Al-Falaq

سورة الفلق

Sura 113 · Makki · 5 aya

113:1 · Al-FalaqJuzuu 30 · uk. 604

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ1

Sema, ewe Mtume, «Najilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa asubuhi.
113:2Juzuu 30 · uk. 604

مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ2

«Kutokana na shari la viumbe na udhia wao
113:3Juzuu 30 · uk. 604

وَمِنْ شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ3

«Na shari la usiku wenye giza lingi ungiapo na ujikitapo na mashari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake.
113:4Juzuu 30 · uk. 604

وَمِنْ شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ4

«Na shari la wchawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga.
113:5Juzuu 30 · uk. 604

وَمِنْ شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ5

«Na shari la hasidi mwenye kutukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Aliyewaneemesha ziwaondokee.»

Cheza kutoka mwanzo wa sura