An-Nazi'at

سورة النازعات

Sura 79 · Makki · 46 aya

79:1Juzuu 30 · uk. 583

وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا1

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Malaika ambao huzing’oa roho za makafiri mng’oo mkali.
79:2Juzuu 30 · uk. 583

وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا2

Na kwa Malaika ambao huzitukua roho za Waumini kwa uchangamfu na upole.
79:3Juzuu 30 · uk. 583

وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا3

Na kwa Malaika wanaoogelea katika kushuka kwao kutoka mbinguni na kupaa kwao kwenda mbinguni.
79:4Juzuu 30 · uk. 583

فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا4

Na kwa Mlaika ambao wanakimbilia kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu.
79:5Juzuu 30 · uk. 583

فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا5

Na kwa Malaika wanaopitisha amri za Mola wao katika mambo ya ulimwengu waliowakilishwa kuyafanya na kuyasimamia, - Wala haifai kwa kiumbe kukiapia chochote kile, bali yapasa kiapo chake kiwe ni kwa jina la Mola wake Muumba au sifa Zake. Na lau ataapa kwa asiye Muumba wake, basi huyo amekuwa mshirikina - Watafufuliwa viumbe bila shaka na watahesabiwa.
79:6Juzuu 30 · uk. 583

يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ6

Siku ambayo ardhi itatetemeka kwa mvuvuo wa kwanza:
79:7Juzuu 30 · uk. 583

تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ7

mvuvio wa kufisha, ukifuatiwa na mvuvio mwingine wa kuhuisha.
79:8Juzuu 30 · uk. 583

قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ8

Nyoyo za makafiri, Siku hiyo, zitakuwa na papatiko kwa kicho kikubwa.
79:9Juzuu 30 · uk. 583

أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ9

Macho ya makafiri hao yatakuwa madhalilifu kwa kitisho watakachokiona.
79:10Juzuu 30 · uk. 583

يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ10

Wanasema hawa wakanushao kufufuliwa:
79:11Juzuu 30 · uk. 583

أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَخِرَةً11

«Je, tutarudishwa baada ya kufa kwetu kwenye yale tuliyokuwa nayo katika ardhi? Je, tutarudishwa na hali tushakuwa mifupa iliochakaa?»
79:12Juzuu 30 · uk. 583

قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ12

Wakasema: «Kurejea kwetu huko kutakuwa kutupu kusikokuwa kweli.’
79:13Juzuu 30 · uk. 583

فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ13

Hakika tukio hilo litakuwa kwa mvivio mmoja tu.
79:14Juzuu 30 · uk. 583

فَإِذَا هُمْ بِالسَّاهِرَةِ14

Wakitahamaki wao wako hai juu ya ardhi baada ya kuwa walikuwa ndani yake.
79:15Juzuu 30 · uk. 583

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ15

Je imekujilia, ewe Mtume, habari ya Mūsā?
79:16Juzuu 30 · uk. 583

إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى16

Pindi Mola wake Alipomwita katika bonde lililotakaswa na kubarikiwa, la Ṭuwā. Akamwambia:
79:17Juzuu 30 · uk. 584

اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ17

«Enda kwa Firauni. Hakika yeye amekiuka mno katika kuasi.
79:18Juzuu 30 · uk. 584

فَقُلْ هَلْ لَكَ إِلَىٰ أَنْ تَزَكَّىٰ18

Ukamwambie, ‘Je, unapendelea kuitakasa nafsi yako na upungufu na kuipamba na imani?
79:19Juzuu 30 · uk. 584

وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ19

Na nikuelekeze njia ya kumtii Mola wako, upate kumcha na kumuogopa?’»
79:20Juzuu 30 · uk. 584

فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ20

Mūsā alimuonyesha Firauni alama kubwa: fimbo na mkono.
79:21Juzuu 30 · uk. 584

فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ21

Hapo Firauni alimkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu , naye ni Mtume Mūsā, amani imshukie, na alimuasi Mola wake Aliyetukuka.
79:22Juzuu 30 · uk. 584

ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ22

Kisha alikengeuka hali ya kuipa mgongo Imani na kufanya bidii katika kumpinga Mūsā.
79:23Juzuu 30 · uk. 584

فَحَشَرَ فَنَادَىٰ23

Hapo aliwakusanya raia wa utawala wake na akawaita kwa
79:24Juzuu 30 · uk. 584

فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ24

kuwaambia,»Mimi ndiye mola wenu ambaye hakuna mola mwengine aliye juu yake.»
79:25Juzuu 30 · uk. 584

