An-Nas

سورة الناس

Sura 114 · Makki · 6 aya

114:1 · An-NasJuzuu 30 · uk. 604

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ1

Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu, Mwenye uweza, Peke Yake, wa kulirudisha shari lao.
114:2Juzuu 30 · uk. 604

مَلِكِ النَّاسِ2

«Mfalme wa watu, Mwenye kupeleka mambo yao yote Anavyotaka, Aliye Mkwasi kutowahitajia.
114:3Juzuu 30 · uk. 604

إِلَٰهِ النَّاسِ3

«Mola wa watu, Ambaye hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye.
114:4Juzuu 30 · uk. 604

مِنْ شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ4

«Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu.
114:5Juzuu 30 · uk. 604

الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ5

«Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu.
114:6Juzuu 30 · uk. 604

مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ6

«Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.»

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Abdullah Basfar - An-Nas · Tlawati