An-Naba

سورة النبأ

Sura 78 · Makki · 40 aya

78:1Juzuu 30 · uk. 582

عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ1

Kuhusu kitu gani baadhi ya makafiri wa Kikureshi wanaulizana?
78:2Juzuu 30 · uk. 582

عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ2

Wanaulizana kuhusu habari iliyo na uzito mkubwa kabisa,
78:3Juzuu 30 · uk. 582

الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ3

nayo ni Qur’ani tukufu inayotoa habari za kufufuliwa ambako makafiri wa Kikureshi wana shaka nako na wanakukanusha.
78:4Juzuu 30 · uk. 582

كَلَّا سَيَعْلَمُونَ4

Mambo sivyo kama wanavyodhania hawa washirikina. Hapo watajua hawa washirikina upeo wa kukanusha kwao na kitawadhihirikia waziwazi kile Atakachowatenda Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama.
78:5Juzuu 30 · uk. 582

ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ5

Kisha litahakikishika kwao jambo hilo na utahakikishika kwao ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuhusu Qur’ani na kufufuliwa. Huu ni utisho na makemeo kwao.
78:6Juzuu 30 · uk. 582

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا6

Kwani hatukuwatandazia ardhi kama tandiko?
78:7Juzuu 30 · uk. 582

وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا7

Na Tukawafanyia majabali kuwa ni vigingi, ili isitisike nanyi?
78:8Juzuu 30 · uk. 582

وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا8

Na Tukawaumba aina mbali-mbali, mume na mke.
78:9Juzuu 30 · uk. 582

وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا9

Na Tukafanya usingizi wenu ni mapumziko kwa viwiliwili vyenu: ndani yake mnatulia na kupumzika?
78:10Juzuu 30 · uk. 582

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا10

Na Tukaufanya usiku kuwa ni vazi, unawavisha giza lake na kuwafinika, kama nguo inavyomsitiri mwenye kuivaa.
78:11Juzuu 30 · uk. 582

وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا11

Na Tukaufanya mchana ni kipindi cha kutafuta maisha, mnaenea humo kwa ajili ya maisha yenu na mnatembea humo kwa ajili ya maslahi yenu?
78:12Juzuu 30 · uk. 582

وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا12

Na Tukajenga juu yenu mbingu saba, madhubuti jengo lake, lilioumbwa kwa uzuri, halina mapasuko wala nyufa?
78:13Juzuu 30 · uk. 582

وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا13

Na Tukalifanya jua kuwa ni taa iwakayo na kung’ara?
78:14Juzuu 30 · uk. 582

وَأَنْزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا14

Na Tukateremsha kutoka kwenye mawingu yanyeshayo maji yamiminikayo kwa wingi,
78:15Juzuu 30 · uk. 582

لِنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا15

ili Tutoe kwa maji hayo nafaka inayoliwa na watu,
78:16Juzuu 30 · uk. 582

وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا16

nyasi zinazoliwa na wanyama na miti iliyosongamana kwa kutawanyika tagaa zake?
78:17Juzuu 30 · uk. 582

إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا17

Hakika Siku ya Uamuzi kati ya viumbe,
78:18Juzuu 30 · uk. 582

يَوْمَ يُنْفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا18

nayo ni Siku ya Kiyama, imekuwa ni wakati na ahadi iliyowekewa muda maalimu kwa watu wa mwanzo na wa mwisho.
78:19Juzuu 30 · uk. 582

وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا19

Na zikafunguliwa mbingu zikawa ni zenye milango mingi kwa ajili ya kuteremka Malaika.
78:20Juzuu 30 · uk. 582

وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا20

Na yakalipuliwa majabali baada ya kuwa yamekita, yakawa ni kama mangati.
78:21Juzuu 30 · uk. 582

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا21

Hakika Jahanamu, Siku Hiyo, itawalindiza wenye ukafiri ambao Moto huo umeandaliwa wao.
78:22Juzuu 30 · uk. 582

