Al-Buruj

سورة البروج

Sura 85 · Makki · 22 aya

85:1Juzuu 30 · uk. 590

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu zenye njia za kupitia jua na mwezi.
85:2Juzuu 30 · uk. 590

وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ2

Na kwa Siku ya Kiyama ambayo Amewaahidi viumbe kuwa Atawakusanya.
85:3Juzuu 30 · uk. 590

وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ3

Na kwa shahidi, mwenye kutoa ushahidi, na mwenye kutolewa ushahidi juu yake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Anachokitaka. Lakini kiumbe hafai kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina.
85:4Juzuu 30 · uk. 590

قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ4

Wamelaaniwa waliofukua chini ya ardhi shimo kubwa ili kuwatesa Waumini.
85:5Juzuu 30 · uk. 590

النَّارِ ذَاتِ الْوَقُودِ5

Wakawasha moto mkubwa wenye kuni nyingi.
85:6Juzuu 30 · uk. 590

إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ6

Wakawa wamekaa kwenye kingo za shimo hilo.
85:7Juzuu 30 · uk. 590

وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِالْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ7

Wakishuhudia vitendo vya mateso na adhabu wanavyowafanyia Waumini.
85:8Juzuu 30 · uk. 590

وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ8

Na hawakuwatesa mateso hayo isipokuwa wenye kuteswa walikuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu Mshindi Asiyeshindwa, Mhimidiwa wa maneno Yake vitendo Vyake na sifa Zake.
85:9Juzuu 30 · uk. 590

الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ9

Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi Ambaye, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Anashuhudia kila kitu, hakuna kinachofichika kwake.
85:10Juzuu 30 · uk. 590

إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ10

Hakika, wale waliowachoma kwa moto Waumini, wa kike na wa kiume, ili kuwazuia watu na dini ya Mwenyezi Mungu, kisha wasitubie, watapata, Siku ya Akhera, adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu kali yenye kuchoma.
85:11Juzuu 30 · uk. 590

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ11

Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya amali njema, watapata Pepo ambayo chini ya majumba yake ya kifahari yapita mito. Huko ni kufaulu kukubwa.
85:12Juzuu 30 · uk. 590

إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ12

Hakika malipizo ya Mola wako kwa maadui Zake na mateso Yake juu yao ni mazito.
85:13Juzuu 30 · uk. 590

إِنَّهُ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ13

Ndiye Yeye Mwenye kuanzisha kuumba na kisha kurudisha.
85:14Juzuu 30 · uk. 590

وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ14

Ndiye Yeye Mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia, Mwingi wa mapenzi kwa wanaoikurubisha kwake.
85:15Juzuu 30 · uk. 590

ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ15

Mwenye Arshi tukufu.
85:16Juzuu 30 · uk. 590

فَعَّالٌ لِمَا يُرِيدُ16

Mfanya Alitakalo: hakuna kitu Anachotaka kiwe kisiwe.
85:17Juzuu 30 · uk. 590

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْجُنُودِ17

Je, ewe Mtume, imekufikia habari ya makundi yaliyokufuru na kukanusha Mitume walioletwa, ya
85:18Juzuu 30 · uk. 590

فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ18

Firauni na Thamūd, misiba na adhabu iliyowashukia? Hawakuzingatia kwa habari hiyo.
85:19Juzuu 30 · uk. 590

بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي تَكْذِيبٍ19

Bali waliokufuru waendelea kukanusha kwao, kama walivyokuwa waliokuja kabla yao.
85:20Juzuu 30 · uk. 590

وَاللَّهُ مِنْ وَرَائِهِمْ مُحِيطٌ20

Na Mwenyezi Mungu Amewazunguka kwa Ujuzi na Uweza Wake, hakuna chenye kufichika Kwake kuhusu wao na vitendo vyao. Hii Qu’ani siyo kama wanavyodai wenye kukanusha katika washirikina kuwa ni mashairi na uchawi ndipo wakaikanusha.
85:21Juzuu 30 · uk. 590

بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَجِيدٌ21

Bali hii ni Qur’ani kubwa iliyo tukufu,
85:22Juzuu 30 · uk. 590

فِي لَوْحٍ مَحْفُوظٍ22

iliyomo kwenye Ubao Uliohifadhiwa, haufikiwi na kubadilishwa wala kupotoshwa.

Cheza kutoka mwanzo wa sura