Al-Muddaththir

سورة المدثر

Sura 74 · Makki · 56 aya

74:1Juzuu 29 · uk. 575

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ1

Ewe uliojifinika nguo zako!
74:2Juzuu 29 · uk. 575

قُمْ فَأَنْذِرْ2

Inuka kutoka kwenye malazi yako owaonye watu adhabu ya Menyezi Mungu.
74:3Juzuu 29 · uk. 575

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ3

Na umkusudie Mola wako, Peke Yake, kwa kumtukuza, kumpwekesha na kumuabudu.
74:4Juzuu 29 · uk. 575

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ4

Na usafishe nguo zako kutokana na najisi, kwani usafi wa nje ni katika kutimia usafi wa ndani.
74:5Juzuu 29 · uk. 575

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ5

Na uendelee daima kuyaepuka masanamu na mizimu, na matendo ya ushirikina yote usiyakaribie.
74:6Juzuu 29 · uk. 575

وَلَا تَمْنُنْ تَسْتَكْثِرُ6

Na usitoe kitu kumpa mtu kwa lengo la kupata zaidi ya hiko. Na kwa ajili ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu,
74:7Juzuu 29 · uk. 575

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ7

vumilia juu ya maamrisho na makatazo.
74:8Juzuu 29 · uk. 575

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ8

Pindi patakapopulizwa kwenye barugumu mpulizo wa Ufufuzi na Uenezaji,
74:9Juzuu 29 · uk. 575

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ9

wakati huo ni wakati ambao ni mgumu kwa makafiri;
74:10Juzuu 29 · uk. 575

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ10

si rahisi kwao kusalimika na yale walionayo ya kujadiliwa hesabu zao na vituko vingine vikubwa.
74:11Juzuu 29 · uk. 575

ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا11

Niache mimi, ewe Mtume, na huyu niliyemuumba ndani ya tumbo la mamake akiwa peke yake, hana mali wala watoto.
74:12Juzuu 29 · uk. 575

وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَمْدُودًا12

Nikamfanya awe na mali mengi yenye kuenea na watoto waliyoko na yeye hapo Makkah hawamuondokei. Na
74:13Juzuu 29 · uk. 575

وَبَنِينَ شُهُودًا13

nikamsahilishia kwa kumrahisishia njia za maisha. Kisha yeye anatarajia, baada ya vitu hivi alivyopewa,
74:14Juzuu 29 · uk. 575

وَمَهَّدْتُ لَهُ تَمْهِيدًا14

nimuongezee kwenye mali yake na watoto wake na huku yeye amenikanusha. Mambo sivyo kama anavyodai huyu mwenye kuasi, mtenda dhambi.
74:15Juzuu 29 · uk. 575

ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ15

Simuongezei zaidi ya hiko nilichompa,
74:16Juzuu 29 · uk. 575

كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا16

kwa kuwa yeye alikuwa mshindani mkanushaji wa Qur’ani na hoja za Mwenyezi Mungu kwa viumbe Wake.
74:17Juzuu 29 · uk. 575

سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا17

Nitambebesha mateso magumu na usumbufu usio na mapumziko. Anayekusudiwa hapa ni Al-Walid mwana wa Al-Mughi rah aliyekuwa akishindana na haki na akijitokeza kupigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Haya ndiyo malipo ya kila mwenye kushindana na haki na kuipiga vita.
74:18Juzuu 29 · uk. 575

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ18

Kwa kweli yeye aliwaza ndani ya nafsi yake akatayarisha la kusema kumtukana Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani.
74:19Juzuu 29 · uk. 576

فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ19

Hivyo basi akalaaniwa na akastahili, kwa hilo, maangamivu: alijiandaa vipi ndani ya nafsi yake kwa hayo matukano?
74:20Juzuu 29 · uk. 576

ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ20

Kisha pia akalaaniwa.
74:21Juzuu 29 · uk. 576

ثُمَّ نَظَرَ21

Kisha yeye alifikiria kuhusu kile alichokipanga na kukitayarisha cha kuitia dosari Qur’ani.
74:22Juzuu 29 · uk. 576

