An-Najm

سورة النجم

Sura 53 · Makki · 62 aya

53:1Juzuu 27 · uk. 526

وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ1

Anaapa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa nyota zinapozama zikawa hazionekani
53:2Juzuu 27 · uk. 526

مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ2

kwamba Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, hakupotoka kwenye njia ya uongofu na haki, na hakutoka nje ya njia ya usawa. Bali yeye yuko kwenye upeo wa unyofu, usawa na uthabiti.
53:3Juzuu 27 · uk. 526

وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ3

Kutamka kwake hakutokani na matamanio ya nafsi yake. Haikuwa
53:4Juzuu 27 · uk. 526

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ4

Qur’ani na haikuwa Sunnah isipokuwa ni wahyi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Nabii Wake Muahammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
53:5Juzuu 27 · uk. 526

عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ5

Alimfundisha Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, Malaika mwenye nguvu nyingi,
53:6Juzuu 27 · uk. 526

ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ6

mwenye mandhari mazuri, naye ni Jibrili, amani imshukie, aliyejitokeza kwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,
53:7Juzuu 27 · uk. 526

وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ7

na akalingana kwa umbo lake la kihakika, kwenye pembe za sehemu za juu, nao ni pembe za jua linapochomoza.
53:8Juzuu 27 · uk. 526

ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ8

Kisha Jibrili akakaribia kwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,
53:9Juzuu 27 · uk. 526

فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ9

na akazidi kukaribia mpaka ikawa kukaribia kwake ni kiasi cha nyuta mbili au karibu zaidi.
53:10Juzuu 27 · uk. 526

فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ10

Hapo Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, alimpelekea wahyi mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kile alichokituma kwa wahyi kupitia Jibrili, amani imshukie.
53:11Juzuu 27 · uk. 526

مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ11

Haukukanusha moyo wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kile alichokiona kwa macho yake.
53:12Juzuu 27 · uk. 526

أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ12

Je mnamkanusha Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amni zimshukie, mkajadiliana naye juu ya kile alichokiona na kukishuhudia miongoni mwa alama za Mola wake?
53:13Juzuu 27 · uk. 526

وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ13

Na Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alimuona Jibrili, kwa sura zake za uhakika Alizomuumba nazo Mwenyezi Mungu,
53:14Juzuu 27 · uk. 526

عِنْدَ سِدْرَةِ الْمُنْتَهَىٰ14

mara nyingine hapo penye Sidrah al-Muntahā- mti wa mkunazi ulio kwenye uwingu wa saba ambapo hapo kinakomea kinachopanda juu kutoka ardhini na kinakomea kinachoshuka chini kutoka juu yake.
53:15Juzuu 27 · uk. 526

عِنْدَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ15

Mbele ya mti huo kuna Pepo ya al- Ma’wā (Makazi ya Daima) ambayo waliahidiwa wachamungu.
53:16Juzuu 27 · uk. 526

إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ16

Pindi huo Mkunazi ulipofinikwa kutokana na amri ya Mwenyezi Mungu na kitu kikubwa hakuna ajuaye sifa zake isipokuwa Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka.
53:17Juzuu 27 · uk. 526

مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ17

Na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikuwa na sifa kubwa ya uthabiti na utiifu, hayakupotoka macho yake kuliani wala kushotoni, wala hakupitisha zaidi ya kile alichoamrishwa kukiona.
53:18Juzuu 27 · uk. 526

لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ18

Hakika Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, aliona, usiku wa Mi'rāj (kwenda mbinguni) alama kubwa zinazojulisha uweza wa Mwenyezi Mungu na ukubwa Wake miongoni mwa Pepo, Moto na vinginevyo.
53:19Juzuu 27 · uk. 526

أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ19

Mnawaonaje, enyi washirikina, waungu hawa mnaowaabudu: Lāta, 'Uzzā
53:20Juzuu 27 · uk. 526

وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَىٰ20

na mwingine wa tatu ni Manātu, je hao wamenufaisha au kudhuru mpaka wawe ni washirika wa Mwenyezi Mungu?
53:21Juzuu 27 · uk. 526

أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الْأُنْثَىٰ21

Je huyu mwanamume mnamfanya ni wenu kwa kuwa mnaridhika naye, na mwanamke ambaye hamridhiki naye nyinyi wenyewe mnamfanya ni wa Mwenyezi Mungu?
53:22Juzuu 27 · uk. 526

تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ22

Hiko ni kigawanyo cha kidhalimu. Hawakuwa hawa masanamu isipokuwa majina yasiyokuwa na sifa zozote za ukamilifu.
53:23Juzuu 27 · uk. 526

إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنْتُمْ وَآبَاؤُكُمْ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ بِهَا مِنْ سُلْطَانٍ ۚ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الْأَنْفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُمْ مِنْ رَبِّهِمُ الْهُدَىٰ23

Hayo si chochote isipokuwa ni majina mliyoyaita nyinyi na baba zenu kulingana na matamanio yenu yaliyo batili, Mwenyezi Mungu hakuteremsha ushahidi wowote wa kusadikisha madai yenu juu ya hayo. Hawafuati hawa washirikina isipokuwa dhana na matamanio ya nafsi zao zilizopotoka zikawa kando na maumbile ya sawa. Na hakika yaliwajia wao kutoka kwa Mola wao, kwa ulimi wa Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yale ambayo ndani yake pana uongofu wao, na wao hawakunufaika nao.
53:24Juzuu 27 · uk. 526

أَمْ لِلْإِنْسَانِ مَا تَمَنَّىٰ24

Binadamu hatapata kile anachokitamani cha kuwa waabudiwa hawa au wasiokuwa hawa, katika vitu vinavyotamaniwa na nafsi yake, watamuombea.
53:25Juzuu 27 · uk. 526

فَلِلَّهِ الْآخِرَةُ وَالْأُولَىٰ25

Basi ni ya Mwenyezi Mungu amri ya duniani na Akhera.
53:26Juzuu 27 · uk. 526

۞ وَكَمْ مِنْ مَلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِنْ بَعْدِ أَنْ يَأْذَنَ اللَّهُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ26

Na kuna Malaika wengi huko mbinguni, pamoja na vyeo vyao vya juu, kuombea kwao hakunufaishi chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kuwapa idhini wao waombee na Aridhike na yule mwenye kuombewa.
53:27Juzuu 27 · uk. 527

إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلَائِكَةَ تَسْمِيَةَ الْأُنْثَىٰ27

Hakika wale ambao hawaamini kuwa kuna maisha ya Akhera miongoni mwa makafiri wa Kiarabu wala hawafanyi matendo ya kuwafaa huko, wanawaita Malaika vile wanavyowaita wanawake, kwa kuitakidi kwao kuwa Malaika ni wanawake na kuwa wao ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu.
53:28Juzuu 27 · uk. 527

وَمَا لَهُمْ بِهِ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ ۖ وَإِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا28

Na wao hawana ujuzi wowote ulio sahihi, kuhusu jambo hilo, wenye kusadikisha hayo waliyoyasema. Hawafuati isipokuwa dhana ambayo haifalii kitu na haisimami kabisa mahali pa haki.
53:29Juzuu 27 · uk. 527

فَأَعْرِضْ عَنْ مَنْ تَوَلَّىٰ عَنْ ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا29

Basi mpuuze yule anaoupa mgongo utajo wetu, nao ni Qur’ani, na asitake chochote isipokuwa uhai wa kilimwengu.
53:30Juzuu 27 · uk. 527

ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُمْ مِنَ الْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنْ ضَلَّ عَنْ سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اهْتَدَىٰ30

Hali hiyo waliyonayo ndio upeo wa ujuzi wao na lengo lao. Hakika Mola wako Ndiye Anayemjua zaidi aliyepotoka kutoka kwenye njia ya uongofu, na Yeye ndiye Anayemjua zaidi aliyeongoka na akafuata njia ya Uislamu.. Hapa pana onyo kali kwa wenye kuasi na kukataa kukitumia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kufuata mwenendo wa Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wenye kufadhilisha matamanio ya nafsi na hadhi za ulimwenguni juu ya Akhera.
53:31Juzuu 27 · uk. 527

وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى31

Ni ya Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, mamlaka ya vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, ili Awalipe wale waliokosa kwa kuwatesa kwa maovu waliyoyafanya na Awalipe Pepo wale waliofanya wema,
53:32Juzuu 27 · uk. 527

الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنْشَأَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنْتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنْفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ32

nao ni wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa dhambi ndogondogo nazo ni dhambi ndogo ambazo haendelei nazo mwenye kuzifanya, au zile ambazo mja amezifanya kwa nadra. Kwani hizo pamoja na kufanya mambo ya wajibu na kujiepusha na mambo ya haramu, Atayasamehe nayo Mwenyezi Mungu na Atawasitiria. Hakika Mola wako ni Mkunjufu wa msamaha. Yeye Anazijua zaidi hali zenu Alipomuumba baba yenu Ādam kwa mchanga, na mlipokuwa bado hamjazaliwa, mko ndani ya matumbo ya mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu, mkazipamba na mkazipa sifa za uchamungu. Yeye Anamjua zaidi anayeogopa mateso Yake miongoni mwa waja Wake na akajiepusha na kufanya mambo ya kumuasi.
53:33Juzuu 27 · uk. 527

أَفَرَأَيْتَ الَّذِي تَوَلَّىٰ33

Unamuonaje, ewe Mtume, yule anayekataa kumtii Mwenyezi Mungu
53:34Juzuu 27 · uk. 527

وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰ34

na akatoa kidogo katika mali yake kisha akaacha kutoa na akakata hisani yake?
53:35Juzuu 27 · uk. 527

أَعِنْدَهُ عِلْمُ الْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰ35

Je huyu anayekata kheri yake ya kutoa ana ujuzi wa ghaibu kuwa yeye atamalizikiwa na mali yaliyoko mkononi mwake ndipo akaizuia kheri yake asiitoe, na akawa aliona hilo waziwazi? Mambo si hivyo! Hakika ni kwamba yeye aliacha kutoa sadaka na kufanya kheri, kutenda wema na kuunga kizazi kwa ubahili na uchoyo.
53:36Juzuu 27 · uk. 527

أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ36

Kwani hakupewa habari ya yaliyomo ndani ya kurasa za Taurati
53:37Juzuu 27 · uk. 527

وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّىٰ37

na nyaraka za Ibrāhīm aliyetekeleza kile alichoamrishwa na akakifikisha?
53:38Juzuu 27 · uk. 527

أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ38

Kwamba haipatilizwi nafsi yoyote kwa kosa la nafsi nyingine, na mzigo wake hakuna yoyote atakayembebea.
53:39Juzuu 27 · uk. 527

وَأَنْ لَيْسَ لِلْإِنْسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ39

Na kwamba binadamu hapewi malipo isipokuwa kwa kile alichokichuma yeye mwenyewe kwa juhudi zake.
53:40Juzuu 27 · uk. 527

وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ40

Na kwamba juhudi zake zitaonekana Akhera, yapambanuliwe mazuri yake na mabaya yake, ili kumkirimu mtenda wema na kumlaumu mfanya mabaya.
53:41Juzuu 27 · uk. 527

ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ41

kisha binadamu atalipwa kwa juhudi zake malipo yenye kuenea kikamilifu matendo yake yote.
53:42Juzuu 27 · uk. 527

وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الْمُنْتَهَىٰ42

Na kwamba kwa Mola wako, ewe Mtume, ndipo watakapokomea viumbe Vyake vyote Siku ya Kiyama.
53:43Juzuu 27 · uk. 527

وَأَنَّهُ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ43

Na kwamba Yeye, Aliyetukuka na kutakasika, Ndiye Anayemfanya Anayemtaka acheke duniani kwa kumfurahisha, na ndiye Anayemfanya Anayemtaka alie kwa kumpa makero.
53:44Juzuu 27 · uk. 527

وَأَنَّهُ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا44

Na kwamba Yeye Ndiye Anayemfisha Anayetaka afe miongoni mwa vuimbe Vyake na Ndiye Anayemuhuisha Anayetaka ahuike miongoni mwao. Basi Yeye Ndiye Aliyepwekeka, kutakasika ni Kwake, kwa kuhuisha na kufisha.
53:45Juzuu 27 · uk. 528

وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنْثَىٰ45

Na kwamba Yeye Ameumba jinsi mbili: ya kiume na ya kike, kati ya wanadamu na wanyama,
53:46Juzuu 27 · uk. 528

مِنْ نُطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ46

kutokana na tone la manii linalomiminwa kwenye kizazi.
53:47Juzuu 27 · uk. 528

وَأَنَّ عَلَيْهِ النَّشْأَةَ الْأُخْرَىٰ47

Na kwamba ni juu ya Mola wako, ewe Mtume, kurejesha uumbaji wao baada ya kufa kwao, na huo ndio uumbaji mwingine Siku ya Kiyama.
53:48Juzuu 27 · uk. 528

وَأَنَّهُ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ48

Na Yeye Ndiye Anayewatajirisha Anaowataka miongoni mwa viumbe Wake kwa mali, na Ndiye Anayewamilikisha na kuwaridhisha nayo.
53:49Juzuu 27 · uk. 528

وَأَنَّهُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَىٰ49

Na kwamba Yeye Ndiye Mola wa al-Shi'rā, nayo ni nyota inayong’ara ambayo baadhi ya watu wa zama za Ujinga walikuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu.
53:50Juzuu 27 · uk. 528

وَأَنَّهُ أَهْلَكَ عَادًا الْأُولَىٰ50

Na kwamba Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, Aliwaangamiza 'Ād wa mwanzo, nao ni watu wa Hūd.
53:51Juzuu 27 · uk. 528

وَثَمُودَ فَمَا أَبْقَىٰ51

Na Akawaangamiza Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, Asimbakishe yoyote katika wao.
53:52Juzuu 27 · uk. 528

وَقَوْمَ نُوحٍ مِنْ قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ52

Na Akawaangamiza watu wa Nūḥ hapo kabla. Hao walikuwa ni wakali zaidi wa uasi na wakubwa zaidi wa ukafiri kuliko wale waliokuja baada yao.
53:53Juzuu 27 · uk. 528

وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ53

Na miji ya watu wa Lūṭ, Mwenyezi Mungu Aliipindua juu yao Akazifanya sehemu za juu yake kuwa chini yake
53:54Juzuu 27 · uk. 528

فَغَشَّاهَا مَا غَشَّىٰ54

na Akaifinika mawe yaliyowateremkia kwa mfululiza kutoka juu kama mvua.
53:55Juzuu 27 · uk. 528

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ55

Basi ni neema zipi za Mola wako, ewe binadamu mkanushaji, unazifanyia shaka?
53:56Juzuu 27 · uk. 528

هَٰذَا نَذِيرٌ مِنَ النُّذُرِ الْأُولَىٰ56

Huyu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni mwonyaji wa haki ambayo kwayo walionya Manabii kabla yake, si kitu kipya katika Mitume.
53:57Juzuu 27 · uk. 528

أَزِفَتِ الْآزِفَةُ57

Kiyama kimekaribia na wakati wake umekaribia.
53:58Juzuu 27 · uk. 528

لَيْسَ لَهَا مِنْ دُونِ اللَّهِ كَاشِفَةٌ58

Hivyo basi hakuna yoyote mwenye kukizuia isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna mwenye kujua wakati wa kufika kwake isipokuwa Mwenyezi Mungu.
53:59Juzuu 27 · uk. 528

أَفَمِنْ هَٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ59

Je hii Qur’ani mnaionea ajabu, enyi washirikina, kuwa ni sahihi.
53:60Juzuu 27 · uk. 528

وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ60

Na mnaicheka kwa shere nastihzai na hamlii kwa kuogopa maonyo yake,
53:61Juzuu 27 · uk. 528

وَأَنْتُمْ سَامِدُونَ61

na hali nyinyi mnapumbaa na mmeipa mgongo?
53:62Juzuu 27 · uk. 528

فَاسْجُدُوا لِلَّهِ وَاعْبُدُوا ۩62

Basi msujudieni Mwenyezi Mungu na mtakasieni Ibada Yeye Peke Yake, Na mumuachie Yeye mambo yenu.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Fares Abbad - An-Najm · Tlawati