As-Saffat

سورة الصافات

Sura 37 · Makki · 182 aya

37:1Juzuu 23 · uk. 446

وَالصَّافَّاتِ صَفًّا1

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anaapa kwa Malaika wanaojipanga, katika kuabudu kwao, mistari iliyofuatana na kushikana,
37:2Juzuu 23 · uk. 446

فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا2

na kwa Malaika wanaofukuza mawingu na kuyaongoza kwa amri ya MwenyeziMungu,
37:3Juzuu 23 · uk. 446

فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا3

na kwa Malaika wanaosoma utajo wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na maneno Yake,
37:4Juzuu 23 · uk. 446

إِنَّ إِلَٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ4

kwamba muabudiwa wenu, enyi watu, ni Mmoja, Asiye na mshirika. Hivyo basi mtakasieni ibada na utiifu. Na Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Anachotaka miongoni mwa viumbe Vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, kwani kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina.
37:5Juzuu 23 · uk. 446

رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ5

Yeye Ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili, na Ndiye Mpelekeshaji jua katika sehemu zake za kuchomozea na zile za kuchwea.
37:6Juzuu 23 · uk. 446

إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ6

Sisi tumeupamba uwingu wa karibu kwa pambo la nyota.
37:7Juzuu 23 · uk. 446

وَحِفْظًا مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ مَارِدٍ7

Na tumeuhifadhi huo uwingu, kwa nyota, na kila shetani mwenye kuasi, mjeuri, aliyefukuzwa (kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu).
37:8Juzuu 23 · uk. 446

لَا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِنْ كُلِّ جَانِبٍ8

Hawawezi hao Mashetani kufika kwenye viumbe vya juu, navyo ni mbingu na Malaika waliyomo ndani yake, wakapata kuwasikiliza wanapoutamka wahyi ambao Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anauleta, unaokusanya sheria Yake na makadirio Yake, na wanavurumizwa vimondo katika kila upande,
37:9Juzuu 23 · uk. 446

دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ9

kwa kuwafukuza ili wasipate kusikiliza. Na huko kwenye Nyumba ya Akhera watakuwa na adhabu ya daima yenye kuumiza.
37:10Juzuu 23 · uk. 446

إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ10

Isipokuwa yule aliyenyakuwa, miongoni mwa Mashetani, mnyakuo wa haraka, nao ni lile neno analolisikia mbinguni kwa haraka, akamtupia aliyekuwa chini yake, na yule mwingine akamtupia aliyekuwa chini yake. Basi pengine huenda akafikiwa na kimondo chenye kutoa mwangaza kabla hajalitupa, na pengine huwa amelitupa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kabla ya kujiwa na kimondo kikamchoma, na yule mwingine akaenda nalo hadi kwa makuhani wakaongeza juu ya neno hilo maneno mia moja ya urongo.
37:11Juzuu 23 · uk. 446

فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمْ مَنْ خَلَقْنَا ۚ إِنَّا خَلَقْنَاهُمْ مِنْ طِينٍ لَازِبٍ11

Basi waulize, ewe Mtume, wenye kukanusha Kufufuliwa: Je kuumbwa kwao ni kugumu zaidi au ni hivyi viumbe tulivyoviumba? Kwa hakika, tulimuumba baba yao Ādam kwa udongo ulioshikana na kuambatana.
37:12Juzuu 23 · uk. 446

بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ12

Bali ulistaajabu, ewe Mtume, kwa ukanushaji wao na kukataa kwao Kufufuliwa. Na la kustaajabiwa zaidi na lililo kubwa zaidi kuliko lile la kukataa kwao ni kwamba wao wanakucheza shere na kulidharau neno lako.
37:13Juzuu 23 · uk. 446

وَإِذَا ذُكِّرُوا لَا يَذْكُرُونَ13

Na wanapokumbushwa walichokisahau au walichoghafilika nacho, hawanufaiki kwa huo ukumbusho wala hawazingatii.
37:14Juzuu 23 · uk. 446

وَإِذَا رَأَوْا آيَةً يَسْتَسْخِرُونَ14

Na wanapoiona miujiza yenye kutolea dalili unabii wako, wanakufanyia shere na wanastaajabu.
37:15Juzuu 23 · uk. 446

وَقَالُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُبِينٌ15

Na wanasema, «Halikuwa hili ulilotuletea isipokuwa ni uchawi uliojitokeza waziwazi.
37:16Juzuu 23 · uk. 446

أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ16

Je, tunapokufa na tukawa ni mchanga na mifupa iliyochakaa, je sisi ni wenye kufufuliwa kutoka makaburini mwetu tukiwa hai?
37:17Juzuu 23 · uk. 446

أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ17

au pia watafufuliwa baba zetu waliopita kabla yetu?»
37:18Juzuu 23 · uk. 446

قُلْ نَعَمْ وَأَنْتُمْ دَاخِرُونَ18

Waambie, ewe Mtume, «Ndio mtafufuliwa hali mkiwa wanyonge, watwevu.»
37:19Juzuu 23 · uk. 446

فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنْظُرُونَ19

Hakika ni kwamba huo utakuwa ni Mvuvio mmoja, wakitahamaki wao wamesimama kutoka makaburini mwao, wanatazama vituko vya Kiyama.
37:20Juzuu 23 · uk. 446

وَقَالُوا يَا وَيْلَنَا هَٰذَا يَوْمُ الدِّينِ20

Na watasema, «Ewe maangamivu yetu! Hii ni siku ya kuhesabiwa na kulipwa!»
37:21Juzuu 23 · uk. 446

هَٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ21

Hapo wataambiwa, «Hii ndiyo Siku ya Uamuzi wa haki baina ya viumbe, ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani na mkiikataa.»
37:22Juzuu 23 · uk. 446

۞ احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ22

Na Malaika wataambiwa, «Wakusanyeni wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na wafananao na wao na waungu wao waliokuwa wakiwaabudu
37:23Juzuu 23 · uk. 446

مِنْ دُونِ اللَّهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ23

badala ya Mwenyezi Mungu, na muwasukume kwa nguvu hadi kwenye moto wa Jahanamu.
37:24Juzuu 23 · uk. 446

وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ24

«Na muwafunge kabla hawajafika kwenye moto wa Jahanamu, kwa kuwa wao ni wenye kuulizwa kuhusu matendo yao na maneno yao yaliyotokana na wao duniani, kwa namna ya kumshtukia kuwakaripia.»
37:25Juzuu 23 · uk. 447

مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ25

Na wataambiwa kwa kulaumiwa, «Kwa nini hamsaidiani nyinyi kwa nyinyi?»
37:26Juzuu 23 · uk. 447

بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ26

Bali wao Leo ni wenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, hawataenda kinyume nayo wala hawataepukana nayo, hawajisaidii wao wenyewe.
37:27Juzuu 23 · uk. 447

وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ27

Na hapo makafiri watakabiliana wao kwa wao wakilaumiana na wakigombana.
37:28Juzuu 23 · uk. 447

قَالُوا إِنَّكُمْ كُنْتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ28

Wafuasi watasema kuwaambia wafuatwa, «Nyinyi mlikuwa mkitujia kwa upande wa dini na haki, mkiifanya Sheria ni twevu kwetu, mkitutia chuki nayo na mkitupambia upotevu.»
37:29Juzuu 23 · uk. 447

قَالُوا بَلْ لَمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ29

Hapo watasema wafuatwa kuwaabia wafuasi, «Mambo si kama vile mnavyodai, bali ni nyoyo zenu zilikuwa zimekataa kuamini, zimeuelekea ukafiri na uasi.
37:30Juzuu 23 · uk. 447

وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُمْ مِنْ سُلْطَانٍ ۖ بَلْ كُنْتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ30

«Na sisi hatukuwa na hoja juu yenu wala nguvu, tukaweza kwa hizo kuwazuilia kuamini. Bali nyinyi wenyewe, enyi washirikina, mlikuwa waasi wenye kupita mipaka ya haki.
37:31Juzuu 23 · uk. 447

فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا ۖ إِنَّا لَذَائِقُونَ31

«Hivyo basi ndio sisi sote ikalazimu tupate onyo la Mola wetu kuwa ni wenye kuonja adhabu, sisi na nyinyi, kwa yale tuliyoyatanguliza ya madhambi na maasia duniani.
37:32Juzuu 23 · uk. 447

فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ32

« Ndipo tukawapoteza na njia ya Mwenyezi Mungu na ya kumuamini, kwa kuwa sisi wenyewe tulikuwa ni wapotevu kabla yenu. Na kwa hivyo tukapotea kwa sababu ya ukafiri wetu na tukawaangamiza nyinyi pamoja na sisi.»
37:33Juzuu 23 · uk. 447

فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ33

Basi wafuasi na wafuatwa watashirikiana katika adhabu Siku ya Kiyama, kama walivyoshirikiana ulimwenguni katika kumuasi Mwenyezi Mungu.
37:34Juzuu 23 · uk. 447

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ34

Hivi ndivyo sisi tunavyowafanyia waliochagua mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu ulimwenguni na wakaacha kumtii, basi tutawaonjesha adhabu kali.
37:35Juzuu 23 · uk. 447

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ35

Hakika wale washirikina walikuwa duniani wakiambiwa, «Hapana mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu,» na wakaitwa kwenye mwito huo na wakaamrishwa kuyaacha yanayopingana nao, wanaufanyia kiburi na kumfanyia kiburi aliyekuja nao.
37:36Juzuu 23 · uk. 447

وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَجْنُونٍ36

Na wanasema, «Je, tuache kuwaabudu waungu wetu kwa maneno ya mshairi mwenye wazimu?» wakimkusudia Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
37:37Juzuu 23 · uk. 447

بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ37

Wamesema urongo! Muhammad sivyo vile walivyomueleza. Bali amekuja na Qur’ani na upwekeshaji Mwenyezi Mungu, na akathibitisha ukweli wa Mitume katika kile walichokitolea habari kuhusu sheria ya Mwenyezi Mungu na kumpwekesha Yeye.
37:38Juzuu 23 · uk. 447

إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ38

Hakika yenu nyinyi, enyi washirikina, kwa neno lenu, ukafiri wenu na kukanusha kwenu, ni wenye kuonja adhabu iliyo kali yenye uchungu.
37:39Juzuu 23 · uk. 447

وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ39

Na hamtalipwa huko Akhera isipokuwa kwa lile la maasia mliokuwa mkilifanya duniani.
37:40Juzuu 23 · uk. 447

إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ40

Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, waliomtakasia Ibada Yake, Akawatakasa na Akawahusu wao kwa rehema Yake, basi hao kwa hakika ni wenye kuokoka na adhabu yenye uchungu.
37:41Juzuu 23 · uk. 447

أُولَٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَعْلُومٌ41

Hao waliotakaswa watapata riziki ijulikanayo isiyokatika ndani ya Pepo.
37:42Juzuu 23 · uk. 447