لِلطَّاغِينَ مَآبًا22

Kwa makafiri ndio marejeo.
78:23Juzuu 30 · uk. 582

لَابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا23

Watabakia humo muda mrefu ufuatanao, usiokoma.
78:24Juzuu 30 · uk. 582

لَا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا24

Hawatakula humo chochote kitakachozizimisha joto la moto kwao.
78:25Juzuu 30 · uk. 582

إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا25

Wala kinywaji kitakachowaondolea kiu yao. Isipokuwa maji moto na usaha wa watu wa motoni.
78:26Juzuu 30 · uk. 582

جَزَاءً وِفَاقًا26

Watakuwa wanalipwa kwa hilo malipo ya sawa yanayolingana na vitendo vyao walivyovitenda duniani
78:27Juzuu 30 · uk. 582

إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا27

Hakika wao walikuwa hawaiyogopi Siku ya Hesabu, na kwa hivyo hawakujitayarisha nayo kwa kufanya matendo ya kuwafaa.
78:28Juzuu 30 · uk. 582

وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا28

Na waliyakanusha waziwazi yaliyoletwa na Mitume.
78:29Juzuu 30 · uk. 582

وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا29

Na kila kitu Tulikijua na Tukakiandika katika Ubao uliohifadhiwa (Al-Lawḥ Al-Maḥfūd).
78:30Juzuu 30 · uk. 582

فَذُوقُوا فَلَنْ نَزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا30

Basi Onjeni, enyi makafiri, hayo yakiwa ni malipo ya vitendo vyenu, Hatutawazidishia isipokuwa adhabu juu ya adhabu yenu.
78:31Juzuu 30 · uk. 583

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا31

Hakika kwa wale ambao wanamuogopa Mola wao na huku wanatenda mema kuna kufaulu kwa kuingia Peponi.
78:32Juzuu 30 · uk. 583

حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا32

Hakika watapata Mabustani makubwa na zabibu.
78:33Juzuu 30 · uk. 583

وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا33

Na watapata wanawake wenye umri mdogo, wenye vifua vilivyojaza, marika na waume zao.
78:34Juzuu 30 · uk. 583

وَكَأْسًا دِهَاقًا34

Na watapata glasi zlizojaa pombe.
78:35Juzuu 30 · uk. 583

لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا35

Hawatasikia katika Pepo hiyo maneno ya upotofu wala kudanganyana.
78:36Juzuu 30 · uk. 583

جَزَاءً مِنْ رَبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا36

Watayapata yote hayo yakiwa ni malipo na zawadi na kipewa kingi cha kuwatosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
78:37Juzuu 30 · uk. 583

رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا37

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati ya hizo, Mwenye kuwarehemu duniani na Akhera. Hawataweza kumuomba isipokuwa kile walichopewa ruhusa kumuomba.
78:38Juzuu 30 · uk. 583

يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا ۖ لَا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَٰنُ وَقَالَ صَوَابًا38

Siku atakaposimama Jibrili na Malaika wengine hali ya kujipanga mlolongo. Hawatamuombea isipokuwa yule aliyetolewa ruhusa na Mwingi wa Rehema ya kuombewa na akasema maneno ya haki na ya sawa.
78:39Juzuu 30 · uk. 583

ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ ۖ فَمَنْ شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا39

Hiyo ndiyo siku ya haki isiyokuwa na shaka kuja kwake. Kwa hivyo, yule atakaye kuokoka na vituko vya Siku hiyo, na ajifanyie njia ya marejeo kwa Mola wake kutenda vitendo vyema.
78:40Juzuu 30 · uk. 583

إِنَّا أَنْذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنْظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنْتُ تُرَابًا40

Sisi Tunawaonya nyinyi adhabu ya Siku ya mwisho iliyo karibu. Siku ambayo atayaona kila mtu aliyoyatenda katika kheri au aliyoyachuma miongoni mwa madhambi. Na kafiri atasema, kwa kitisho cha Hesabu, «Laiti mimi nilikuwa mchanga na sikufufuliwa.»

Cheza kutoka mwanzo wa sura