Al-Ghashiyah

سورة الغاشية

Sura 88 · Makki · 26 aya

88:1Juzuu 30 · uk. 592

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ1

Je, ilikujia,ewe Mtume, habari ya Kiyama chenye vituko venye kuwaenea watu?
88:2Juzuu 30 · uk. 592

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ2

Nyuso za Makafiri, Siku hiyo, zitakuwa zimenyongeka kwa adhabu.
88:3Juzuu 30 · uk. 592

عَامِلَةٌ نَاصِبَةٌ3

Zishughulishie, zimechoka na kutaabika.
88:4Juzuu 30 · uk. 592

تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً4

Zinachomwa kwa Moto wenye kuwaka kwa ukali.
88:5Juzuu 30 · uk. 592

تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ5

Zitanyweshwa maji ya chemchemi yenye moto sana.
88:6Juzuu 30 · uk. 592

لَيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِنْ ضَرِيعٍ6

Watu wa Motoni hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotoka kwenye mti wa miba ilioshikana na chini. Ni kibaya sana chakula hiko na ni kichafu mno.
88:7Juzuu 30 · uk. 592

لَا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِنْ جُوعٍ7

Hakimnoneshi mwenye kukila, awapo amekonda, wala hakimuondolei njaa, awapo na njaa.
88:8Juzuu 30 · uk. 592

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَاعِمَةٌ8

Nyuso za Waumini, siku ya Kiyama, zitakuwa kwenye neema.
88:9Juzuu 30 · uk. 592

لِسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ9

Kwa kuwa zilijishughulisha ulimwenguni kumtii Mwenyezi Mungu na kuridhika na Akhera.
88:10Juzuu 30 · uk. 592

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ10

Zitakuwa kwenye Pepo ya daraja ya juu.
88:11Juzuu 30 · uk. 592

لَا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً11

Hutasikia humo hata neno moja la upuuzi.
88:12Juzuu 30 · uk. 592

فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ12

Ndani yake kuna chemchemi yenye kuteremka maji yake.
88:13Juzuu 30 · uk. 592

فِيهَا سُرُرٌ مَرْفُوعَةٌ13

Ndani yake mna vitanda vilioangatika,
88:14Juzuu 30 · uk. 592

وَأَكْوَابٌ مَوْضُوعَةٌ14

na vikombe vilivyotayarishwa kwa wenye kunywa,
88:15Juzuu 30 · uk. 592

وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ15

na mito iliyopangwa, mmoja baada ya mwingine,
88:16Juzuu 30 · uk. 592

وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ16

na mazulia mengi yaliyotandikwa.
88:17Juzuu 30 · uk. 592

أَفَلَا يَنْظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ17

Kwani, hawa makafiri wenye kukanusha, hawaangalii ngamia namna walivyoumbwa kiajabu?
88:18Juzuu 30 · uk. 592

وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ18

Na mbingu namna zlizoinuliwa juu kwa namna ya kupendeza?
88:19Juzuu 30 · uk. 592

وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ19

Na milima namna iliyoimarishwa ukapatikana uthabiti na utulivu wa ardhi?
88:20Juzuu 30 · uk. 592

وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ20

Na ardhi namna ilivyotandikwa na kutayarishwa?
88:21Juzuu 30 · uk. 592

فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنْتَ مُذَكِّرٌ21

Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale wenye kupa nyongo yale uliyotumilizwa kwayo wala usihuzunike kwa kupa mgongo kwao.
88:22Juzuu 30 · uk. 592

لَسْتَ عَلَيْهِمْ بِمُصَيْطِرٍ22

Kwani wewe ni muwaidhiaji kwao, na si juu yako kuwalazimisha kuamini..
88:23Juzuu 30 · uk. 593

إِلَّا مَنْ تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ23

Lakini yule mwenye kuyapa mgongo makumbusho na mawaidha na akawa mkakamavu kwenye ukafiri wake,
88:24Juzuu 30 · uk. 593

فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ24

Mwenyezi Mungu Atamuadhibu adhabu kali Motoni.
88:25Juzuu 30 · uk. 593

إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ25

Hakika wao watarudi kwetu baada ya kufa.
88:26Juzuu 30 · uk. 593

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُمْ26

Kisha ni juu yetu kuwalipa kwa waliyoyafanya.

Cheza kutoka mwanzo wa sura