فَوَاكِهُ ۖ وَهُمْ مُكْرَمُونَ42

Riziki hiyo ni matunda aina mbalimbali. Na wao ni wenye kukirimiwa kwa takrima ya Mwenyezi Mungu
37:43Juzuu 23 · uk. 447

فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ43

kuwafanyia wao ndani ya mabustani ya Pepo ya starehe ya milele.
37:44Juzuu 23 · uk. 447

عَلَىٰ سُرُرٍ مُتَقَابِلِينَ44

Na miongoni mwa takrima yao watakayoipata kwa Mola wao, na kukirimiana wao kwa wao, ni kuwa wao watakuwa kwenye vitanda wameelekeana.
37:45Juzuu 23 · uk. 447

يُطَافُ عَلَيْهِمْ بِكَأْسٍ مِنْ مَعِينٍ45

Zinazungushwa kwao gilasi za Pombe inayotoka kwenye mito inayotembea, hawachelei kuwa itamalizika,
37:46Juzuu 23 · uk. 447

بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِلشَّارِبِينَ46

ni nyeupe rangi yake, ni tamu katika kuinywa,
37:47Juzuu 23 · uk. 447

لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنْزَفُونَ47

haina madhara yoyote ya akili wala ya mwili.
37:48Juzuu 23 · uk. 447

وَعِنْدَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ48

Na hapo kwao kwenye makao yao watakuwako wanawake waliojihifadhi, hawawatazami isipokuwa waume zao, wazuri wa macho,
37:49Juzuu 23 · uk. 447

كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَكْنُونٌ49

kama kwamba wao ni mayai yaliyotunzwa ambayo hayajaguswa na mikono.
37:50Juzuu 23 · uk. 447

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ50

Hapo wataelekeana wakiulizana kuhusu hali zao za duniani na mambo ya usumbufu waliokuwa wakikutana nayo huko, na yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaneemesha nayo Peponi. Na huku ndiko kuliwazika kuliotimia.
37:51Juzuu 23 · uk. 447

قَالَ قَائِلٌ مِنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ51

Atasema msemaji miongoni mwa watu wa Peponi, «Kwa kweli, nilikuwa na rafiki duniani aliyeshikana na mimi.
37:52Juzuu 23 · uk. 448

يَقُولُ أَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ52

«Aliyekuwa akisema, ‘Ni vipi wewe unaamini Ufufuzi ambao ni upeo wa kustaajabisha?
37:53Juzuu 23 · uk. 448

أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ53

Je, tunapokufa, tukakatika vipande- vipande na tukawa mchanga na mifupa, kwani ni wenye kufufuliwa, kuhesabiwa na kulipwa kwa matendo yetu?’»
37:54Juzuu 23 · uk. 448

قَالَ هَلْ أَنْتُمْ مُطَّلِعُونَ54

Atasema huyu Muumini aliyetiwa Peponi akiwaambia wenzake, «Je, nyinyi ni wenye kuchungulia mpate kuona mwisho wa yule rafiki?»
37:55Juzuu 23 · uk. 448

فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ55

Hapo akachungulia na akamuona rafiki yake katikati ya Moto.
37:56Juzuu 23 · uk. 448

قَالَ تَاللَّهِ إِنْ كِدْتَ لَتُرْدِينِ56

Muumini atasema kumwambia rafiki yake mwenye kukanusha kufufuliwa, «Ulikaribia kuniangamiza kwa kunizuia nisiamini lau nilikutii.
37:57Juzuu 23 · uk. 448

وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنْتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ57

Na lau si wema wa Mola wangu kwa kuniongoza mimi kwenye Imani na kunithibitisha juu yake, ningalikuwa ni mwenye kuhudhurishwa kwenye adhabu pamoja na wewe.
37:58Juzuu 23 · uk. 448

أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ58

«Je, ni kweli sisi ni wenye kukalishwa milele na kuneemeshwa, si wenye kufa
37:59Juzuu 23 · uk. 448

إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ59

isipokuwa kifo chetu cha mwanzo huko ulimwenguni, na sisi si wenye kuadhibiwa baada ya kuingia kwetu Peponi?
37:60Juzuu 23 · uk. 448

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ60

Hakika starehe hii tuliyo nayo ndiyo kufaulu kukubwa.
37:61Juzuu 23 · uk. 448

لِمِثْلِ هَٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ61

«Basi kwa kupata mfano wa starehe hizi kamilifu, makazi ya daima na kufaulu kukubwa, na watende wenye kutenda duniani ili wazifikie huko Akhera.»
37:62Juzuu 23 · uk. 448

أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ62

Je, hayo yaliyotangulia kuelezwa ya starehe za Pepo ni makaribisho bora na vipewa vya Mwenyezi Mungu, au ni mti mbaya uliolaaniwa wa zaqqūm, ambao ni chakula cha watu wa Motoni?
37:63Juzuu 23 · uk. 448

إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِلظَّالِمِينَ63

Sisi tumeufanya ni mtihani waliotahiniwa nao madhalimu kwa ukanushaji na kufanya mambo ya uasi na wakasema kwa njia ya kiburi, «Mtu wenu anawapa habari kwamba motoni kuna mti, na moto unakula miti.»
37:64Juzuu 23 · uk. 448

إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ64

Hakika huo ni mti ambao unaota kwenye uketo wa moto wa Jahanamu, matunda yake yana sura mbaya
37:65Juzuu 23 · uk. 448

طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ65

kama vichwa vya Mashetani.
37:66Juzuu 23 · uk. 448

فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ66

Basi yanapokuwa hivyo, usiulize baada ya haya kuhusu utamu wake. Kwani washirikina ni wenye kula kutoka mti huo na ni wenye kujaza matumbo yao kwa matunda hayo.
37:67Juzuu 23 · uk. 448

ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِنْ حَمِيمٍ67

Kisha wao, baada ya kuyala ni wenye kunywa kinywaji mchanganyiko kilicho kibaya na kilicho moto.
37:68Juzuu 23 · uk. 448

ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ68

Kisha marejeo yao baada ya adhabu hii ni kuishia (hukohuko) kwenye adhabu ya Moto.
37:69Juzuu 23 · uk. 448

إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءَهُمْ ضَالِّينَ69

Hakika wao waliwakuta baba zao kwenye ushirikina na upotevu,
37:70Juzuu 23 · uk. 448

فَهُمْ عَلَىٰ آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ70

na wakakimbilia kuwafuata katika hilo.
37:71Juzuu 23 · uk. 448

وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ الْأَوَّلِينَ71

na kwa hakika, kabla ya watu wako, ewe Mtume, walipotea na kuwa kando na haki ummah wengi waliotangulia.
37:72Juzuu 23 · uk. 448

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِمْ مُنْذِرِينَ72

Na kwa hakika, tuliwatumiliza kwa ummah hao Mitume waliowaonya adhabu, lakini wakakanusha.
37:73Juzuu 23 · uk. 448

فَانْظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنْذَرِينَ73

Basi fikiria: ulikuwa vipi mwisho wa ummah hao walioonywa na wakakanusha? Waliadhibiwa na wakawa ni mazingatio kwa watu.
37:74Juzuu 23 · uk. 448

إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ74

Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu Aliyowasafisha na Akawachagua kwa kuwapa rehema Yake kwa kule kumtakasa kwao Yeye.
37:75Juzuu 23 · uk. 448

وَلَقَدْ نَادَانَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ الْمُجِيبُونَ75

Na kwa hakika Alituita kwa kutuomba Nabii wetu Nūḥ tumlinde na watu wake, basi bora wa wenye kumuitikia tulikuwa ni sisi.
37:76Juzuu 23 · uk. 448

وَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ76

Na tukamuokoa yeye na watu wa nyumbani kwake na Waumini pamoja naye kutokana na maudhi ya washirikina na kutokana na kuzamishwa kwa mafuriko makubwa.
37:77Juzuu 23 · uk. 449

وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُ هُمُ الْبَاقِينَ77

Na tukawafanya watoto wa Nūḥ ndio wenye kusalia baada ya kuzamishwa watu wake.
37:78Juzuu 23 · uk. 449

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ78

Na tukamuwekea utajo mwema na sifa nzuri kwa watu waliokuja baada yake wakawa wanamtaja nazo.
37:79Juzuu 23 · uk. 449

سَلَامٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِي الْعَالَمِينَ79

Amani imfikie Nūḥ na asalimike na kutajwa kwa ubaya katika kipindi cha watu wa mwisho, bali asifiwe na watu wa vizazi vinavyokuja baada yake.
37:80Juzuu 23 · uk. 449

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ80

Mfano wa malipo mema tuliomlipa Nūḥ, tutamlipa kila aliyefanya vizuri, miongoni mwa waja, katika kumtii Mwenyezi Mungu.
37:81Juzuu 23 · uk. 449

إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ81

Hakika Nūḥ ni miongoni mwa waja wetu wenye kuamini, wenye kumtakasia Mwenyezi Mungu na wenye kufuata amri za Mwenyezi Mungu kivitendo.
37:82Juzuu 23 · uk. 449

ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ82

Kisha tukawazamisha wengine, wenye kukanusha kati ya watu wake, kwa mafuriko, kisisalie chochote, miongoni mwao, hata jicho lenye kupepesa.
37:83Juzuu 23 · uk. 449

۞ وَإِنَّ مِنْ شِيعَتِهِ لَإِبْرَاهِيمَ83

Na miongoni mwa waliokuwa katika nyendo za Nūḥ, njia yake na mila yake ni Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrāhīm,
37:84Juzuu 23 · uk. 449

إِذْ جَاءَ رَبَّهُ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ84

alipomjia Mola wake kwa moyo uliyojitenga na kila itikadi ya ubatilifu na tabia ya kujitukanisha,
37:85Juzuu 23 · uk. 449

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَاذَا تَعْبُدُونَ85

alipomwambia babake na watu wake kwa njia ya kuwakanya, «Ni kitu gani hiko mnachokiabudu badala ya Mwenyezi Mungu?
37:86Juzuu 23 · uk. 449

أَئِفْكًا آلِهَةً دُونَ اللَّهِ تُرِيدُونَ86

Je, mnataka kuabudu waungu wa kuzuliwa na mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake?
37:87Juzuu 23 · uk. 449

فَمَا ظَنُّكُمْ بِرَبِّ الْعَالَمِينَ87

Mnamdhani Mola wa viumbe vyote Atawafanya nini mkimshirikisha Yeye na mkamuabudu asiyekuwa Yeye?
37:88Juzuu 23 · uk. 449

فَنَظَرَ نَظْرَةً فِي النُّجُومِ88

Akatazama mtazamo mmoja kwenye nyota kulingana na mila ya watu wake kuhusu hilo, huku akifikiria udhuru wa kuutoa ili asipate kutoka na wao kwenda kwenye sherehe zao,
37:89Juzuu 23 · uk. 449

فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ89

akawaambia, «Mimi ni mgonjwa.» Hii ilikuwa ni ishara ya mbali kutoka kwake.
37:90Juzuu 23 · uk. 449

فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ90

Basi wakamuacha nyuma yao.
37:91Juzuu 23 · uk. 449

فَرَاغَ إِلَىٰ آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ91

Akabeta kwa haraka kuelekea kwenye masanamu wa watu wake, akasema kwa njia ya kuwakejeli, «Si mkile chakula hiki ambacho washika mlango wenu wanawapatia?
37:92Juzuu 23 · uk. 449

مَا لَكُمْ لَا تَنْطِقُونَ92

Muna nini nyinyi mbona hamsemi wala hamumjibu mwenye kuwaomba?
37:93Juzuu 23 · uk. 449

فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًا بِالْيَمِينِ93

Akawaelekea waungu wao kuwapiga na kuwavunja-vunja kwa mkono wake wa kulia, ili kuwathibitishia makosa ya kuwaabudu.
37:94Juzuu 23 · uk. 449

فَأَقْبَلُوا إِلَيْهِ يَزِفُّونَ94

Wakaja kumkabili kwa haraka na mbio huku wana hasira.
37:95Juzuu 23 · uk. 449

قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ95

Ibrāhīm akakutana na wao akiwa imara kwa kusema, «Vipi mtaabudu masanamu mnaowachonga nyinyi wenyewe na mnaowatengeneza kwa mikono yenu,
37:96Juzuu 23 · uk. 449

وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ96

na mnaacha kumuabudu Mola wenu Aliyewaumba nyinyi na Akayaumba matendo yenu?»
37:97Juzuu 23 · uk. 449

قَالُوا ابْنُوا لَهُ بُنْيَانًا فَأَلْقُوهُ فِي الْجَحِيمِ97

Hoja ilipowasimamia, waliamua kutumia nguvu na wakasema, «Jengeni jengo kwa ajili yake, mlijaze kuni kisha mumtupe ndani yake»
37:98Juzuu 23 · uk. 449

فَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَسْفَلِينَ98

Watu wa Ibrāhīm wakataka kumfanyia vitimbi ili wamuangamize, tukawafanya wao kuwa ndio wenye kutendeshwa nguvu na kushindwa. Mwenyezi Mungu Akavirudisha vitimbi vyao kwenye shingo zao na akaufanya ule moto uwe baridi na salama kwa Ibrāhīm.
37:99Juzuu 23 · uk. 449

وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهْدِينِ99

Akasema Ibrāhīm, «Mimi nahamia kwa Mola wangu kutoka kwenye mji wa watu wangu kuelekea pale ambapo nitamakinika kumuabudu Mola wangu, kwani Yeye Atanielekeza kwenye kheri ya Dini yangu na dunia yangu.
37:100Juzuu 23 · uk. 449

رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ100

Mola wangu! Nipe mtoto mwema.»
37:101Juzuu 23 · uk. 449

فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ101

Tukamkubalia ombi lake na tukambashiria kuwa atapata mtoto wa kiume atakayekuwa mpole ukubwani mwake, naye ni Ismā'īl.
37:102Juzuu 23 · uk. 449

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانْظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ102

Alipokuwa mkubwa Ismā'īl, akawa anatembea na babake, babake alimwambia, «Mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja, je, una maoni gani?» (na ndoto za Manabii ni za kweli). Ismā'īl akasema, kwa kumridhisha Mola wake, kumtii mzazi wake na kumsaidia juu ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, «Endelea katika jambo Alilokuamrisha Mwenyezi Mungu la kunichinja mimi. Utanikuta, Mwenyezi Mungu Akitaka, ni mvumilivu, mtiifu na ni mwenye kutarajia malipo mema (kutoka kwa Mwenyezi Mungu)».
37:103Juzuu 23 · uk. 450

فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ103

Walipojisalimisha wao wawili kwa kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu na kuiandama, na Ibrāhīm akambwaga Ismā'īl chini, kwa upande wa paji la uso, ili kumchinja.
37:104Juzuu 23 · uk. 450

وَنَادَيْنَاهُ أَنْ يَا إِبْرَاهِيمُ104

Na tukamuita Ibrāhīm katika hali hiyo ngumu kwamba: Ewe Ibrāhīm! Umeshalifanya uliloamrishwa na, kwa hivyo,
37:105Juzuu 23 · uk. 450

قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ105

umeisadikisha ndoto yako. Hakika yetu sisi kama vile tulivyokulipa mema kwa kuamini kwako , ndivyo tunavyowalipa wale waliofanya wema mfano wako, tuwaepushie shida duniani na Akhera.
37:106Juzuu 23 · uk. 450

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ106

Hakika amri ya kuwa wewe umuue mwano ndio mtihani mgumu uliodhihirisha ukweli wa Imani yako.
37:107Juzuu 23 · uk. 450

وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ107

Na tukamuokoa Ismā'īl, na tukamuekea kondoo mkubwa kuwa ni badala yake.
37:108Juzuu 23 · uk. 450

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ108

Na tukambakishia Ibrāhīm baada yake sifa njema kwa watu.
37:109Juzuu 23 · uk. 450

سَلَامٌ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ109

Maamkizi kwa Ibrāhīm kutoka kwa Mola wake na kumuombea asalimike na kila dhara.
37:110Juzuu 23 · uk. 450

كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ110

Kama tulivyomlipa malipo mema Ibrāhīm kwa utiifu wake kwetu na kufuata kwake amri yetu, ndivyo tutakavyowalipa wenye kufanya wema miongoni mwa waja wetu.
37:111Juzuu 23 · uk. 450

إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ111

Hakika yeye ni miongoni mwa waja wetu Waumini waliyoipa hiyo sifa ya uja haki yake.
37:112Juzuu 23 · uk. 450

وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِنَ الصَّالِحِينَ112

Na tukampa bishara Ibrāhīm ya mtoto wake, Isḥāq, kuwa atakuwa Nabii, miongoni mwa watu wema. Hayo yakiwa ni malipo ya uvumilivu wake na kuridhika kwake na amri ya Mola wake na utiifu wake Kwake.
37:113Juzuu 23 · uk. 450

وَبَارَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰ إِسْحَاقَ ۚ وَمِنْ ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِنَفْسِهِ مُبِينٌ113

Na tukawateremshia baraka. Na miongoni mwa wale wanaotokana na kizazi chao kuna anayemtii Mola wake, anayeifanyia wema nafsi yake, na kuna anayeidhulumu (nafsi yake) dhulma iliyo wazi kwa ukafiri wake na utendaji wake maasia.
37:114Juzuu 23 · uk. 450

وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ114

Na kwa hakika tuliwafanyia wema Mūsā na Hārūn kwa kuwapa unabii na utume.
37:115Juzuu 23 · uk. 450

وَنَجَّيْنَاهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ115

Na tukawaokoa wao wawili na watu wao kutokana na gharika, utumwa na unyonge waliokuwa nao.
37:116Juzuu 23 · uk. 450

وَنَصَرْنَاهُمْ فَكَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ116

Na tukawanusuru, wakawa na enzi, usaidizi na ushindi juu ya Fir'awn na jamaa zake.
37:117Juzuu 23 · uk. 450

وَآتَيْنَاهُمَا الْكِتَابَ الْمُسْتَبِينَ117

Na tukawapa wao wawili Taurati yenye ufafanuzi,
37:118Juzuu 23 · uk. 450

وَهَدَيْنَاهُمَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ118

na tukawaongoza njia iliyonyoka isiyokuwa na upotovu, nayo ni Uislamu, Dini ya Mwenyezi Mungu ambayo Amewatumiliza Manabii Wake kwayo,
37:119Juzuu 23 · uk. 450

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِي الْآخِرِينَ119

na tukazifanya sifa zao nzuri na utajo wao mwema ni vyenye kusalia baada yao.
37:120Juzuu 23 · uk. 450

سَلَامٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ120

Maamkizi kwa Mūsā na Hārūn kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na sifa njema na kuwaombea wao wasalimike na kila dhara.
37:121Juzuu 23 · uk. 450

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ121

Kama tulivyowalipa wao malipo mema , ndivyo tutakavyowalipa wenye kufanya wema miongoni mwa waja wetu wenye kututakasia kwa ukweli, kuamini na kutenda.
37:122Juzuu 23 · uk. 450

إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ122

Hakika ya wao wawili ni miongoni mwa waja wetu waliojikita katika Imani.
37:123Juzuu 23 · uk. 450

وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ123

Na hakika mja wetu Ilyas ni miongoni mwa wale ambao tuliwakirimu kwa unabii na utume.
37:124Juzuu 23 · uk. 450

إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَلَا تَتَّقُونَ124

Kumbuka na utaja pindi aliposema kuwaambia watu wake, kati ya Wana wa Isrāīl, «Mcheni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na mumuogope, na msimshirikishe mwengine pamoja na Yeye.
37:125Juzuu 23 · uk. 450

أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ125

Vipi nyinyi mtaliabudu sanamu ambalo ni kiumbe dhaifu na mtamuacha Mzuri wa kuumba, Mwenye sifa nzuri na kamilifu kabisa,
37:126Juzuu 23 · uk. 450

اللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ126

mkawa hamtamuabudu Mwenyezi Mungu Ambaye ni Mola wenu Aliyewaumba nyinyi na Akawaumba baba zenu waliopita kabla yenu?»
37:127Juzuu 23 · uk. 451

فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ127

Watu wa Ilyas walimkanusha Nabii wao. Basi Mwenyezi Mungu , kwa hakika, Atawakusanya Siku ya Kiyama ili wahesabiwe na wateswe.
37:128Juzuu 23 · uk. 451

إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ128

Isipokuwa wale waja wa Mwenyezi Mungu waliomtakasia Mwenyezi Mungu Dini yao, basi hao ni wenye kuokoka na adhabu Yake.
37:129Juzuu 23 · uk. 451

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ129

Tulimfanya Ilyas awe na sifa nzuri kwa ummah waliokuja baada yake.
37:130Juzuu 23 · uk. 451

سَلَامٌ عَلَىٰ إِلْ يَاسِينَ130

Maamkizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na sifa njema kwa Ilyas.
37:131Juzuu 23 · uk. 451

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ131

Na kama tulivyomlipa Ilyas malipo mema kwa utiifu wake, ndivyo tutakavyowalipa walio wema miongoni mwa waja wetu Waumini.
37:132Juzuu 23 · uk. 451

إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ132

Hakika yake yeye ni miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu waliomtakasia wenye kufuata amri zake kivitendo.
37:133Juzuu 23 · uk. 451

وَإِنَّ لُوطًا لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ133

Na hakika mja wetu Lūṭ tulimchagua na tukamfanya ni miongoni mwa Mitume.
37:134Juzuu 23 · uk. 451

