Abasa

سورة عبس

Sura 80 · Makki · 42 aya

80:1Juzuu 30 · uk. 585

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ1

Yalidhihiri mabadiliko na mkunjiko katika uso wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,
80:2Juzuu 30 · uk. 585

أَنْ جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ2

na akapa nyongo kwa sababu ya kwamba Abdallah bin Ummi Maktum alimjilia akitaka aelekezwe. Na alikuwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ameshughulika kuwalingania miamba wa Kikureshi katika Uislamu.
80:3Juzuu 30 · uk. 585

وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ3

Ni kitu gani kinakufanya wewe ujue uhakika wa jambo lake? Kwani huenda ikawa, kwa kuuliza kwake, nafsi yake itatakasika na kusafika.
80:4Juzuu 30 · uk. 585

أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنْفَعَهُ الذِّكْرَىٰ4

Au pengine apate mazingatio zaidi na kutishika.
80:5Juzuu 30 · uk. 585

أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ5

Basi yule alijyejitosheleza na kutouhitajia uongozi wako,
80:6Juzuu 30 · uk. 585

فَأَنْتَ لَهُ تَصَدَّىٰ6

wewe ndiye unayemjali na wapulikiza maneno yake.
80:7Juzuu 30 · uk. 585

وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ7

Na ni kitu gani kinachokupa jukumu kwako iwapo hakusafika na ukafiri wake?
80:8Juzuu 30 · uk. 585

وَأَمَّا مَنْ جَاءَكَ يَسْعَىٰ8

Ama yule ambaye amekuwa na pupa la kukutana na wewe,
80:9Juzuu 30 · uk. 585

وَهُوَ يَخْشَىٰ9

na huku anamuogopa Mwenyezi Mungu asiwe na kasoro katika kupata uongofu,
80:10Juzuu 30 · uk. 585

فَأَنْتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ10

wewe unampuuza. Ilivyotakikana ufanye si kama ulivyofanya, ewe Mtume.
80:11Juzuu 30 · uk. 585

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ11

Hakika Sura hii ni mawaidha kwako na kwa kila anayetaka kuwaidhika.
80:12Juzuu 30 · uk. 585

فَمَنْ شَاءَ ذَكَرَهُ12

Basi atakaye atamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja na atafuata Wahyi Wake.
80:13Juzuu 30 · uk. 585

فِي صُحُفٍ مُكَرَّمَةٍ13

Wahyi huu, nao ni Qur’ani, uko katika kurasa zilizotukuzwa,
80:14Juzuu 30 · uk. 585

مَرْفُوعَةٍ مُطَهَّرَةٍ14

zenye kuheshimiwa, zenye cheo cha juu,
80:15Juzuu 30 · uk. 585

بِأَيْدِي سَفَرَةٍ15

zilizosafishwa na uchafu, uongezaji na upunguzaji.
80:16Juzuu 30 · uk. 585

كِرَامٍ بَرَرَةٍ16

Zilizoko mikononi mwa Malaika waandishi, mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na viumbe Wake, wenye maumbile mema, tabia zao ni nzuri na njema na pia matendo yao.
80:17Juzuu 30 · uk. 585

قُتِلَ الْإِنْسَانُ مَا أَكْفَرَهُ17

Amelaaniwa mtu kafiri na ataadhibiwa. Ni uovu ulioje wa ukafiri wake kwa Mola wake!
80:18Juzuu 30 · uk. 585

مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ18

Kwani hajui ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Alimuumba kwacho mwanzo wake?
80:19Juzuu 30 · uk. 585

مِنْ نُطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ19

Mwenyezi Mungu Alimuumba kwa maji machache, nayo ni manii. Akayakadiria miongo yake.
80:20Juzuu 30 · uk. 585

ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ20

Kisha Akambainishia njia ya kheri na ya shari.
80:21Juzuu 30 · uk. 585

ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ21

Kisha humkosesha uhai, na Amemuekea mahali pa kuzikiwa.
80:22Juzuu 30 · uk. 585

ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنْشَرَهُ22

Kisha Akitaka Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa mbaya, Atamhuisha na kumfufua baada ya kifo chake, kwa ajili ya kuhesabiwa na kulipwa.
80:23Juzuu 30 · uk. 585

كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ23

Mambo siyo kama yale anayoyasema kafiri na anayoyafanya. Bado hajatakeleza Aliyomuamrisha kwayo Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda wema kwa kumtii.
80:24Juzuu 30 · uk. 585

فَلْيَنْظُرِ الْإِنْسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ24

Na azingatie binadamu, vipi Mwenyezi Mungu Amekiumba chakula chake ambacho ndicho kinachoendeleza maisha yake?
80:25Juzuu 30 · uk. 585

أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا25

Aone kwamba Sisi Tumeyamimina maji ya mvua juu ya ardhi kwa wingi.
80:26Juzuu 30 · uk. 585

ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا26

Kisha Tumeipasua ardhi kwa Tulivyo vitoa kutoka humo miongoni mwa mimea tofauti.
80:27Juzuu 30 · uk. 585

فَأَنْبَتْنَا فِيهَا حَبًّا27

Tukaotesha humo nafaka
80:28Juzuu 30 · uk. 585

وَعِنَبًا وَقَضْبًا28

na zabibu, na nyasi za wanyama.Na mizaituni na mitende.
80:29Juzuu 30 · uk. 585

وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا29

Na mabustani yenye miti mikubwa.
80:30Juzuu 30 · uk. 585

وَحَدَائِقَ غُلْبًا30

Na matunda
80:31Juzuu 30 · uk. 585

وَفَاكِهَةً وَأَبًّا31

na ndisha.
80:32Juzuu 30 · uk. 585

مَتَاعًا لَكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ32

Mnajistareheshea kwazo, nyinyi na wanyama wenu.
80:33Juzuu 30 · uk. 585

فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ33

Utakapokuja Ukelele wa Siku ya Kiyama, ambao utayatia uziwi, kwa kitisho chake, masikizi.
80:34Juzuu 30 · uk. 585

يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ34

Siku mtu atakapomkimbia, kwa kitisho cha Siku Hiyo, nduguye
80:35Juzuu 30 · uk. 585

وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ35

na babake na mamake na
80:36Juzuu 30 · uk. 585

وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ36

mkewe na wanawe.
80:37Juzuu 30 · uk. 585

لِكُلِّ امْرِئٍ مِنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ37

Kila mmoja Siku Hiyo, atakuwa na jambo litakalomzuia asishughulike na mwingine.
80:38Juzuu 30 · uk. 585

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُسْفِرَةٌ38

Nyuso za wenye neema, Siku Hiyo, zitakuwa ni zenye kung’ara,
80:39Juzuu 30 · uk. 585

ضَاحِكَةٌ مُسْتَبْشِرَةٌ39

zenye furaha na nderemo.
80:40Juzuu 30 · uk. 585

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ40

Na nyuso za watu wa Motoni zitakuwa na giza,
80:41Juzuu 30 · uk. 586

تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ41

nyeusi, zafinikwa na unyonge.
80:42Juzuu 30 · uk. 586

أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ42

Hao wenye kusifika na sifa hiyo ndiwo wale waliozikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wakazikanusha aya zake na wakayakeuka Aliyoyaharamisha kwa kutenda maovu na kukiuka mipaka.

Cheza kutoka mwanzo wa sura