Nuh

سورة نوح

Sura 71 · Makki · 28 aya

71:1Juzuu 29 · uk. 570

إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ أَنْ أَنْذِرْ قَوْمَكَ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ1

Kwa hakika sisi tulimpeleka Nūḥ kwa watu wake na tukamwambia, «Waonye watu wako kabla ya kufikiwa na adhabu yenye kuumiza.»
71:2Juzuu 29 · uk. 570

قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُبِينٌ2

Nūḥ akasema, «Enyi watu wangu! Mimi kwenu nyinyi ni mwonyaji waziwazi, anayewaonya nyinyi adhabu ya Mwenyezi Mungu iwapo mtamuasi.
71:3Juzuu 29 · uk. 570

أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ3

Na mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu. Muabuduni Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake na muogopeni Yeye na nitiini mimi katika kile ninachowaamrisha nyinyi na kuwakataza. Basi mkinitii mimi na mkanikubalia,
71:4Juzuu 29 · uk. 570

يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ اللَّهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ4

Mwenyezi Mungu Atawasamehe dhambi zenu na kuwafinikia, atawarefushia umri wenu mpaka kipindi kilichokadiriwa katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Kwani kifo kikija hakicheleweshwi kabisa. Lau mngalijua hilo mngalifanya haraka kuamini na kutii.»
71:5Juzuu 29 · uk. 570

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا5

Nūḥ akasema, «Mola wangu! Kwa hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana ili wakuamini wewe na wakutii.
71:6Juzuu 29 · uk. 570

فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا6

Ulinganizi wangu kwao ili waamini, haukuwaongezea kitu isipokuwa ni kukimbia na kuipa mgongo haki.
71:7Juzuu 29 · uk. 570

وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا7

Na mimi kila nikiwalingania wao ili wakuamini wewe, ipate kuwa hiyo ni njia ya wewe kuwasamehe dhambi zao, hutia vidole vyao masikioni mwao, ili wasisikie ulinganizi wa haki, na hujifinika nguo zao wasipate kuniona, na hujikita kwenye ukafiri wao na hufanya kiburi sana cha kutoikubali haki.
71:8Juzuu 29 · uk. 570

ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا8

Kisha mimi ni kawalingania wao kwenye Imani waziwazi na sio kwa kujificha.
71:9Juzuu 29 · uk. 570

ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنْتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا9

Kisha nikawatangazia wao ulinganizi kwa sauti kubwa wakati mwingine, na nikausirisha huo ulinganizi kwa sauti ya chini wakati mwingine.
71:10Juzuu 29 · uk. 570

فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا10

Ni kawaambia watu wangu, ‘Muombeni Mola wenu msamaha wa dhambi zenu na tubieni Kwake kutokana na ukafiri wenu, hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia miongoni mwa waja Wake na akurudia Kwake.’»
71:11Juzuu 29 · uk. 571

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُمْ مِدْرَارًا11

Mtakapotubia na mkaomba msamaha, Mwenyezi Mungu Atawateremshia mvua nyingi ya mfululizo,
71:12Juzuu 29 · uk. 571

وَيُمْدِدْكُمْ بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَلْ لَكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَلْ لَكُمْ أَنْهَارًا12

Atayaongeza mali yenu na pia watototo wenu, Atawafanya muwe na mabustani ya nyinyi kuneemeka kwa matunda yake na uzuri wake, na Atawajaalia nyinyi muwe na mito ambayo mtaitumia kwa kuipatia maji mimea yenu na pia wanyama wenu.
71:13Juzuu 29 · uk. 571

مَا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّهِ وَقَارًا13

Mnani nyinyi, enyi watu, hamuogopi ukuu wa Mwenyezi Mungu na uweza Wake,
71:14Juzuu 29 · uk. 571

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا14

na hali yeye Amewaumba nyinyi katika miongo yenye kufuatana :tone la manii, kisha pande la damu, kisha nofu la nyama, kisha mifupa na nyama?
71:15Juzuu 29 · uk. 571

أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا15

Kwani hamtazami namna alivyoumba Mwenyezi Mungu mbingu saba zilizopandana, kila uwingu juu ya mwingine,
71:16Juzuu 29 · uk. 571

وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا16

Akajaalia mwezi, katika mbigu hizi, ni wenye mwangaza,, na Akajaalia jua ni taa yenye kung’ara ili kuwapatia mwangaza watu walioko ardhini?
71:17Juzuu 29 · uk. 571

