Al-Adiyat

سورة العاديات

Sura 100 · Makki · 11 aya

100:1Juzuu 30 · uk. 599

وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا1

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda shoti katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina.
100:2Juzuu 30 · uk. 599

فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا2

Na wenye kutoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi.
100:3Juzuu 30 · uk. 599

فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا3

Wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi.
100:4Juzuu 30 · uk. 599

فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا4

Wakarusha vumbi kwa mbio zao.
100:5Juzuu 30 · uk. 599

فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا5

Wakautia kati, kwa kuuzunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui.
100:6Juzuu 30 · uk. 600

إِنَّ الْإِنْسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ6

Hakika binadamu ni mkanushaji sana neema za Mola wake.
100:7Juzuu 30 · uk. 600

وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ7

Na yeye anakubali ukanushaji wake.
100:8Juzuu 30 · uk. 600

وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ8

Na yeye ana pupa sana la mali.
100:9Juzuu 30 · uk. 600

۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ9

Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa?
100:10Juzuu 30 · uk. 600

وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ10

Na (kwani yeye hajui) yakatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema au maovu?.
100:11Juzuu 30 · uk. 600

إِنَّ رَبَّهُمْ بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَخَبِيرٌ11

Hakika Mola wao kwao na kwa amali zao, Siku Hiyo, ni Mtambuzi; hakuna chenye kufichamana Kwake.

Cheza kutoka mwanzo wa sura