Al-Waqi'ah

سورة الواقعة

Sura 56 · Makki · 96 aya

56:1Juzuu 27 · uk. 534

إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ1

Kitakaposimama Kiyama.
56:2Juzuu 27 · uk. 534

لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ2

Hakutakuwa na yoyote mwenye kukanusha kusimama kwake.
56:3Juzuu 27 · uk. 534

خَافِضَةٌ رَافِعَةٌ3

Ni chenye kuwainamisha chini maadui wa Mwenyezi Mungu ndani ya Moto na ni chenye kuwainua juu Peponi wale wenye kumtegemea.
56:4Juzuu 27 · uk. 534

إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا4

Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.
56:5Juzuu 27 · uk. 534

وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا5

Na yakamumunyuliwa majabali mmumunyuo wa kina.
56:6Juzuu 27 · uk. 534

فَكَانَتْ هَبَاءً مُنْبَثًّا6

Yakawa vumbi lenye kuruka angani lililosukumwa na upepo.
56:7Juzuu 27 · uk. 534

وَكُنْتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً7

Na mkawa, enyi viumbe, makundi matatu:
56:8Juzuu 27 · uk. 534

فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ8

Kundi la watu wa upande wa kulia, wenye daraja kubwa. Ni kikubwa kilioje cheo chao!
56:9Juzuu 27 · uk. 534

وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ9

Kuna na kundi la watu wa upande wa kushoto, wenye daraja duni. Ni mbaya iliyoje hali yao!
56:10Juzuu 27 · uk. 534

وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ10

Na wale waliotangulia mbele kwenye kheri duniani ndio wenye kutangulia mbele kwenye daraja za juu huko Akhera.
56:11Juzuu 27 · uk. 534

أُولَٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ11

Wao ndio walioletwa karibu kwa Mwenyezi Mungu,
56:12Juzuu 27 · uk. 534

فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ12

Mola wao Atawatia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe.
56:13Juzuu 27 · uk. 534

ثُلَّةٌ مِنَ الْأَوَّلِينَ13

Watayaingia watu wengi watu wa mwanzo wa ummah huu, na ummah wengineo wasiokuwa wao,
56:14Juzuu 27 · uk. 534

وَقَلِيلٌ مِنَ الْآخِرِينَ14

na wachache miongoni mwa watu mwisho wa ummah huu,
56:15Juzuu 27 · uk. 534

عَلَىٰ سُرُرٍ مَوْضُونَةٍ15

wakiwa juu ya vitanda vilivyofumwa kwa dhahabu,
56:16Juzuu 27 · uk. 534

مُتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ16

na wakiwa katika hali ya kuvitegemea na huku wanaelekeana na kukutana.
56:17Juzuu 27 · uk. 535

يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُخَلَّدُونَ17

Wanawazunguka wao kuwatumikia watumishi vijana wasiozeeka wala kufa,
56:18Juzuu 27 · uk. 535

بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِنْ مَعِينٍ18

wakiwa na vikombe, mabirika na gilasi kutoka kwenye chemchemi ya pombe yenye kupita ndani ya Pepo,
56:19Juzuu 27 · uk. 535

لَا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنْزِفُونَ19

na hawaumwi na vichwa kutokana nayo wala hawarukwi na akili.
56:20Juzuu 27 · uk. 535

وَفَاكِهَةٍ مِمَّا يَتَخَيَّرُونَ20

Na watawazunguka wao watumishi vijana na kila kitu wanachokichagua miongoni mwa matunda,
56:21Juzuu 27 · uk. 535

وَلَحْمِ طَيْرٍ مِمَّا يَشْتَهُونَ21

nyama ya ndege ambayo nafsi zao inavutika nayo.
56:22Juzuu 27 · uk. 535

وَحُورٌ عِينٌ22

Na watakuwa na wanawake wenye macho makubwa kama kwamba wao,
56:23Juzuu 27 · uk. 535

كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ23

kwa usafi wao na uzuri wao, ni lulu iliyohifadhiwa ndani ya mashaza yake,
56:24Juzuu 27 · uk. 535

جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ24

hali hayo yakiwa ni malipo yao kwa yale waliokuwa wakiyafanya duniani.
56:25Juzuu 27 · uk. 535

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا25

Hawatasikia humo Peponi ubatilifu wala yale ya kuwatia madhambini kuyasikia,
56:26Juzuu 27 · uk. 535

إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا26

isipokuwa maneno yasiyokuwa na kasoro hizi na kusalimiana wao kwa wao.
56:27Juzuu 27 · uk. 535

وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ27

Na watu wa upande wa kulia,
56:28Juzuu 27 · uk. 535

فِي سِدْرٍ مَخْضُودٍ28

ni kikubwa kilioje cheo chao na malipo yao!
56:29Juzuu 27 · uk. 535

وَطَلْحٍ مَنْضُودٍ29

Watakuwa kwenye mikunazi isiyo na miba, na ndizi zilizopandana na kupangika,
56:30Juzuu 27 · uk. 535

وَظِلٍّ مَمْدُودٍ30

kila ndizi juu ya nyingine, na vivuli vya daima visivyoondoka,
56:31Juzuu 27 · uk. 535

وَمَاءٍ مَسْكُوبٍ31

na maji yanayotembea yasiyokatika,
56:32Juzuu 27 · uk. 535

وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ32

na matunda mengi
56:33Juzuu 27 · uk. 535

لَا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ33

yasiyomalizika wala kuwaishia wala hakuna kizuizi chochote kinachowazuia wao kuyafikia,
56:34Juzuu 27 · uk. 535

وَفُرُشٍ مَرْفُوعَةٍ34

na matandiko yaliyoinuliwa juu ya vitanda.
56:35Juzuu 27 · uk. 535

إِنَّا أَنْشَأْنَاهُنَّ إِنْشَاءً35

Sisi tumewaumba wanawake wa watu wa Peponi umbile ambalo silo lile umbile lililokuwa duniani, umbile lililokamilika lisilokubali kutoweka,
56:36Juzuu 27 · uk. 535

فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا36

na tumewafanya ni wanawali wenye kujipendekeza kwa waume zao,
56:37Juzuu 27 · uk. 535

عُرُبًا أَتْرَابًا37

hali ya kuwa ni marika na wao kimiaka.
56:38Juzuu 27 · uk. 535

لِأَصْحَابِ الْيَمِينِ38

Tumewaumbia wanawake hao watu wa upande wa kulia.
56:39Juzuu 27 · uk. 535

ثُلَّةٌ مِنَ الْأَوَّلِينَ39

Nao ni kundi la watu wengi wa mwanzo
56:40Juzuu 27 · uk. 535

وَثُلَّةٌ مِنَ الْآخِرِينَ40

na kundi la watu wengi wa mwisho.
56:41Juzuu 27 · uk. 535

وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ41

Na watu wa upande wa kushoto, ni mbaya iliyoje hali yao na malipo yao!
56:42Juzuu 27 · uk. 535

فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ42

Watakuwa kwenye upepo ulio moto utokanao na joto la Moto wa Jahanamu utakaozuia pumzi zao, na maji moto yanayochemka,
56:43Juzuu 27 · uk. 535

وَظِلٍّ مِنْ يَحْمُومٍ43

na kivuli cha moshi mweusi sana,
56:44Juzuu 27 · uk. 535

لَا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ44

usio na mashukio baridi wala mandhari mazuri.
56:45Juzuu 27 · uk. 535

إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ45

Kwani wao walikuwa duniani wakijistarehesha kwa vitu vya haramu wakijiepusha na yale ambayo Mitume walikuja nayo.
56:46Juzuu 27 · uk. 535

وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنْثِ الْعَظِيمِ46

Na walikuwa wamesimama wima katika kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumshirikisha na kumuasi, na hawakuwa na nia ya kutubia kwa hayo.
56:47Juzuu 27 · uk. 535

وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ47

Na walikuwa wakisema hali ya kukanusha Ufufuzi, «Je hivi sisi tutafufuliwa tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa iliyochakaa?» Maneno yao hayo yanaonesha kuwa wao walikuwa wakiliona jambo hili la kufufuliwa kuwa liko mbali na ukweli na wakilikanusha.
56:48Juzuu 27 · uk. 535

أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ48

«Je tutafufuliwa sisi na hali baba zetu waliotangulia wamekuwa mchanga uliotapakaa kwenye ardhi?»
56:49Juzuu 27 · uk. 535

قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ49

Sema uwaambie, «Hakika wa mwanzo na wa mwisho miongoni mwa binadamu
56:50Juzuu 27 · uk. 535

لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَعْلُومٍ50

watakusanywa katika Siku iliyowekewa wakati maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama.
56:51Juzuu 27 · uk. 536

ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ51

«Kisha nyinyi, enyi mliopotea njia ya uongofu mnaokanusha onyo la Mwenyezi Mungu na agizo Lake,
56:52Juzuu 27 · uk. 536

لَآكِلُونَ مِنْ شَجَرٍ مِنْ زَقُّومٍ52

ni wenye kula kutokana na mti wa zaqqūm,
56:53Juzuu 27 · uk. 536

فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ53

nao ni katika miti mibaya zaidi, na ni wenye kujaza matumbo yenu kutokana nao kwa sababu ya ukali wa njaa,
56:54Juzuu 27 · uk. 536

فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ54

na ni wenye kunywa juu yake maji yaliyo moto hadi ya mwisho, yasiyomaliza kiu.
56:55Juzuu 27 · uk. 536

فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ55

Mtayanywa maji hayo kwa wingi kama vile ngamia wenye kiu wasioshiba maji kwa ugonjwa uliowapata.»
56:56Juzuu 27 · uk. 536

هَٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ56

Adhabu hii watakayoipata ndiyo zawadi Aliyowaandalia Siku ya Kiyama. Katika haya kuna kuwalaumu na kuwacheza shere.
56:57Juzuu 27 · uk. 536

نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ57

Sisi tumewaumba, enyi watu, na hamkuwa kitu chochote. Basi si msadiki kuwa kuna kufufuliwa?
56:58Juzuu 27 · uk. 536

أَفَرَأَيْتُمْ مَا تُمْنُونَ58

Mnayaonaje maji ya manii mnayoyatupa ndani ya vizazi vya wake zenu,
56:59Juzuu 27 · uk. 536

أَأَنْتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ59

je nyinyi ndio mnaomuumba mwanadamu kutokana na hayo au ni sisi ndio wenye kuumba?
56:60Juzuu 27 · uk. 536

نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ60

Sisi tumekadiria kifo kwenu,
56:61Juzuu 27 · uk. 536

عَلَىٰ أَنْ نُبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنْشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ61

na sisi si wenye kushindwa kubadilisha umbo lenu Siku ya Kiyama na kuwaumba kwa sifa na namna msizozijua.
56:62Juzuu 27 · uk. 536

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ62

Na hakika mlijua kuwa Mwenyezi Mungu Aliwaumba uumbaji wa kwanza na hamkuwa kitu chochote. Basi si mkumbuke uweza wa Mwenyezi Mungu wa kuwaumba mara nyingine?
56:63Juzuu 27 · uk. 536

أَفَرَأَيْتُمْ مَا تَحْرُثُونَ63

Mnazionaje mbegu mnazozipanda?
56:64Juzuu 27 · uk. 536

أَأَنْتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ64

Je ni nyinyi mnaoziotesha kutoka ardhini? Sisi ndio tuaozituliza na kuziotesha ardhini.
56:65Juzuu 27 · uk. 536

لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ65

Lau tungalitaka tungaliifanya mimea inayotokana na mbegu hizo kuwa mapepe, haimkiniki kunufaika nayo kwa kula,
56:66Juzuu 27 · uk. 536

إِنَّا لَمُغْرَمُونَ66

mkawa mnaona ajabu kwa kilichoshukia mimea yenu na mnasema, «Sisi tumepata hasara na ni wenye kuungulika.
56:67Juzuu 27 · uk. 536

بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ67

Bali sisi tumekoseshwa riziki.»
56:68Juzuu 27 · uk. 536

أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ68

Mnayaonaje maji mnayokunywa ili mhuike kwayo?
56:69Juzuu 27 · uk. 536

أَأَنْتُمْ أَنْزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنْزِلُونَ69

Je ni nyinyi mliyoyateremsha kutoka kwenye mawingu hadi kwenye kituo cha ardhi au ni sisi tuliyoyateremsha ili kuwarehemu nyinyi?
56:70Juzuu 27 · uk. 536

لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ70

Lau tungalitaka tungaliyafanya maji haya yawe na chumvi sana, ikiwa haiwezekani kunufaika nayo kwa kunywa wala kwa mimea. Basi si mumshukuru Mola wenu kwa kuteremsha maji tamu kwa kuwanufaisha nyinyi.
56:71Juzuu 27 · uk. 536

أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ71

Mnaouonaje moto mnaouwasha?
56:72Juzuu 27 · uk. 536

أَأَنْتُمْ أَنْشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنْشِئُونَ72

Je ni nyinyi mlioufanya mti wake, unaozalisha moto kwa kukwaruzwa, upatikane au ni sisi tulioufanya upatikane?
56:73Juzuu 27 · uk. 536

نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَةً وَمَتَاعًا لِلْمُقْوِينَ73

Sisi tumeufanya moto wenu mnaouwasha ni ukumbusho kwenu wa Moto wa Jahanamu na pia ni manufaa kwa wasafiri.
56:74Juzuu 27 · uk. 536

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ74

Basi mtakase Mola wako, ewe Nabii, Aliye mtukufu Mwenye ukamilifu wa majina na sifa, Mwingi wa wema na kheri.
56:75Juzuu 27 · uk. 536

