Al-Masad

سورة المسد

Sura 111 · Makki · 5 aya

111:1Juzuu 30 · uk. 603

تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ1

Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutu.
111:2Juzuu 30 · uk. 603

مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ2

Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukia.
111:3Juzuu 30 · uk. 603

سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ3

Ataingia kwenye Moto wenye kuroroma,
111:4Juzuu 30 · uk. 603

وَامْرَأَتُهُ حَمَّالَةَ الْحَطَبِ4

yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi.
111:5Juzuu 30 · uk. 603

فِي جِيدِهَا حَبْلٌ مِنْ مَسَدٍ5

Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini.

Cheza kutoka mwanzo wa sura