Al-Ma'arij

سورة المعارج

Sura 70 · Makki · 44 aya

70:1Juzuu 29 · uk. 568

سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ1

Ameapiza mwenye kuapiza miongoni mwa washirikina, kujiapiza mwenyewe na kuwaapiza watu wake kuteremkiwa na adhabu,
70:2Juzuu 29 · uk. 568

لِلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ2

nayo ni yenye kuwashukia bila shaka Siku ya Kiyama.
70:3Juzuu 29 · uk. 568

مِنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ3

Hakuna mzuiaji yoyote wa kuizuia isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenye utukufu na haiba.
70:4Juzuu 29 · uk. 568

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ4

Malaika na Jibrili wanapanda kuenda Kwake, Aliyetukuka, kwa siku moja ambayo kadiri yake ni myaka elfu hamsini katika myaka ya duniani, nayo kwa aliyeamini ni kama muda wa Swala moja ya faradhi.
70:5Juzuu 29 · uk. 568

فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا5

Basi vumilia, ewe Mtume, kule kufanya kwao shere na kutaka kwao wafikiwe na adhabu kwa haraka, uvumilivu usiokuwa na babaiko wala kumshtakia asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
70:6Juzuu 29 · uk. 568

إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا6

Kwa kweli makafiri wanaiona adhabu kuwa iko mbali na wanaona kuwa si yenye kutukia.
70:7Juzuu 29 · uk. 568

وَنَرَاهُ قَرِيبًا7

Na sisi tunaiona ni yenye kutukia kwa kipindi cha karibu bila shaka.
70:8Juzuu 29 · uk. 568

يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ8

Siku ambayo mbingu itayayuka iwe ni kama rojo la mafuta,
70:9Juzuu 29 · uk. 568

وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ9

na majabali yawe ni kama sufi iliyochanganywa na iliyoshanuliwa na kupeperushwa na upepo.
70:10Juzuu 29 · uk. 568

وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا10

Wala mtu hatamuuliza jamaa yake wa karibu kuhusu jambo lake, kwani kila mmoja ameshughulishwa na nafsi yake.
70:11Juzuu 29 · uk. 569

يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ11

Watawaona na watawajua, na hakuna yoyote atakayeweza kumnufaisha yoyote. Kafiri atatamani lau ajikomboa nafsi yake na adhabu ya Siku ya Kiyama kwa watoto wake,
70:12Juzuu 29 · uk. 569

وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ12

mkewe, nduguye,
70:13Juzuu 29 · uk. 569

وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ13

jamaa zake wanaomuhami na ambao anajinasibisha nao kwa ujamaa
70:14Juzuu 29 · uk. 569

وَمَنْ فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنْجِيهِ14

na kwa wote walio kwenye ardhi miongoni mwa binadamu na wengineo ili aokoke na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
70:15Juzuu 29 · uk. 569

كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ15

Mambo siyo kama vile unavyotamani yawe, ewe kafiri, ya kujikomboa.
70:16Juzuu 29 · uk. 569

نَزَّاعَةً لِلشَّوَىٰ16

Huo ni moto wa Jahanamu, moto wake unawaka na kuroroma, joto lake linatoa kwa nguvu ngozi ya kichwa na sehemu nyingine za mwili,
70:17Juzuu 29 · uk. 569

تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ17

unamwita aliyeipa mgongo haki duniani na akaacha kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake,
70:18Juzuu 29 · uk. 569

وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ18

na akakusanya mali na kuyaweka kwenye mahazina yake na asitekeleze amri ya Mwenyezi Mungu kwenye mali hayo.
70:19Juzuu 29 · uk. 569

۞ إِنَّ الْإِنْسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا19

Hakika binadamu ameumbwa akiwa na tabia ya babaiko na pupa.
70:20Juzuu 29 · uk. 569

إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا20

Yakimpata makero na shida, anababaika sana na kufa moyo.
70:21Juzuu 29 · uk. 569

وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا21

Na yakimpata mambo mazuri na ukunjufu wa maisha, huwa ni mwingi wa kuzuia na.
70:22Juzuu 29 · uk. 569

إِلَّا الْمُصَلِّينَ22

Isipokuwa wenye kusimamisha Swala,
70:23Juzuu 29 · uk. 569

الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ23

wanaochunga kuitekeleza katika nyakati zake zote, hakuna shughuli yoyote inayowashughulisha nayo.
70:24Juzuu 29 · uk. 569

وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَعْلُومٌ24

Na wale ambao katika mali yao kuna fungu maalumu alililowafaradhia Mwenyezi Mungu, nalo ni Zaka
70:25Juzuu 29 · uk. 569

لِلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ25

wanaozitoa kwa anayeomba msaada na kwa na kwa asiyeomba.
70:26Juzuu 29 · uk. 569

وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ26

Na wale ambao wanaiamini Siku ya kuhesabiwa na kulipwa wakajiandaa nayo kwa matendo mema.
70:27Juzuu 29 · uk. 569

وَالَّذِينَ هُمْ مِنْ عَذَابِ رَبِّهِمْ مُشْفِقُونَ27

Na wale ambao wao wanaiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu,
70:28Juzuu 29 · uk. 569

إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ28

kwani adhabu ya Mola wao haipaswi kwa yoyote kujiaminisha nayo.
70:29Juzuu 29 · uk. 569

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ29

Na wale ambao wao ni wenye kutunza tupu zao na kila alichokiharamishia Mwenyezi Mungu,
70:30Juzuu 29 · uk. 569

إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ30

isipokuwa wake zao na vijakazi vyao, hakika wao kwa hao hawapatilizwi.
70:31Juzuu 29 · uk. 569

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ31

Basi mwenye kutaka kumaliza matamanio yake ya kimwili kwa wasiokuwa wake zake au vijakazi vyake, basi hao ndio wenye kukiuka mipaka ya halali kuingia kwenye haramu.
70:32Juzuu 29 · uk. 569

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ32

Na wale ambao wanazitunza amana za Mwenyezi Mungu na amana za waja, na wanatunza ahadi zao pamoja na Mwenyezi Munmgu, Aliyetukuka, na pamoja na waja.
70:33Juzuu 29 · uk. 569

وَالَّذِينَ هُمْ بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ33

Na wale ambao wanatekeleza ushahidi wao kwa ukweli bila kubadilisha au kuficha.
70:34Juzuu 29 · uk. 569

وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ34

Na wale ambao wanatunza utekelezaji Swala wala hawaharibu chochote cha wajibu katika hiyo Swala.
70:35Juzuu 29 · uk. 569

أُولَٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُكْرَمُونَ35

Hao waliosifika kwa sifa hizo njema, ni wenye kutulia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe, ni wenye kukirimiwa humo kwa kila aina ya takrima.
70:36Juzuu 29 · uk. 569

فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ36

Ni msukumo gani unaowasukuma makafiri watembee kwa haraka kuelekea upande wako, ewe Mtume, na huku wamenyosha shingo zao kwako, wamekukabili kwa macho yao,
70:37Juzuu 29 · uk. 569

عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ37

wanajikusanya kuliani kwako na kushotoni kwako, wakiwa wamekaa kwa kupiga maduara na wamejigawa vikundi mbalimbali, wanazungumza na kuona ajabu?
70:38Juzuu 29 · uk. 569

أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِنْهُمْ أَنْ يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ38

Je ana tamaa kila mmoja miongoni mwa makafiri kuwa Mwenyezi Mungui Atamuingiza kwenye Pepo ya starehe ya daima? Mambo siyo kama vile wanavyotazamia. Wao hawataiingia hiyo Pepo kabisa.
70:39Juzuu 29 · uk. 569

كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُمْ مِمَّا يَعْلَمُونَ39

Hakika sisi tumewaumba kwa kile wanachokijua cha maji matwevu kama wengineo, na vilevile hawakuamini. Basi vipi watapata heshima ya kuingia Pepo ya sterehe?
70:40Juzuu 29 · uk. 569

فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ40

Sivyo hivyo. Najiapia Mimi Mwenyewe niliye Mola wa pande za kuchomoza na kutua jua, mwezi na sayari nyinginezo, kwa yanayopatikana humo miongoni mwa dalili waziwazi za kujulisha kufufuliwa,
70:41Juzuu 29 · uk. 570

عَلَىٰ أَنْ نُبَدِّلَ خَيْرًا مِنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ41

kuwa Sisi tunaweza kuwaleta watu badala yao walio bora zaidi kuliko wao na watiifu zaidi wa Mwenyezi Mungu. Na hakuna yoyote atakayetushinda na kutuponyoka na kutuelemea iwapo tunataka kumrudisha uhai baada ya kufa.
70:42Juzuu 29 · uk. 570

فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ42

Basi waache wavame kwenye ubatilifu wao na wacheze kwenye ulimwengu wao mpaka wakutane na Siku ya Kiyama ambayo wanaahidiwa kuwa wataadhibiwa.
70:43Juzuu 29 · uk. 570

يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ43

Siku watakapotoka makaburini wakienda kwa haraka, kama wlivyokuwa duniani wakienda mbio na haraka kwa waungu wao wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu,
70:44Juzuu 29 · uk. 570

خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ44

hali ya kuwa macho yao ni madhalilifu yanatazama chini, wamefinikwa na unyonge na utwevu. Hiyo ndiyo Siku waliyoahidiwa duniani na walikuwa wakiifanyia shere na kuikanusha.

Cheza kutoka mwanzo wa sura