وَاللَّهُ أَنْبَتَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا17

Mwenyezi Mungu aliumba asili yenu kutokana na ardhi,
71:18Juzuu 29 · uk. 571

ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا18

kisha Atawarudisha humo ardhini baada ya kufa, na Awatoe Siku ya kufufuliwa kuwatoa kihakika.
71:19Juzuu 29 · uk. 571

وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا19

Na Mwenyezi Mungu Amewafanyia hii ardhi ni tandiko kama mkeka.
71:20Juzuu 29 · uk. 571

لِتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا20

Ili mfuate humo njia zilizo kunjufu.
71:21Juzuu 29 · uk. 571

قَالَ نُوحٌ رَبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَنْ لَمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا21

Nūḥ alisema, «Mola wangu! Kwa hakika watu wangu wameendelea sana kuniasi na kunikanusha, na wanyonge miongoni mwao wakawafuata viongozi wapotevu ambao mali yao na watoto wao havikuwaongezea isipokuwa upotevu wa duniani na mateso ya Akhera.
71:22Juzuu 29 · uk. 571

وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا22

Na hao viongozi wa upotevu wakawafanyia wafuasi wao wanyonge vitimbi vikubwa,
71:23Juzuu 29 · uk. 571

وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا23

na wakawaambia, ‘Msiache kuwaabudu waungu wenu mkaelekea kwenye kumubadu Mwenyezi Mungu Peke Yake, ambaye Nūḥ anawalingania nyinyi mumuabudu, na msimuache Wadd, Suwā‘, Yghūth, Ya’ūq wala Nasr.» Na haya ni majina ya masanamu wao ambao walikuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, na yalikuwa ni majina ya watu wema. Walipokufa, Shetani alitia kwenye mawazo ya watu wao wawasimamishie masanamu na picha ili wapate moyo, kama wanavyodai, wa kuwa watiifu wanapoyaona. Walipoondoka hao waliosimamisha masanamu na muda mrefu ukapita, wakaja watu wasiokuwa wao, Shetani aliwatia tashwishi kwamba wakale wao waliopita walikuwa wakiyaabudu haya masanamu na picha na kutawasali nayo. Hii ndio hekima ya kuharamishwa masanamu na kuharamishwa ujengaji wa makuba juu ya makaburi. Kwa kuwa hayo kwa kupitiwa na muda yanakuwa ni yenye kuabudiwa na wajinga.
71:24Juzuu 29 · uk. 571

وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا24

Na hawa wafuatwa wamewapoteza watu wengi kwa vile walivyowapambia njia za upotofu upotevu. Kisha Nūḥ akaendelea kusema, «Na usiwaongezee, ewe Mola wetu, hawa waliozidhulumu nafsi zao kwa ukanushaji na ushindani isipokuwa kuwaepusha na haki.»
71:25Juzuu 29 · uk. 571

مِمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْصَارًا25

Kwa sababu ya dhambi zao na ukakamavu wao juu ya ukafiri na uasi, walizamishwa kwa mafuriko na wakaingizwa baada ya kuzamishwa kwenye Moto unaowakia sana na kuchoma, na wasimpate, badala ya Mwenyezi Mungu, mwenye kuwaokoa au kuwaepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu
71:26Juzuu 29 · uk. 571

وَقَالَ نُوحٌ رَبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا26

Na akasema Nūḥ, amani imshukie, baada ya kukata tama na watu wake, «Mola wangu! Usimuache yoyote miongoni mwa wale wanaokukanusha kuwa ni mwenye kuishi juu ardhi akizunguka na kutembea.
71:27Juzuu 29 · uk. 571

إِنَّكَ إِنْ تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا27

Hao ukiwaacha, bila kuwaangamiza, watawapoteza waja wako waliokuamini na kuwapotosha njia ya haki, na haji yoyote kutokana na migongo yao na vizazi vyao isipokuwa yule aliyepotoka na njia ya haki na kukukanusha wewe sana na kukuasi.
71:28Juzuu 29 · uk. 571

رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَنْ دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا28

Mola wangu! Nisamehe mimi, wazazi wangu wawili, mwenye kuingia nyumbani kwangu na hali yeye ameamini, wanaume na wanawake waliokuamini wewe, na usiwaongezee makafiri isipokuwa maangamivu na hasara, duniani na Akhera.»

Cheza kutoka mwanzo wa sura