إِذْ نَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ134

Tulipomuokoa yeye na watu wa nyumbani kwake wote,
37:135Juzuu 23 · uk. 451

إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ135

isipokuwa mkongwe aliyezeeka, naye ni mke wake, ambaye aliangamia pamoja na wale walioangamia miongoni mwa watu wake kwa ukafiri wake.
37:136Juzuu 23 · uk. 451

ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ136

Kisha tukawaangamiza wakanushaji waliosalia miongoni mwa watu wake.
37:137Juzuu 23 · uk. 451

وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِمْ مُصْبِحِينَ137

Na hakika yenu nyinyi, enyi watu wa Makkah mnazipitia katika safari zenu nyumba za watu wa Lūṭ na athari zao katika kipindi cha asubuhi,
37:138Juzuu 23 · uk. 451

وَبِاللَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ138

na pia mnazipitia katika kipindi cha usiku. Basi hamtii akilini, mkaogopa kisije kikawafika nyinyi kile kilichowafika wao?
37:139Juzuu 23 · uk. 451

وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ139

Hakika mja wetu Yūnus, tulimchagua na tukamfanya ni miongoni mwa Mitume.
37:140Juzuu 23 · uk. 451

إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ140

Alipokimbia kutoka mji wake, akiwa na hasira juu ya watu wake, akapanda jahazi iliyojaa abiria na vyombo.
37:141Juzuu 23 · uk. 451

فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ141

Mawimbi makubwa yakaizunguka jahazi hiyo kila upande. Na watu waliokuwa wamepanda jahazi wakapiga kura ili kupunguza shehena ili wasizame. Yūnus akawa ni miongoni mwa wale walioshindwa kwa kura.
37:142Juzuu 23 · uk. 451

فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ142

Hivyo basi akatupwa baharini na chewa akammeza, na hali ni kwamba Yūnus, amani imshukie, ameleta jambo la kumfanya alaumiwe.
37:143Juzuu 23 · uk. 451

فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ143

Lau si yale yaliyotangulia kwake, ya wingi wa Ibada na matendo mema kabla ya kuingia ndani ya tumbo la chewa kwa kusema, «Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, kutakasika na sifa za upungufu ni kwako, mimi nimekuwa miongoni mwa wenye kudhulumu,»
37:144Juzuu 23 · uk. 451

لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ144

angalikaa ndani ya tumbo la chewa, na lingalikuwa ni kaburi lake mpaka Siku ya Kiyama.
37:145Juzuu 23 · uk. 451

۞ فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ145

Tukamtoa kwenye tumbo la chewa na tukamtupa kwenye ardhi tupu, isiyokuwa na miti wala majengo, akiwa dhaifu wa mwili.
37:146Juzuu 23 · uk. 451

وَأَنْبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِنْ يَقْطِينٍ146

Na tukamuoteshea mmea wa matango ili umfinike na anufaike nao.
37:147Juzuu 23 · uk. 451

وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ147

Tukamtumiliza aende kwa watu wake wanaofikia elfu mia moja, bali wanazidi idadi hiyo.
37:148Juzuu 23 · uk. 451

فَآمَنُوا فَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ148

Wakamuamini na wakafuata aliyokuja nayo kivitendo, na kwa hivyo tukawastarehesha maishani mwao mpaka wakati wa kufika ajali zao.
37:149Juzuu 23 · uk. 451

فَاسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ الْبَنَاتُ وَلَهُمُ الْبَنُونَ149

Basi waulize watu wako, ewe Mtume, «Ni vipi wamemfanya Mwenyezi Mungu ana watoto wa kike ambao wao wenyewe wanawachukia, na wao wana watoto wa kiume wanaowataka?»
37:150Juzuu 23 · uk. 451

أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ150

Na waulize wao, «Je, tuliwaumba Malaika wakiwa wanawake, na hali wao wapo (wakishuhudia uumbaji huo)?»
37:151Juzuu 23 · uk. 451

أَلَا إِنَّهُمْ مِنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ151

Na miongoni mwa urongo wao ni kule kusema kwao, «Mwenyezi Mungu Amezaa!
37:152Juzuu 23 · uk. 451

وَلَدَ اللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ152

Na kwa hakika, wao ni warongo, kwa kuwa wanakisema wasichokijua.»
37:153Juzuu 23 · uk. 451

أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ153

Ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Achague watoto wa kike na sio wa kiume?
37:154Juzuu 23 · uk. 452

مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ154

Ni uamuzi mbaya sana mnaoutoa, enyi watu, wa kuwa Mwenyezi Mungu Ana watoto wa kike na nyinyi mna watoto wa kiume, na hali nyinyi hamridhiki nafsi zenu kuwa na watoto wa kike.
37:155Juzuu 23 · uk. 452

أَفَلَا تَذَكَّرُونَ155

Je, hamkumbuki kwamba haifai wala haitakikani Awe na mtoto? Ametukuka Mwenyezi Mungu na kuwa mbali na hilo, umbali ulio juu sana.
37:156Juzuu 23 · uk. 452

أَمْ لَكُمْ سُلْطَانٌ مُبِينٌ156

Lakini je, mna hoja ya wazi juu ya hilo neno lenu na uzushi wenu?
37:157Juzuu 23 · uk. 452

فَأْتُوا بِكِتَابِكُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ157

Iwapo mna hoja ndani ya kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, basi kileteni, mkiwa ni wa kweli katika hilo neno lenu.
37:158Juzuu 23 · uk. 452

