Quraysh

سورة قريش

Sura 106 · Makki · 4 aya

106:1Juzuu 30 · uk. 602

لِإِيلَافِ قُرَيْشٍ1

Oneni ajabu ya mazowea ya Makureshi, amani walionayo, kuwaendea uzuri mambo yao,
106:2Juzuu 30 · uk. 602

إِيلَافِهِمْ رِحْلَةَ الشِّتَاءِ وَالصَّيْفِ2

kupangika na kusahilika misafara yao ya kwenda Yamani kipindi cha kusi na kwenda Shamu kipindi cha kaskazi, ili kuleta vitu wanavyohitajia.
106:3Juzuu 30 · uk. 602

فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَٰذَا الْبَيْتِ3

Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada.
106:4Juzuu 30 · uk. 602

الَّذِي أَطْعَمَهُمْ مِنْ جُوعٍ وَآمَنَهُمْ مِنْ خَوْفٍ4

Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na kicho kikubwa na babaiko.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Muhammad Abdulkarim - Quraysh · Tlawati