Ad-Duha

سورة الضحى

Sura 93 · Makki · 11 aya

93:1Juzuu 30 · uk. 596

وَالضُّحَىٰ1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima.
93:2Juzuu 30 · uk. 596

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ2

Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likashadidi giza lake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina.
93:3Juzuu 30 · uk. 596

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ3

Hakukuwacha Mola wako, ewe Mtume, wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi.
93:4Juzuu 30 · uk. 596

وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَكَ مِنَ الْأُولَىٰ4

Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu.
93:6Juzuu 30 · uk. 596

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ6

Kwani Hakukupata, kabla ya hapo, kuwa ni yatima Akakukusanya na kukutunza.
93:7Juzuu 30 · uk. 596

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ7

Na Akakupata hujui Kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakuafikia kufanya amali bora?
93:8Juzuu 30 · uk. 596

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ8

Na Akakupata masikini, Akakuletea riziki yako na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri?
93:9Juzuu 30 · uk. 596

فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ9

Basi yatima usimtende ubaya.
93:10Juzuu 30 · uk. 596

وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ10

Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja yake.
93:11Juzuu 30 · uk. 596

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ11

Na ama neema ya Mola wako Aliyokuneemesha nayo izungumze.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Maher Al-Muaiqly - Ad-Duha · Tlawati