وَجَعَلُوا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ الْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ158

Na washirikina walifanya kuwa kuna uhusiano wa kizazi baina ya Mwenyezi Mungu na Malaika, na hakika ni kwamba Malaika washajua kuwa washirikina ni wenye kuletwa Siku ya Kiyama ili kuadhibiwa.
37:159Juzuu 23 · uk. 452

سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ159

Ametakasika Mwenyezi Mungu na kila lisilofaa asifike nalo miongoni mwa yale wanaomsifu nayo washirikina.
37:160Juzuu 23 · uk. 452

إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ160

Lakini wale waja wa Mwenyezi Mungu wanaomtakasia katika kumuabudu hawamsifu isipokuwa kwa sifa zinazolingana na utukufu Wake, kutakasika ni Kwake.
37:161Juzuu 23 · uk. 452

فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ161

Hakika yenu nyinyi, enyi wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kile mnachokiabudu badala ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa waungu,
37:162Juzuu 23 · uk. 452

مَا أَنْتُمْ عَلَيْهِ بِفَاتِنِينَ162

hamkuwa ni wenye kumpoteza yoyote
37:163Juzuu 23 · uk. 452

إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ الْجَحِيمِ163

isipokuwa yule Aliyemkadiria Mwenyezi Mungu aingie kwenye Moto wa Jaḥīm kwa sababu ya ukafiri wake na udhalimu wake.
37:164Juzuu 23 · uk. 452

وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَعْلُومٌ164

Malaika wanasema, «Hakuna yoyote miongoni mwetu isipokuwa ana makao maalumu mbinguni.
37:165Juzuu 23 · uk. 452

وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ165

Na sisi ndio tunaosimama kwa kujipanga kwa safu katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii.
37:166Juzuu 23 · uk. 452

وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ166

Na sisi ndio tunaomtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisichofaa kunasibishwa nacho.»
37:167Juzuu 23 · uk. 452

وَإِنْ كَانُوا لَيَقُولُونَ167

Na hakika makafiri wa Makkah walikuwa wakisema kabla hujatumilizwa,
37:168Juzuu 23 · uk. 452

لَوْ أَنَّ عِنْدَنَا ذِكْرًا مِنَ الْأَوَّلِينَ168

«Ewe Mtume! Lau vingalitujia vitabu na Manabii vile vilivyowajia wa mwanzo kabla yetu,
37:169Juzuu 23 · uk. 452

لَكُنَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ169

tungalikuwa waja wa Mwenyezi Mungu wakweli katika Imani, waliotakaswa kwa kufanya Ibada.»
37:170Juzuu 23 · uk. 452

فَكَفَرُوا بِهِ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ170

Ulipowajia wao utajo wa watu wa mwanzo na utajo wa watu wa mwisho na kitabu kikamilifu kabisa na bora wa Mitume, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, walimkanusha. Basi wataijua adhabu watakayopatiwa Siku ya Mwisho.
37:171Juzuu 23 · uk. 452

وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا الْمُرْسَلِينَ171

Kwa hakika lishatangulia neno letu, ambalo halina namna ya kurudi, la kuwaahidi waja wetu waliopewa utume
37:172Juzuu 23 · uk. 452

إِنَّهُمْ لَهُمُ الْمَنْصُورُونَ172

kwamba watapata usaidizi juu ya maadui zao, kwa hoja na nguvu,
37:173Juzuu 23 · uk. 452

وَإِنَّ جُنْدَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ173

na kwamba askari wetu wanaopigana jihadi katika njia yetu ndio wenye kuwashinda maadui zao kila mahali, kuzingatia mwishoni na marejeo.
37:174Juzuu 23 · uk. 452

فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ174

Basi wape mgongo, ewe Mtume, wale walioshindana na wasiikubali haki mpaka ukamalizika muda waliopatiwa muhula na ikaja amri ya Mwenyezi Mungu ya wao kuadhibiwa,
37:175Juzuu 23 · uk. 452

وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ175

wangojee na subiri uone: ni adhabu gani itakayowashukia wao kwa kuenda kinyume nawe? Basi wataiona adhabu ya Mwenyezi Mungu itakayowashukia.
37:176Juzuu 23 · uk. 452

أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ176

Je kuteremkiwa kwao na adhabu yetu ndilo jambo wanalokuharakishia, ewe Mtume?
37:177Juzuu 23 · uk. 452

فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنْذَرِينَ177

Basi adhabu yetu itakapowashukia, asubuhi mbaya zaidi ni asubuhi yao!
37:178Juzuu 23 · uk. 452

وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ178

Na uwape mgongo mpaka Mwenyezi Mungu Atoe idhini ya wao kuadhibiwa.
37:179Juzuu 23 · uk. 452

وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ179

Na uwangojee, kwani wataiona adhabu itakayowashukia na mateso.
37:180Juzuu 23 · uk. 452

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ180

Mola wa enzi na utukufu Ameepukana na kuwa juu ya kila kile ambacho wanaomzulia urongo wanamsifu nacho.
37:181Juzuu 23 · uk. 452

وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ181

Na maamkizi ya Mwenyezi Mungu ya daima,sifa Zake na amani Yake ziwafikie Mitume wote.
37:182Juzuu 23 · uk. 452

وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ182

Na shukrani na sifa njema ni za Mola wa viumbe wote ulimwenguni na Akhera. Yeye Ndiye Mstahiki wa hilo Peke Yake, Hana mshirika Wake.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Hani Ar-Rifai - As-Saffat · Tlawati