Al-Mursalat

سورة المرسلات

Sura 77 · Makki · 50 aya

77:1Juzuu 29 · uk. 580

وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا1

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa upepo unapovuma kwa mfululizo, huu baada ya huu.
77:2Juzuu 29 · uk. 580

فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا2

Na kwa upepo wenye kuvuma kwa ukali wenye kuangamiza.
77:3Juzuu 29 · uk. 580

وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا3

Na kwa Malaika waliopewa jukumu la mawingu, wakawa wayapeleka pale anapotaka Mwenyezi Mungu.
77:4Juzuu 29 · uk. 580

فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا4

Na kwa Malaika wanaoshuka, kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
77:5Juzuu 29 · uk. 580

فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا5

na amri zinazopambanua baina ya haki na batili na halali na haramu.
77:6Juzuu 29 · uk. 580

عُذْرًا أَوْ نُذْرًا6

Na kwa Malaika wanaoupokea wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuuteremsha kwa Manabii Wake, unaowapa viumbe wake udhuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na pia onyo kutoka Kwake, ili watu wasiwe na hoja.
77:7Juzuu 29 · uk. 580

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ7

Hakika jambo la Kiyama mnaloahidiwa pamoja na lile la kuhesabiwa na kulipwa ni lenye kuwa hapana shaka.
77:8Juzuu 29 · uk. 580

فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ8

Basi nyota zitakapofutwa na mwangaza wake ukaondoka,
77:9Juzuu 29 · uk. 580

وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ9

na mbingu zitakapopasuka,
77:10Juzuu 29 · uk. 580

وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ10

na majabali yatakapopeperuka na kukueanea huku na kule na yakawa ni mapepe yanayorushwa na upepo,
77:11Juzuu 29 · uk. 580

وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ11

Na Mitume watapowekewa wakati na muda wa baina yao na ummah wao na kusemwe,
77:12Juzuu 29 · uk. 580

لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ12

«Ni Siku kubwa gani Mitume wameahirishiwa?»
77:13Juzuu 29 · uk. 580

لِيَوْمِ الْفَصْلِ13

Wameahirishiwa Siku ya hukumu na uamuzi baina ya viumbe.
77:14Juzuu 29 · uk. 580

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ14

Na nilipi lililokujulisha wewe, ewe binadamu, ni siku gani hiyo ya kutolewa uamuzi na ni zipi shida zake na vituko vyake?
77:15Juzuu 29 · uk. 580

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ15

Maangamivu makubwa Siku hiyo ni ya wale waliyoikanusha Siku hii iliyoahidiwa.
77:16Juzuu 29 · uk. 580

أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ16

Kwani hatukuawaangamiza walitangulia kati ya umma waliopita kwa kuwakanusha kwao Mitume, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd?
77:17Juzuu 29 · uk. 580

ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ17

Kisha tutawakutanisha na wao wale waliokuja nyuma kati ya wale waliokuwa ni kama wao katika ukanushaji na uasi.
77:18Juzuu 29 · uk. 580

كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ18

Mfano wa uangamizaji huo mkali ndivyo tutakavyowafanya wahalifu kati ya makafiri wa Makkah, kwa kumkanusha kwao Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
77:19Juzuu 29 · uk. 580

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ19

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa kila mwenye kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, unabii, kufufuliwa na kuhesabiwa.
77:20Juzuu 29 · uk. 581

أَلَمْ نَخْلُقْكُمْ مِنْ مَاءٍ مَهِينٍ20

Je kwani sisi hatukuwaumba nyinyi, enyi mkusanyiko wa makafiri, kutokana na maji dhaifu yaliyo matwevu nayo ni tone la manii,
77:21Juzuu 29 · uk. 581

فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَكِينٍ21

tukayaweka maji haya kwenye mahali palipohifadhika, napo ni kizazi cha mwanamke,
77:22Juzuu 29 · uk. 581

إِلَىٰ قَدَرٍ مَعْلُومٍ22

mpaka kipindi maalumu kinachojulikana na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?
77:23Juzuu 29 · uk. 581

فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ23

Tukaweza kumuumba, kumtia sura na kumtoa. Basi bora wa wenye kuweza ni s isi.
77:24Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ24

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kukanusha uweza wetu.
77:25Juzuu 29 · uk. 581

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا25

Je kwani hatukuifanya hii ardhi mnayoishi juu yake
77:26Juzuu 29 · uk. 581

أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا26

ikusanye juu ya mgongo wake walio hai wasiohesabika, na ndani ya matumbo yake wafu wasiodhibitika, na
77:27Juzuu 29 · uk. 581

وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُمْ مَاءً فُرَاتًا27

tukajaalia iwe na majabali yaliyojikita yaliyo marefu ili isitikisike na nyinyi, na tukawanywesha maji tamu yaliyo mazuri?
77:28Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ28

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa waliozikanusha neema hizi.
77:29Juzuu 29 · uk. 581

انْطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ29

Wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama, «Endeni kwenye adhabu ya moto wa Jahanamu mliokuwa mkiukanusha duniani.
77:30Juzuu 29 · uk. 581

انْطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ30

Endeni mjifinike kwenye kivuli cha moshi wa moto wa Jahanamu ambacho hapo panachembuka vipande vitatu.
77:31Juzuu 29 · uk. 581

لَا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ31

Kivuli hiko hakimfanyi mtu ahifadhike na joto la Siku hiyo wala hakizuii muwako wa Moto chochote.
77:32Juzuu 29 · uk. 581

إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ32

Hakika moto wa Jahanamu unarusha macheche makubwa ya moto, kila cheche moja katika hayo ni kama jengo lililoimarishwa katika ukubwa na urefu wa kuenda juu.
77:33Juzuu 29 · uk. 581

كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ33

Kama kwamba hizo cheche za moto wa Jahanamu zinazopaa juu ni ngamia weusi ambao rangi yao imeingia kwenye umanjano.»
77:34Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ34

Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kukanusha mateso yaliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu.
77:35Juzuu 29 · uk. 581

هَٰذَا يَوْمُ لَا يَنْطِقُونَ35

Hii ndiyo Siku ya Kiyama ambayo wakanushaji hawatatamka maneno ya kuwanufaisha
77:36Juzuu 29 · uk. 581

وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ36

wala hawatapewa idhini ya kusema wakatoa nyudhuru, kwa kuwa hawatakuwa na udhuru wowote.
77:37Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ37

Maangamivu na adhabu kali kwa wenye kuikanusha siku hii na yaliyomo ndani yake.
77:38Juzuu 29 · uk. 581

هَٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ38

Hii ni Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atatoa uamuzi baina ya viumbe, na ukweli na ubatilifu utapambanuka. Tutawakusanya nyinyi Siku hiyo, enyi makafiri wa ummah huu, pamoja na makafiri wa mwanzo miongoni mwa ummah waliopita.
77:39Juzuu 29 · uk. 581

فَإِنْ كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ39

Basi mkiwa na hila za kujitoa na adhabu, tumieni hila zenu na mziokoe nafsi zenu na msukosuko wa Mwenyezi Mungu na mateso Yake.
77:40Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ40

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Kiyama.
77:41Juzuu 29 · uk. 581

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ41

Hakika ya wale waliomuogopa Mola wao duniani na wakaiogopa adhabu Yake kwa kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Wao Siku ya Kiyama watakuwa kwenye vivuli vya miti vilivyonyoka, na chemchemi za maji zinazotembea,
77:42Juzuu 29 · uk. 581

وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ42

na matunda mengi yanayopendwa na nafsi zao ambayo wao wanastarehe nayo. Hapo waambiwe,
77:43Juzuu 29 · uk. 581

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ43

«Kuleni chakula chenye ladha na mnyweni kinywaji chenye kufurahisha kwa sababu ya matendo mema mliyoyatanguliza duniani.»
77:44Juzuu 29 · uk. 581

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ44

Sisi, kwa mfano wa malipo hayo makubwa, tutawalipa watu wema katika matendo yao na utiifu wao kwetu.
77:45Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ45

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya Malipo na Hesabu, na kuzikanusha sterehe na mateso yaliyomo Siku hiyo.
77:46Juzuu 29 · uk. 581

كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُمْ مُجْرِمُونَ46

Kisha Mwenyezi Mungu Akawaonya makafiri kwa kusema, «Kuleni aina ya vyakula vya ladha duniani na stareheni kwa matamanio yake yenye kumalizika kwa muda mchache, hakika nyinyi ni wahalifu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.»
77:47Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ47

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa.
77:48Juzuu 29 · uk. 581

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ48

Na wanapoambiwa hawa washirikina, «Mswalieni Mwenyezi Mungu na mnyenyekeeni,» hawanyenyekei wala hawaswali, bali wanaendelea kuonyesha kiburi chao.
77:49Juzuu 29 · uk. 581

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ49

Maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa wenye kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu.
77:50Juzuu 29 · uk. 581

فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ50

Iwapo wao hawataiamini hii Qur’ani, basi wataamini kitabu gani na maneno gani baada yake? Na Qur’ani yenyewe ni Kitabu kilichobainisha kila kitu, kilicho wazi katika hekima zake, hukumu zake na habari zake, chenye kushinda katika matamko yake na maana yake.

Cheza kutoka mwanzo wa sura