Al-Mutaffifin

سورة المطففين

Sura 83 · Makki · 36 aya

83:1Juzuu 30 · uk. 587

وَيْلٌ لِلْمُطَفِّفِينَ1

Adhabu kali ni ya wale wanaopunja vipimo vya vibaba na mezani.
83:2Juzuu 30 · uk. 587

الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ2

Ambao wakinunua kwa watu cha kupimwa kwa vibaba au kwa mizani hujikamilishia wao wenyewe.
83:3Juzuu 30 · uk. 587

وَإِذَا كَالُوهُمْ أَوْ وَزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ3

Na wakiwauzia watu kinachouzwa kwa vibaba au mizani wanapunguza vipimo.
83:4Juzuu 30 · uk. 587

أَلَا يَظُنُّ أُولَٰئِكَ أَنَّهُمْ مَبْعُوثُونَ4

Basi itakuwaje hali ya yule anayeiba na kupunja katika vipimo vyote hivyo, au yule anayeiba katika vipimo hivyo na huku awapunja watu vitu vyao? Hakika huyo yuwastahiki mateso zaidi kuliko wapunguzaji wa vipimo vya vibaba na mizani. Kwani hawaamini wale wapunjaji ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kuwafufua na kuwahesabu juu ya vitendo vyao.
83:5Juzuu 30 · uk. 588

لِيَوْمٍ عَظِيمٍ5

katika Siku itakapokuwa na kitisho?
83:6Juzuu 30 · uk. 588

يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ6

Siku watakaposimama watu mbele ya Mweyezi Mungu ili Awahesabu kwa machache na mengi walioyatenda, hali ya kuwa wao Siku Hiyo ni wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, Mlezi wa viumbe vyote.
83:7Juzuu 30 · uk. 588

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ7

Hakika marejeo ya watu waovu na makazi yao yatakuwa katika hali ya dhiki.
83:8Juzuu 30 · uk. 588

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ8

Na ni kipi kinachokujulidha dhiki hii ni ipi?
83:9Juzuu 30 · uk. 588

كِتَابٌ مَرْقُومٌ9

Hakika hiyo itakuwa ni jela ya kudumu na adhabu iliyo na uchungu. Penye jela hiyo ni pale walipoandikiwa kuwa watakwenda. Wameandikiwa na imepitishwa. Hapana kitakachozidishwa wala kupunguzwa.
83:10Juzuu 30 · uk. 588

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ10

Adhabu kali Siku Hiyo ni ya wale wenye kukanusha.
83:11Juzuu 30 · uk. 588

الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ11

Wale ambao wanakanusha kuwako tukio la Siku ya Malipo.
83:12Juzuu 30 · uk. 588

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ12

Na wala haikanushi Siku Hiyo isipokuwa kila dhalimu mwenye madhambi mengi.
83:13Juzuu 30 · uk. 588

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ13

Anaposomewa aya za Qur’ani, husema, «Hizi ni hadithi za urongo za watu wa kale.» Mambo yalivyo si kama wanavyodai!
83:14Juzuu 30 · uk. 588

كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ14

Bali hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu na Wahyi Wake kwa Mtume Wake.
83:15Juzuu 30 · uk. 588

كَلَّا إِنَّهُمْ عَنْ رَبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَمَحْجُوبُونَ15

Na hakika zimezibwa nyoyo zao zikawa hazimkubali Mwenyezi Mungu. Na kile kilichoziziba nyoyo hizo ni kufinikwa na wingi wa madhambi wanayoyafanya. Mambo hayako kama vile wanavyodai makafiri! Bali hakika wao, Siku ya Kiyama watazibwa wasimuone Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda. Aya hii ni ushahidi kwamba Waumini watamuona Mola Wao Peponi.
83:16Juzuu 30 · uk. 588

ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ16

Kisha hakika hao makafiri ni wenye kuingia Motoni, na wataziona na kuzihisi dharubu zake.
83:17Juzuu 30 · uk. 588

ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ17

Kisha wataambiwa,»Haya ndiyo malipo ya yale ambayo mlikuwa mnayakanusha.»
83:18Juzuu 30 · uk. 588

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ18

Ni kweli kabisa kwamba kitabu cha watu wema, nao ni wachamungu, kiko katika ngazi za juu Peponi.
83:19Juzuu 30 · uk. 588

وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ19

Na ni kipi kinachokujulisha ni zipi hizi ngazi za juu?
83:20Juzuu 30 · uk. 588

كِتَابٌ مَرْقُومٌ20

Ni kitabu cha watu wema kilichopitishwa mambo yake, hakizidishwi kitu humo wala hakipunguzwi.
83:21Juzuu 30 · uk. 588

يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ21

Wanayatazama yaliyomo ndani yake Malaika waliokurubishwa, wa kila mbingu.
83:22Juzuu 30 · uk. 588

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ22

Hakika wale wenye ukweli na kufuata amri za Mwenyezi Mungu watakuwa Peponi wnaneemeka,
83:23Juzuu 30 · uk. 588

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنْظُرُونَ23

juu ya viti vya fahari wanamwangalia Mola wao na wanaangalia yale waliyoandaliwa miongoni mwa kheri nyingi.
83:24Juzuu 30 · uk. 588

تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ24

Unaonekana katika nyuso zao mng’aro wa neema.
83:25Juzuu 30 · uk. 588

يُسْقَوْنَ مِنْ رَحِيقٍ مَخْتُومٍ25

Watanyweshwa tembo safi, lililotengezewa vyombo kwa ustadi na mwishowe kuna harufu ya miski.
83:26Juzuu 30 · uk. 588

خِتَامُهُ مِسْكٌ ۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ26

Katika kuzipata neema hizo, nawashindane wenye kushindana.
83:27Juzuu 30 · uk. 588

وَمِزَاجُهُ مِنْ تَسْنِيمٍ27

Na kinywaji hiki, mchanganyo wake watokana na chemchemi iliyoko Peponi linalojulikana, kwa ubora wake, kwa jina la Tasnīm.
83:28Juzuu 30 · uk. 588

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ28

Hiyo ni chemchemi iliyoandaliwa wale waliokurubishwa kwa Mwenyezi Mungu na watajiburudisha nayo.
83:29Juzuu 30 · uk. 588

إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ29

Hakika wale waliotenda maovu walikuwa duniani wakiwacheza shere Waumini.
83:30Juzuu 30 · uk. 588

وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ30

Na wanapowapitia wanakonyezana kwa kuwakejeli.
83:31Juzuu 30 · uk. 588

وَإِذَا انْقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انْقَلَبُوا فَكِهِينَ31

Na wnaporudi, hawa waovu, kwa watu wao na jamaa zao, huwa na vihunzi na wao kwa kuwafanyia maskhara Waumini.
83:32Juzuu 30 · uk. 588

وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ32

Na hawa makafiri wanapowaona Maswahaba wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wamefuata uongofu, huwa wakisema, «Hakika hawa wamepotea kwa kumfuata Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
83:33Juzuu 30 · uk. 588

وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ33

Na wala waovu hawa hawakutumwa wawe ni wachunguzi kwa Maswahaba na Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
83:34Juzuu 30 · uk. 589

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ34

Basi Siku ya Kiyama wale waliomkubali Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakafanya vitendo vinavyolingana na sheria Zake, watawafanyia maskhara makafiri kama makafiri walivyokuwa wakiwafanyia mashara duniani.
83:35Juzuu 30 · uk. 589

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنْظُرُونَ35

Juu ya viti vya fahari, watakuwa Waumini wanaangalia yale Aliyowapa Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo matukufu na neema, wakiwa Peponi. Na neema kubwa ya zote ni kuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
83:36Juzuu 30 · uk. 589

هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ36

Je, wamelipwa makafiri, pindi watakapo kufanyiwa hayo, malipo muwafaka na yale waliyoyafanya duniani ya shari na madhambi?

Cheza kutoka mwanzo wa sura