Ash-Sharh

سورة الشرح

Sura 94 · Makki · 8 aya

94:1Juzuu 30 · uk. 596

أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ1

Kwani Hatukukunjulia, ewe Mtume, kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa tabia nzuri,
94:2Juzuu 30 · uk. 596

وَوَضَعْنَا عَنْكَ وِزْرَكَ2

Tukakuondolea mazito yako yaliyoemea mgongo wako
94:3Juzuu 30 · uk. 597

الَّذِي أَنْقَضَ ظَهْرَكَ3

na Tukakuweka, kwa matukufu Tuliyokuneemesha,
94:4Juzuu 30 · uk. 597

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ4

kwenye cheo cha juu?

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا5

Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa makero ya maadui zako. Kwani kwenye dhiki kuna faraji.
94:7Juzuu 30 · uk. 597

فَإِذَا فَرَغْتَ فَانْصَبْ7

Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada.
94:8Juzuu 30 · uk. 597

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَبْ8

Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Ali Jaber - Ash-Sharh · Tlawati