Al-Ma'un

سورة الماعون

Sura 107 · Makki · 7 aya

107:1Juzuu 30 · uk. 602

أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ1

Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa?
107:2Juzuu 30 · uk. 602

فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ2

Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake.
107:3Juzuu 30 · uk. 602

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ3

Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?.
107:4Juzuu 30 · uk. 602

فَوَيْلٌ لِلْمُصَلِّينَ4

Basi adhabu kali itawafikia wenye kusali,
107:5Juzuu 30 · uk. 602

الَّذِينَ هُمْ عَنْ صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ5

ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake.
107:6Juzuu 30 · uk. 602

الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ6

Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria.
107:7Juzuu 30 · uk. 602

وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ7

Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kumuabudu Mola wao wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Ali Jaber - Al-Ma'un · Tlawati