Ar-Rahman

سورة الرحمن

Sura 55 · Makki · 78 aya

55:1Juzuu 27 · uk. 531

الرَّحْمَٰنُ1

mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema
55:2Juzuu 27 · uk. 531

عَلَّمَ الْقُرْآنَ2

Amemfundisha binadamu Qur’ani kwa kurahisisha kuisoma, kuihifadhi na kuelewa maana yake.
55:3Juzuu 27 · uk. 531

خَلَقَ الْإِنْسَانَ3

Amemuumba binadamu,
55:4Juzuu 27 · uk. 531

عَلَّمَهُ الْبَيَانَ4

Amemfundisha ufasaha wa kujieleza ili kumtenganisha na wengine.
55:5Juzuu 27 · uk. 531

الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ5

Jua na mwezi zinatembea kwa kufuatana, moja baada ya nyingine, kwa hesabu madhubuti isiyotafautiana wala kugongana.
55:6Juzuu 27 · uk. 531

وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ6

Na nyota iliyo mbinguni na miti ya ardhini, vinamjua Mola wao, vinamsujudia na vinanyosha shingo zao kufuata vile ambavyo vimepangiwa vifuate vya maslahi ya waja Wake na manufaa yao.
55:7Juzuu 27 · uk. 531

وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ7

Na mbingu Ameiinua na kuifanya iwe juu ya ardhi, Na Ameweka kwenye ardhi uadilifu Aliouamrisha na kuulazimisha kwa waja Wake.
55:8Juzuu 27 · uk. 531

أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ8

Ili msipite mipaka na msimfanyie hiyana mnayempimia.
55:9Juzuu 27 · uk. 531

وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ9

Na simamisheni upimaji kwa usawa na msipunguze mizani mnapowapimia watu.
55:10Juzuu 27 · uk. 531

وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ10

Na ardhi Ameiweka na Ameitayarisha, ili viumbe vitulie juu yake.
55:11Juzuu 27 · uk. 531

فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ11

Humo mna matunda na mitende yenye makarara ya matunda. Na humo kuna nafaka zenye maganda, vikiwa ni chakula chenu na wanyama wenu.
55:12Juzuu 27 · uk. 531

وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ12

Na humo mna kila mmea wenye harufu nzuri.

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ13

Bas ni neema gani za Mola wenu, za kidini na za kidunia, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha? Na ni jawabu nzuri ilioje ya majini alipowasomea wao Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, sura hii, kila akipita kwenye aya hii walikuwa wakisema, «Hakuna chochote miongoni mwa neema zako, ewe Mola wetu, tunachokanusha. Sifa njema zote ni zako.» Na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa mja anapoelezewa neema za Mwenyezi Mungu na mema Yake akubali na amshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
55:14Juzuu 27 · uk. 531

خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ14

Amemuumba baba wa wanadamu, naye ni Ādam, kwa udongo mkavu kama vyungu.
55:15Juzuu 27 · uk. 531

وَخَلَقَ الْجَانَّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ15

Na Amemuumba Iblisi, naye ni katika majini, kwa mroromo wa moto uliochanganyika.
55:16Juzuu 27 · uk. 531

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ16

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:17Juzuu 27 · uk. 531

رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ17

Mola wa pande mbili za Mashariki ya jua, katika kusi na kaskazi, na Mola wa pande mbili za Magharibi ya jua, katika kusi na kaskazi, kwani vyote viko chini ya uendeshaji Wake na ulezi Wake..
55:18Juzuu 27 · uk. 531

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ18

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:19Juzuu 27 · uk. 532

مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ19

Mwenyezi Mungu Ameyachanganya maji ya bahari mbili, tamu na chumvi, yanakutana, baina yake kuna kizuizi,
55:20Juzuu 27 · uk. 532

بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَا يَبْغِيَانِ20

mojawapo haiingii sehemu ya nyingine na kuiondoa sifa yake, bali ya tamu inasalia kuwa tamu na ya chumvi inasalia kuwa chumvi pamoja na kukutana kwake.
55:21Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ21

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:22Juzuu 27 · uk. 532

يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ22

Inatoka kwenye bahari mbili hizo, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, lulu na marjani.
55:23Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ23

