kumridhisha;
69:22Juzuu 29 · uk. 567

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ22

kwenye Pepo ya juu kimahali na daraja;
69:23Juzuu 29 · uk. 567

قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ23

matunda yake yako karibu, anayachuma anayesimama, anayeketi na anayelala.
69:24Juzuu 29 · uk. 567

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ24

Wataambiwa, «Kuleni na mnyweni kila aina ya vyakula na vinywaji, mkiwa mbali na kila kero, mkiwa mmesalimika na kila mnalolichukia, kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza siku za ulimwenguni.»
69:25Juzuu 29 · uk. 567

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ25

Na ama yule atakayepewa kitabu cha matendo yake kwa mkono wake wa kushoto,
69:26Juzuu 29 · uk. 567

وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ26

atasema akiwa katika hali ya kujuta na kupata hasara,
69:27Juzuu 29 · uk. 567

يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ27

«Natamani lau mimi sikupewa kitabu changu na sikujua malipo yangu! Natamani lau kile kifo nilichokufa duniani kilikuwa ndicho chenye kukata kabisa mambo yangu na nisifufuliwe baada yake!
69:28Juzuu 29 · uk. 567

مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ۜ28

Mali yangu niliyoyakusanya hayakuninufaisha duniani!
69:29Juzuu 29 · uk. 567

هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ29

Hoja zangu zote zimenionokea, na sina hoja tena ya kuitumia kama hoja.»
69:30Juzuu 29 · uk. 567

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ30

Hapo waambiwe walinzi wa Moto wa Jahanamu, «Mchukueni mhalifu huyu mfanya dhambi, ikusanyeni mikono yake shingoni mwake muitie pingu,
69:31Juzuu 29 · uk. 567

ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ31

kisha mtieni kwenye Moto unaowaka sana, apate kulihisi joto lake.
69:32Juzuu 29 · uk. 567

ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ32

Kisha mfungeni mnyororo wa chuma ambao urefu wake ni dhiraa sabini mumkokote nao na mumtie humo.
69:33Juzuu 29 · uk. 567

إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ33

Kwani yeye hakuwa akiamini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa Haki, Peke Yake, Asiye na mshirika.
69:34Juzuu 29 · uk. 567

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ34

Wala hakuwa akitenda matendo yanayoambatana na uongofu Wake, wala hakuwa akiwahimiza watu duniani kuwalisha wenye uhitaji miongoni mwa masikini na wengineo.
69:35Juzuu 29 · uk. 567

فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ35

basi kafiri huyu Siku ya Kiyama hatakuwa na jamaa wa karibu wa kumuepushia adhabu,
69:36Juzuu 29 · uk. 568

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ36

wala hatakuwa na chakula isipokuwa kile kinachotokana na usaa wa watu wa motoni,
69:37Juzuu 29 · uk. 568

لَا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ37

hakuna mwenye kukila isipokuwa wale wenye dhambi, wanaoshikilia kumkanusha Mwenyezi mungu.
69:38Juzuu 29 · uk. 568

فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ38

Naapa kwa mnavyoviona miongoni mwa vitu vinavyooonekana,
69:39Juzuu 29 · uk. 568

وَمَا لَا تُبْصِرُونَ39

na vile msivyoviona miongoni mwa vile vilivyoghibu kwenu., hakika Qur’ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu.
69:40Juzuu 29 · uk. 568

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ40

Inasomwa na mjumbe mkubwa wa cheo na utukufu.
69:41Juzuu 29 · uk. 568

وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَا تُؤْمِنُونَ41

Na si maneno ya mshairi kama mnavyodai, ni uchache mno mnavyoamini.
69:42Juzuu 29 · uk. 568

وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ42

Wala si tungo kama zile tungo za makuhani, ni kuchache mno kule kukumbuka kwenu na kutia akilini kuwa kuna tafauti baina ya mawili hayo.
69:43Juzuu 29 · uk. 568

تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ43

Lakini hiyo Qur’ani ni maneno ya Mola wa viumbe wote Aliyoyateremshia Mtume Wake Muhaammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
69:44Juzuu 29 · uk. 568

وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ44

Na lau Muhammad angalitusingizia maneno tusiyoyanena
69:45Juzuu 29 · uk. 568

لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ45

tungalimtesa na tungalimkamata kwa nguvu na uweza, kwani nguvu ya kila kitu iko kwenye upande wake wa kulia,
69:46Juzuu 29 · uk. 568

ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ46

kisha tungalimkata mshipa wa moyo wake.,
69:47Juzuu 29 · uk. 568

فَمَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ47

hataweza yoyote kuyazuia mateso yetu yasimpate.
69:48Juzuu 29 · uk. 568

وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِلْمُتَّقِينَ48

Na hii Qur’ani ni mawaidha kwa wachamungu wanaofuata amri za Mwenyezi Mungu na kuyaepuka makatazo yake.
69:49Juzuu 29 · uk. 568

وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنْكُمْ مُكَذِّبِينَ49

Na sisi kwa hakika tunajua kwamba miongoni mwenu kuna wanaoikanusha hii Qur’ani pamoja na kuwa dalili zake ziko wazi.
69:50Juzuu 29 · uk. 568

وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ50

Na kwa hakika kuikanusha Qur’ani ni majuto makubwa kwa wenye kuikanusha pindi watakapoiona adhabu yao na kuona starehe za wenye kuiamini.
69:51Juzuu 29 · uk. 568

وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ51

Na kwa hakika hii Qur’ani ni haki iliyothibiti na yakini isiyo na shaka.
69:52Juzuu 29 · uk. 568

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ52

Basi Mwepushie Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kila sifa isiyonasibiana na haiba Yake, na umtaje kwa jina Lake tukufu.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Abdulkarim - Al-Haqqah · Tlawati