Al-Humazah

سورة الهمزة

Sura 104 · Makki · 9 aya

104:1Juzuu 30 · uk. 601

وَيْلٌ لِكُلِّ هُمَزَةٍ لُمَزَةٍ1

Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana.
104:2Juzuu 30 · uk. 601

الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ2

Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuyahesabu.
104:3Juzuu 30 · uk. 601

يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ3

Akidhani kuwa mali yake ambayo ameyakusanya yatampa dhamana ya kuishi milele duniani na kuhepa kuhesabiwa.
104:4Juzuu 30 · uk. 601

كَلَّا ۖ لَيُنْبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ4

Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa.
104:5Juzuu 30 · uk. 601

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ5

Lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni upi huo Moto unaovunjavunja?
104:6Juzuu 30 · uk. 601

نَارُ اللَّهِ الْمُوقَدَةُ6

Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.
104:7Juzuu 30 · uk. 601

الَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى الْأَفْئِدَةِ7

Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo.
104:8Juzuu 30 · uk. 601

إِنَّهَا عَلَيْهِمْ مُؤْصَدَةٌ8

Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo
104:9Juzuu 30 · uk. 601

فِي عَمَدٍ مُمَدَّدَةٍ9

na pingu ndefu ili wasitoke.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Mishary Al-Afasy - Al-Humazah · Tlawati