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:24Juzuu 27 · uk. 532

وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنْشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ24

Ni Yake Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, mamlaka ya kuyaendesha majahazi makubwa yanayotembea baharini kwa manufaa ya watu, yenye kusimamisha juu milongoti yake na matanga yake kama vile majabali.
55:25Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ25

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu mnazikanusha?
55:26Juzuu 27 · uk. 532

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ26

Kila aliye juu ya uso wa ardhi miongoni mwa viumbe ni mwenye kuangamia,
55:27Juzuu 27 · uk. 532

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ27

na utasalia uso wa Mola wako Mwenye utukufu, ubora, kheri nyingi na upaji. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya uso kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inavyonasibiana na Yeye, kutakasika ni Kwake, bila kufananisha wala kueleza namna ulivyo.
55:28Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ28

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:29Juzuu 27 · uk. 532

يَسْأَلُهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ29

Wanamuomba Yeye walioko mbinguni na ardhini haja zao. Hakuna yoyote anayejitosheleza kutomhitajia Yeye, kutakasika ni Kwake. Kila siku Yeye Yuko kwenye jambo: Anatukuza na Anatweza, Anatoa na Anazuia.
55:30Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ30

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:31Juzuu 27 · uk. 532

سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ31

Nitawatengea kipindi cha kuwahesabu na kuwalipa kwa matendo yenu mliyoyafanya, enyi vizito viwili:-majini na binadamu-, tuwatese watu wa maasia na tuwape malipo mema watu wa utiifu.
55:32Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ32

Ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:33Juzuu 27 · uk. 532

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَنْ تَنْفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانْفُذُوا ۚ لَا تَنْفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ33

Enyi mkusanyiko wa majini na binadamu! Mkiweza kuihepa amri ya Mwenyezi Mungu na uamuzi Wake kwa kukimbia kwenye pambe za mbingu na ardhi basi fanyeni, na hamuwezi kufanya hivyo isipokuwa kwa nguvu na hoja na amri inayotoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. (Na vipi mtaweza kufanya hivyo na hali nyinyi hamzimilikii nafsi zenu manufaa yoyote wala madhara?).
55:34Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ34

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:35Juzuu 27 · uk. 532

يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِنْ نَارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنْتَصِرَانِ35

Mtatumiwa mroromo wa moto na shaba iliyoyayushwa, mmiminiwe juu ya vichwa vyenu msiweze kusaidiana.
55:36Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ36

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazukanusha?
55:37Juzuu 27 · uk. 532

فَإِذَا انْشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ37

Na pindi mbingu itakapopasuka na kuachana Siku ya Kiyama, ikawa nyekundu kama rangi ya waridi na kama mafuta yaliyochemshwa na risasi iliyoyayushwa, kutokana na mambo magumu na vituko vya Siku ya Kiyama.
55:38Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ38

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:39Juzuu 27 · uk. 532

فَيَوْمَئِذٍ لَا يُسْأَلُ عَنْ ذَنْبِهِ إِنْسٌ وَلَا جَانٌّ39

Katika Siku hiyo Malaika hawatawauliza wale wahalifu, miongoni mwa binadamu na majini, kuhusu dhambi zao.
55:40Juzuu 27 · uk. 532

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ40

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:41Juzuu 27 · uk. 532

يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ41

Malaika watawajua wahalifu kwa alama zao, hapo wawashike kwenye paa za vichwa vyao na nyayo zao wawarushe Motoni.
55:42Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ42

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:43Juzuu 27 · uk. 533

هَٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ43

Wataambiwa hao wahalifu kwa njia ya kulaumiwa na kudhalilishwa, «Huu ndio moto wa Jahanamu ambao wahalifu duniani walikuwa wakiukanusha:
55:44Juzuu 27 · uk. 533

يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ44

mara wanaadhibiwa kwenye Jaḥīm, na mara nyingine wananyweshwa Hāmīm, nacho ni kinywaji kilichofikia upeo wa ukali wa moto, kinakata tumbo na sehemu za ndani ya mbavu.
55:45Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ45

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu mnazikanusha?
55:46Juzuu 27 · uk. 533

وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ46

Na anayemcha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa waja Wake binadamu na majini, akaogopa kusimama kwake mbele Yake, akamtii na akaacha kumuasi atakuwa na mabustani mawili ya Pepo.
55:47Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ47

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:48Juzuu 27 · uk. 533

ذَوَاتَا أَفْنَانٍ48

Mabustani mawili hayo ya Pepo yana matawi yaliyostawi kwa matunda ya kila aina.
55:49Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ49

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:50Juzuu 27 · uk. 533

فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ50

Katika Pepo mbili hizo kuna chemchemi mbili za maji zinazopita katikati yake.
55:51Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ51

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:52Juzuu 27 · uk. 533

فِيهِمَا مِنْ كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ52

Katika mabustani hayo mawili ya Pepo kuna sampuli mbili za kila aina ya matunda.
55:53Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ53

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:54Juzuu 27 · uk. 533

مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ54

Na wale wanaoogopa kusimama mbele ya Mola Wao watakuwa na mabustani mawili ya Pepo, ambayo ndani yake watastarehe, hali ya kutegemea juu ya matandiko yaliyojazwa dibaji nzito. Na matunda ya mabustani mawili hayo ya pepo yako karibu nao.
55:55Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ55

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mtazikanusha?
55:56Juzuu 27 · uk. 533

فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ56

Katika matandiko hayo wapo wake macho yao yanawatazama waume zao tu, hawawatazami wengineo, wamefungamana na wao. Hakuna aliyewaingilia, kabla ya hao waume zao, binadamu yoyote wala jini.
55:57Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ57

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadanu, mnazikanusha?
55:58Juzuu 27 · uk. 533

كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ58

Kama kwamba hawa wake wa kihurulaini ni yakuti na marijani katika sifa zao na uzuri wao.
55:59Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ59

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa najini na binadamu , mnazikanusha?
55:60Juzuu 27 · uk. 533

هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ60

Je atakuwa na malipo yoyote, huyu aliyekuwa mwema wa matendo duniani, isipokuwa ni afanyiwe wema kwa kupewa Pepo huko Akhera?
55:61Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ61

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:62Juzuu 27 · uk. 533

وَمِنْ دُونِهِمَا جَنَّتَانِ62

Na chini ya mabustani ya Pepo mawili yaliyotangulia kuna mabustani ya Pepo mawili mengine.
55:63Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ63

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:64Juzuu 27 · uk. 533

مُدْهَامَّتَانِ64

Mabustani haya mawili ni rangi ya kijani. Ujani wake umeiva sana mapaka umeingia kwenye weusi.
55:65Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ65

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:66Juzuu 27 · uk. 533

فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ66

Ndani ya mabustani mawili hayo ya Peponi kuna chemchemi mbili zenye kububujika maji daima bila kukatika.
55:67Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ67

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:68Juzuu 27 · uk. 533

فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ68

Kwenye mabustani hayo mawili kuna aina za matunda, mitende na mikomamanga.
55:69Juzuu 27 · uk. 533

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ69

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:70Juzuu 27 · uk. 534

فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ70

Ndani ya mabustani haya manne ya Pepo kuna wake walio wema wa tabia na wazuri wa nyuso.
55:71Juzuu 27 · uk. 534

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ71

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:72Juzuu 27 · uk. 534

حُورٌ مَقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ72

Mahurulaini wakunjufu wa macho, waliositiriwa na kuhifadhiwa mahemani.
55:73Juzuu 27 · uk. 534

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ73

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:74Juzuu 27 · uk. 534

لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ74

Hawajaingiliwa Mahurulaini hawa na binadamu yoyote wala jini kabla ya waume zao.
55:75Juzuu 27 · uk. 534

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ75

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:76Juzuu 27 · uk. 534

مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ76

Hali ya kuwa wametegemea kwenye mito yenye mifuko rangi ya kijani na matandiko mazuri.
55:77Juzuu 27 · uk. 534

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ77

Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
55:78Juzuu 27 · uk. 534

تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ78

Zimekithiri mno baraka za Jina la Mola wako, na kheri Zake zimekuwa nyingi, Mwenye haiba kubwa, utukufu wenye kukamilika na takrima kwa wenye kumtegemea Yeye.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Ali Jaber - Ar-Rahman · Tlawati