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ22

Kisha akafinya uso wake na akazidi katika hali ile ya ukunjaji uso kwa kukosa hila za kufanya na kutopata ila yoyote ya kuitia dosari Qur’ani.
74:23Juzuu 29 · uk. 576

ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ23

Kisha akarudi kuipa mgongo haki na akajiona ni mkubwa wa kutofaa kuikubali,
74:24Juzuu 29 · uk. 576

فَقَالَ إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ24

hapo akasema kuhusu Qur’ani, «Haya anayoyasema Muhammad si chochote isipokuwa ni uchawi uliopokewa kutoka kwa watu wa mwanzo waliopita.
74:25Juzuu 29 · uk. 576

إِنْ هَٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ25

Haikuwa hi Qur’ani isipokuwa ni maneno ya viumbe ambayo Muhammad amejifunza kutoka kwao kisha akadai kuwa yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.»
74:26Juzuu 29 · uk. 576

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ26

Basi nitamuingiza kwenye moto wa Jahanamu ili alionje joto lake na achomeke kwa moto wake.
74:27Juzuu 29 · uk. 576

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ27

Na ni lipi lililokujulisha wewe ni kitu gani hiyo Jahanamu?
74:28Juzuu 29 · uk. 576

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ28

Haibakishi nyama wala haiachi mfupa isipokuwa huvichoma.
74:29Juzuu 29 · uk. 576

لَوَّاحَةٌ لِلْبَشَرِ29

Unageuza ngozi ya mwili, unazifanya ngozi kuwa nyeusi na unazichoma.
74:30Juzuu 29 · uk. 576

عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ30

Wanasimamia mambo yake na kushikilia kazi ya kuwatesa watu wake Malaika kumi na tisa katika washika zamu wa Motoni wenye nguvu.
74:31Juzuu 29 · uk. 576

وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ31

Na hatukuwafanya washika hazina wa Motoni isipokuwa miongoni mwa Malaika washupavu. Na hatukuiweka idadi hiyo isipokuwa kuwatahini wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na ili imani ya yakini ipatikane kwa wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu kwamba yaliyokuja ndani ya Qur’ani juu ya washika hazina wa Motoni ni ukweli utokao kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kwani hayo yanaafikiana na vitabu vyao, na ili Waumini wazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na waifuate Sheria Yake kivitendo, na ili wasilifanyie shaka hilo wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu wala wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ili wapate kusema wale wenye unafiki ndani ya nyoyo zao na makafiri, «Ni lipi alilolikusudia Mwenyezi Mungu kwa idadi hii ya ajabu?» Kwa mfano wa hayo yaliyotajwa, Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayetaka kumpoteza na Anamuongoza Anayetaka kumuongoza. Na hakuna ajuwaye idadi ya askari wa Mola wako, na miongoni mwao ni Malaika, isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na haukuwa huu Moto isipokuwa ni ukumbusho na mazingatio kwa watu.
74:32Juzuu 29 · uk. 576

كَلَّا وَالْقَمَرِ32

Mambo sivyo kama walivyotaja ya ukanushaji Mtume katika yale aliyokuja nayo! Anaapa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, kwa mwezi,
74:33Juzuu 29 · uk. 576

وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ33

na kwa usiku unapogeuka kwenda zake,
74:34Juzuu 29 · uk. 576

وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ34

na kwa asubuhi inapotoa mwangaza na kufunuka,
74:35Juzuu 29 · uk. 576

إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ35

hakika Moto ni mojawapo ya mambo makubwa,
74:36Juzuu 29 · uk. 576

نَذِيرًا لِلْبَشَرِ36

kwa ajili ya kuwaonya na kuwatisha watu,
74:37Juzuu 29 · uk. 576

لِمَنْ شَاءَ مِنْكُمْ أَنْ يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ37

kwa anayetaka miongoni mwenu kujiweka karibu na Mola wake kwa kufanya matendo ya utiifu, au kujikalisha nyuma kwa kufanya matendo ya uasi.
74:38Juzuu 29 · uk. 576