فَأَخَذَهُ اللَّهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ25

Hapo Mwenyezi Mungu Alimtesa kwa adhabu ya duniani na ya Akhera.
79:26Juzuu 30 · uk. 584

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِمَنْ يَخْشَىٰ26

Na Akaifanya adhabu hiyo iwe ni mazingatio na ni onyo kwa watu mfano wake kati ya wale waasi. Hakika Firauni na kile kilichompata cha adhabu ni mawaidha kwa mwenye kuwaidhika na kutishika.
79:27Juzuu 30 · uk. 584

أَأَنْتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ ۚ بَنَاهَا27

Je, kufufuliwa kwenu, enyi watu, baada ya kufa ni kugumu zaidi, katika vipimo vyenu, au ni kuumbwa kwa mbingu?
79:28Juzuu 30 · uk. 584

رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا28

Amezipanga juu yenu kama jengo. Na Ameinua sakafu yake angani, haina tofauti wala nyufa.
79:29Juzuu 30 · uk. 584

وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا29

Na Ameutia giza usiku wake kwa kutwa kwa jua lake. Na Ameweka wazi mchana wake kwa kuchomoza kwake.
79:30Juzuu 30 · uk. 584

وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا30

Na ardhi baada ya kuumba mbingu Ameitandaza. Na Ameweka humo manufaa yake.
79:31Juzuu 30 · uk. 584

أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا31

Na Ametumbua humo chemchemu za maji. Na Ameotesha humo mimea inayolishwa.
79:32Juzuu 30 · uk. 584

وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا32

Na Ameyakita humo majabali yakiwa ni vigingi vyake. Ameumba, Aliyetakasika na kila upungufu,
79:33Juzuu 30 · uk. 584

مَتَاعًا لَكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ33

neema zote hizi zikiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu. (Hakika kurudisha kuumbwa kwenu, Siku ya Kiyama, ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kushinda kuumba viumbe hivyo vyingine. Na vyote hivyo, kwa Mwenyezi Mungu, ni rahisi na ni vipesi).
79:34Juzuu 30 · uk. 584

فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ34

Pindi kitakapokuja Kiyama Kikubwa na balaa nzito, nao ni Mvuvio wa pili. Kipindi hicho zitaoneshwa kwa binadamu vitendo vyake vyote, za kheri na za shari.
79:35Juzuu 30 · uk. 584

يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنْسَانُ مَا سَعَىٰ35

Hapo atazikumbuka na kuzitambua.
79:36Juzuu 30 · uk. 584

وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَنْ يَرَىٰ36

Na utaoneshwa Moto wa Jahanamu kwa kila aonaye, uwe waonekana waziwazi.
79:37Juzuu 30 · uk. 584

فَأَمَّا مَنْ طَغَىٰ37

Ama yule atakayekiuka amri ya Mwenyezi Mungu
79:38Juzuu 30 · uk. 584

وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا38

na akapendelea maisha ya ulimwenguni kuliko ya Akhera,
79:39Juzuu 30 · uk. 584

فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ39

basi kwa kweli marejeo yake ni Motoni.
79:40Juzuu 30 · uk. 584

وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ40

Na ama yule atakayeogopa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kuhesabiwa na akaikanya nafsi yake na matamanio mapotofu,
79:41Juzuu 30 · uk. 584

فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ41

basi Peponi ndiko makazi yake.
79:42Juzuu 30 · uk. 584

يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا42

Wanakuuliza washirikina, ewe Mtume, kwa madharau, kuhusu wakati wa kuanzia Kiyama unachowaonya.
79:43Juzuu 30 · uk. 584

فِيمَ أَنْتَ مِنْ ذِكْرَاهَا43

Wewe huna kamwe ujuzi nacho.
79:44Juzuu 30 · uk. 584

إِلَىٰ رَبِّكَ مُنْتَهَاهَا44

Bali mambo ya ujuzi huo yarejeshwe kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Sifa Tukufu.
79:45Juzuu 30 · uk. 584

إِنَّمَا أَنْتَ مُنْذِرُ مَنْ يَخْشَاهَا45

Wewe linalokuhusu katika habari zake ni kumuonya nacho yule anayekiogopa.
79:46Juzuu 30 · uk. 584

كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا46

Kama kwamba wao siku watakapouona Kiyama kimesimama, watakuwa hawakukaa katika maisha yao ya duniani, kwa vituko vya hiko Kiyama, isipokuwa ni kama kwamba wamkaa kati ya adhuhuri mpaka kutwa juwa, au ni kama kati ya kuchomoza jua mpaka nusu ya mchana.

Cheza kutoka mwanzo wa sura