Al-Layl

سورة الليل

Sura 92 · Makki · 21 aya

92:1Juzuu 30 · uk. 595

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake.
92:2Juzuu 30 · uk. 595

وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ2

Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku.
92:3Juzuu 30 · uk. 595

وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنْثَىٰ3

Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike,
92:4Juzuu 30 · uk. 595

إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ4

Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera.
92:5Juzuu 30 · uk. 595

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ5

Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa,
92:6Juzuu 30 · uk. 595

وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ6

akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo,
92:7Juzuu 30 · uk. 595

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ7

Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake.
92:8Juzuu 30 · uk. 595

وَأَمَّا مَنْ بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ8

Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake,
92:9Juzuu 30 · uk. 595

وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ9

akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo,
92:10Juzuu 30 · uk. 596

فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ10

Tutamnyoshea njia za mateso.
92:11Juzuu 30 · uk. 596

وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ11

Wala hayatamfaa yeye mali yake aliyoyafanyia ubakhili atakapotumbukia Motoni.
92:12Juzuu 30 · uk. 596

إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ12

Ni juu Yetu, kwa fadhila Zetu na busara Yetu, kueleza njia ya uongofu yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na ya upotevu.
92:13Juzuu 30 · uk. 596

وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ13

Na Sisi Tuna mamlaka ya maisha ya Akhera na maisha ya ulimwenguni.
92:14Juzuu 30 · uk. 596

فَأَنْذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ14

Ndipo nikawaonya , enyi watu, na kuwatisha moto wenye kuwaka, nao ni moto wa Jahanamu.
92:15Juzuu 30 · uk. 596

لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى15

Hataingia Moto huo isipokuwa aliyekuwa mbaya sana. Mwenye kumkanusha Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,
92:16Juzuu 30 · uk. 596

الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ16

na akakataa kumwamini na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
92:17Juzuu 30 · uk. 596

وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى17

Na ataepushwa nao mchaji Mwenyezi Mungu sana.
92:18Juzuu 30 · uk. 596

الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ18

Ambaye hutoa mali yake kwa kutaka nyongeza za kheri
92:19Juzuu 30 · uk. 596

وَمَا لِأَحَدٍ عِنْدَهُ مِنْ نِعْمَةٍ تُجْزَىٰ19

kutoa Kwake si kwa kulipa zema alizofanyiwa na mtu.
92:20Juzuu 30 · uk. 596

إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ20

Lakini anatoa kwa kutaka uso wa Mola wake na radhi zake. Basi Mwenyezi Mungu atampa,
92:21Juzuu 30 · uk. 596

وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ21

huko Peponi, malipo ya kumridhisha.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Ahmad Nainaa - Al-Layl · Tlawati