لَا أُقْسِمُ بِهَٰذَا الْبَلَدِ1
Al-Balad
سورة البلد
Sura 90 · Makki · 20 aya
90:1Juzuu 30 · uk. 594
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mji huu mtakatifu wa Makkah.
90:2Juzuu 30 · uk. 594
وَأَنْتَ حِلٌّ بِهَٰذَا الْبَلَدِ2
Na wewe, ewe Nabii, ni mkazi wa mji huu mtakatifu.
90:3Juzuu 30 · uk. 594
وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ3
Na Anaapa kwa mzazi wa wanaadamu, ambaye ni Ādam, amani imshukie, na kilichozalikana na yeye.
90:4Juzuu 30 · uk. 594
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي كَبَدٍ4
Hakika Tumemuumba binadamu katika usumbufu na shida za kilimwengu.
90:5Juzuu 30 · uk. 594
أَيَحْسَبُ أَنْ لَنْ يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ5
Kwani anadhani kwa mali aliyoyakusanya kuwa Mwenyezi Mungu Hatakuwa na uwezo juu yake?
90:6Juzuu 30 · uk. 594
يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُبَدًا6
Huwa akisema kwa kujigamba: «Nimetumia mali mengi.»
90:7Juzuu 30 · uk. 594
أَيَحْسَبُ أَنْ لَمْ يَرَهُ أَحَدٌ7
Kwani anadhani, kwa kitendo chake hiko, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, Hamuoni wala hatamhesabu juu ya kubwa na dogo?
90:8Juzuu 30 · uk. 594
أَلَمْ نَجْعَلْ لَهُ عَيْنَيْنِ8
Kwani hatukumpa macho mawili ya kuonea,
90:9Juzuu 30 · uk. 594
وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ9
ulimi na midomo miwili ya kusemea
90:10Juzuu 30 · uk. 594
وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ10
na kumfafanulia njia mbili: ya kheri na ya shari?
90:11Juzuu 30 · uk. 594
فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ11
Basi ajiepushe na janga la Akhera kwa kutoa mali yake ili aokoke.
90:12Juzuu 30 · uk. 594
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ12
Ni kitu gani kilichojulisha ni lipi hilo janga la Akhera na ni mambo gani yenye kusaidia kujiepusha nalo?
90:13Juzuu 30 · uk. 594
فَكُّ رَقَبَةٍ13
Ni kuacha huru shingo iliyoamini kuikomboa na utumwa.
90:14Juzuu 30 · uk. 594
أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ14
Au kulisha, wakati wa shida ya njaa,
90:15Juzuu 30 · uk. 594
يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ15
yatima mwenye ujamaa, ili ipatikane fadhila ya sadaka na ya kuunga kizazi,
90:16Juzuu 30 · uk. 594
أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ16
au masikini asiyekuwa na kitu.
90:17Juzuu 30 · uk. 594
ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ17
Kisha akawa, baada ya kufanya amali njema zilizotajwa, ni miongoni mwa waliotakasa Imani yao kwa Mwenyezi Mungu, wakausiana kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi na wakausiana kuwahurumia viumbe.
90:18Juzuu 30 · uk. 594
أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ18
Wenye kufanya hayo ndiwo watu wa kulia ambao watapelekwa Siku ya Kiyama upande wa kulia kuelekea Peponi.
90:19Juzuu 30 · uk. 595
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ19
Na wale waliokanusha Qur’ani ndio ambao watapelekwa, Siku ya Kiyama, upande wa kushoto kuelekea Motoni.
90:20Juzuu 30 · uk. 595
عَلَيْهِمْ نَارٌ مُؤْصَدَةٌ20
Malipo yao ni Moto wa Jahanamu wenye kuwafinika na kuwaziba.