۞ فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ75

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mapomoko ya nyota nyakati za kuzama kwake mbinguni.
56:76Juzuu 27 · uk. 536

وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ76

Nacho ni kiapo kikubwa lau mnajua kadiri yake.
56:77Juzuu 27 · uk. 537

إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ77

Hakika hii Qur’ani iliyoteremshiwa Muhammad ni Qur’ani yenye manufaa makubwa, yenye kheri nyingi na yenye elimu tele,
56:78Juzuu 27 · uk. 537

فِي كِتَابٍ مَكْنُونٍ78

iliyo ndani ya Kitabu kilichohifadhiwa, kilichofichwa na macho ya viumbe, nacho ni Kitabu ambacho kiko mikononi mwa Malaika.

لَا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ79

Hawaigusi Qur’ani isipokuwa malaika watukufu ambao Mwenyezi Mungu Amewasafisha na aibu na madhambi. Na pia hawaigusi isipokuwa watu waliojitohirisha na ushirikina na janaba na ukosefu wa udhu.
56:80Juzuu 27 · uk. 537

تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ80

Na hii Qur’ani tukufu imeteremshwa kutoka kwa Mola wa viumbe vyote, kwani hiyo ndiyo haki isiyo na shaka ndani yake.
56:81Juzuu 27 · uk. 537

أَفَبِهَٰذَا الْحَدِيثِ أَنْتُمْ مُدْهِنُونَ81

je hii Qur’ani, enyi washirikina, mnaikanusha?
56:82Juzuu 27 · uk. 537

وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ82

Na je mnaifanya shukrani yenu kwa neema za Mola wenu ni kuwa nyinyi mnazikanusha na kukufuru? Hapa pana makaripio kwa anayedharau amri za Qur’ani na kutojali mwito wake.
56:83Juzuu 27 · uk. 537

فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ83

Basi je mnaweza pindi roho ya mmoja wenu inapofika kwenye koo katika uchungu wa kifo,
56:84Juzuu 27 · uk. 537

وَأَنْتُمْ حِينَئِذٍ تَنْظُرُونَ84

na hali nyinyi mmehudhuria mnamtazama, kuizuia roho yake ndani ya mwili wake? Hamtaweza hilo!
56:85Juzuu 27 · uk. 537

وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْكُمْ وَلَٰكِنْ لَا تُبْصِرُونَ85

Na sisi tuko karibu na yeye zaidi, kupitia Malaika wetu, kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamuwaoni.
56:86Juzuu 27 · uk. 537

فَلَوْلَا إِنْ كُنْتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ86

Na je mnaweza, iwapo nyinyi si wenye kuhesabiwa wala kulipwa kwa matendo yenu,
56:87Juzuu 27 · uk. 537

تَرْجِعُونَهَا إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ87

kuirudisha roho kwenye mwili, iwapo nyinyi ni wakweli? Hamtaweza kuirudisha.
56:88Juzuu 27 · uk. 537

فَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ88

Basi iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia, atapata rehema kunjufu na furaha,
56:89Juzuu 27 · uk. 537

فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ89

wakati wa kufa kwake, na kila kinachoifurahisha nafsi yake, Na atapata Pepo ya starehe huko Akhera.
56:90Juzuu 27 · uk. 537

وَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ90

Na iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia,
56:91Juzuu 27 · uk. 537

فَسَلَامٌ لَكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ91

ataambiwa, «Umesalimika na kuwa kwenye amani, kwa kuwa wewe ni miongoni mwa watu wa upande wa kulia.»
56:92Juzuu 27 · uk. 537

وَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ92

Na iwapo yule anayekufa ni miongoni mwa wenye kukanusha kufufuliwa, waliopotoka na njia ya uongofu,
56:93Juzuu 27 · uk. 537

فَنُزُلٌ مِنْ حَمِيمٍ93

basi atapata makaribisho ya kinywaji cha moto wa Jahanamu kilichochemshwa, kilicho na joto hadi ya mwisho,
56:94Juzuu 27 · uk. 537

وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ94

na atachomwa na Moto na aungulike na adhabu yake kali.
56:95Juzuu 27 · uk. 537

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ95

Hakika habari hii tumezokuelezea, ewe Mtume, ni ukweli wa yakini usio na shaka.
56:96Juzuu 27 · uk. 537

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ96

Basi litakase jina la Mola wako Aliyetukuka na umtakase na yale ambayo madhalimu na wenye kukanusha wanayasema. Mwenyezi Mungu Yuko juu ya yale wanayoyasema ujuu mkubwa sana.

Cheza kutoka mwanzo wa sura