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ38

Kila nafsi imefungwa na kuwekwa rahani kwa ilichokitenda, miongoni mwa matendo mema au mabaya, kwa kukichuma. Haifunguliwi mpaka itekeleze haki zilizo juu ya lazima yake na ipatiwe mateso yanayostahili kupatiwa.
74:39Juzuu 29 · uk. 576

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ39

Isipokuwa Waislamu waliotakaswa, watu wa upande wa kulia waliojikomboa shingo zao kwa utiifu.
74:40Juzuu 29 · uk. 576

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ40

Wao watakuwa kwenye mabustani ya Peponi ambayo sifa zake hazifikiwi ukomo. Watakuwa wakiulizana wao kwa wao
74:41Juzuu 29 · uk. 576

عَنِ الْمُجْرِمِينَ41

kuhusu makafiri waliojikosea nafsi zao,
74:42Juzuu 29 · uk. 576

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ42

«Ni lipi lililowaingiza kwenye moto wa Jahanamu na likawafanya
74:43Juzuu 29 · uk. 576

قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ43

mlionje joto lake lililo kali sana?» Wahalifu waseme , «Hatukuwa ni miongoni mwa wanaoswali duniani,
74:44Juzuu 29 · uk. 576

وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ44

na hatukuwa tukitoa sadaka na kuwafanyia wema wahitaji na maskini,
74:45Juzuu 29 · uk. 576

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ45

na tulikuwa tukizungumza maneno ya ubatilifu na watu wa upotofu na upotevu,
74:46Juzuu 29 · uk. 576

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ46

na tulikuwa tukiikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa,
74:47Juzuu 29 · uk. 576

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ47

mpaka kifo kikatujia na hali sisi tuko kwenye mambo hayo mabaya ya upotevu.
74:48Juzuu 29 · uk. 577

فَمَا تَنْفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ48

Basi hayatawafalia neno maombezi ya wenye kuombea wote, miongoni mwa Malaika, Manabii na wengineo, kwa kuwa aombewaye ni yule aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na akamuidhinisha mwenye kumuombea.
74:49Juzuu 29 · uk. 577

فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ49

Basi wana nini hawa washirikina wamejiepusha na Qur’ani na
74:50Juzuu 29 · uk. 577

كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُسْتَنْفِرَةٌ50

mawaidha yaliyomo ndani yake? Kama kwamba wao ni pundamilia wanaobabaika
74:51Juzuu 29 · uk. 577

فَرَّتْ مِنْ قَسْوَرَةٍ51

wanaomkimbia simba mshambulizi.
74:52Juzuu 29 · uk. 577

بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِنْهُمْ أَنْ يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُنَشَّرَةً52

Lakini kila mmoja, miongoni mwa hawa washirikina, ana matumaini ateremshiwe kitabu kutoka mbinguni kilichokunjuliwa kama kile kilichoteremshiwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
74:53Juzuu 29 · uk. 577

كَلَّا ۖ بَلْ لَا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ53

Mambo si hivyo kama wanavyodai. Ukweli ni kwamba wao hawaiogopi Akhera wala hawaamini kuwa kuna kufufuliwa na kulipwa.
74:54Juzuu 29 · uk. 577

كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ54

Ni kweli kwamba Qur’ani ni mawaidha yenye ufasaha, yanayotosha kuwafanya wao wawaidhike.
74:55Juzuu 29 · uk. 577

فَمَنْ شَاءَ ذَكَرَهُ55

Anayetaka kuwaidhika, basi na awaidhike kwa yaliyomo ndani yake na anufaike na uongofu wake.
74:56Juzuu 29 · uk. 577

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ56

Na hawawaidhiki kwayo isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Amewatakia kuongoka. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayestahiki kuogopewa na kutiiwa, na Ndiye Anayestahiki kumsamehe anayemuamini Yeye na kumtii.

Cheza kutoka mwanzo wa sura