At-Takwir

سورة التكوير

Sura 81 · Makki · 29 aya

81:1Juzuu 30 · uk. 586

إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ1

Pindi jua litakapokunjwa, na mwangaza wake ukaondoka.
81:2Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا النُّجُومُ انْكَدَرَتْ2

Na pindi nyota zitakapopuputika na nuru yake ikafutika.
81:3Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ3

Na pindi majabali yatakapoondoshawa kwenye uso wa ardhi yakawa ni vumbi linaloenea.
81:4Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ4

Na pindi ngamia wenye mimba watakapoachwa na kupuuzwa.
81:5Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ5

Na pindi wanyama mwitu watakapokusanywa na kutangamanishwa, ili Mwenyezi Mungu Awape nafasi ya kulipizana wao kwa wao.
81:6Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ6

Na pindi bahari zitakapowashwa moto zikawa ni moto unaowaka.
81:7Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ7

Na pindi nafsi zitakapokutanishwa na mfano wake na sampuli yake.
81:8Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ8

Na pindi mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa, Siku ya Kiyama, suala la kumbembeleza na kumkejeli aliyemzika:
81:9Juzuu 30 · uk. 586

بِأَيِّ ذَنْبٍ قُتِلَتْ9

ni kwa dhambi gani ilikuwa kuzikwa kwake?
81:10Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ10

Na pindi kurasa za matendo zitakapoonyeshwa.
81:11Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ11

Na pindi mbingu zitakapong’olewa na kuondoshwa zilipokuwa.
81:12Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ12

Na pindi Moto utakapowashwa na ukawaka.
81:13Juzuu 30 · uk. 586

وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ13

Na pindi Pepo , Nyumba ya Neema, itakaposongezewa watu wake wachamungu.
81:14Juzuu 30 · uk. 586

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَا أَحْضَرَتْ14

Litakapotokea hilo, itayakinisha kila nafsi na kujua kile ilichokitanguliza cha kheri au shari.
81:15Juzuu 30 · uk. 586

فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ15

Anaapa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa nyota zinazofichika nuru yake mchana,
81:16Juzuu 30 · uk. 586

الْجَوَارِ الْكُنَّسِ16

zinazotembea na zinazoghibu katika anga zake.
81:17Juzuu 30 · uk. 586

وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ17

Na Anaapa kwa usiku unapojitokeza na giza lake.
81:18Juzuu 30 · uk. 586

وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ18

Na kwa asubuhi unapojitokeza mwangaza wake.
81:19Juzuu 30 · uk. 586

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ19

Hakika Qur’ani ni ujumbe wa mjumbe mtukufu , naye ni Jibrili, amani imshukike.
81:20Juzuu 30 · uk. 586

ذِي قُوَّةٍ عِنْدَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ20

Mwenye nguvu katika kuyapitisha yale anayoamrishwa. Mwenye cheo cha juu kwa Mwenyezi Mungu. Anayesikilizwa na Malaika.
81:21Juzuu 30 · uk. 586

مُطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ21

Anayeaminiwa juu ya Wahyi anaoteremka nao.
81:22Juzuu 30 · uk. 586

وَمَا صَاحِبُكُمْ بِمَجْنُونٍ22

Hakuwa Muhammad mnayemjua ni mwendawazimu.
81:23Juzuu 30 · uk. 586

وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ23

Na kwa hakika Muhammad alimuona Jibrili anayemjia na utume katika pambizo kubwa.
81:24Juzuu 30 · uk. 586

وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ24

Wala yeye hafanyi ubakhili katika kufikisha Wahyi.
81:25Juzuu 30 · uk. 586

وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَجِيمٍ25

Wala haikuwa hii Qur’ani ni neno la Shetani aliyefukuzwa na kutolewa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu. Lakini Qur’ani hii ni maneno ya Mwenyezi Mungu na ni Wahyi wake.
81:26Juzuu 30 · uk. 586

فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ26

Akili zenu zawapeleka wapi katika kukanusha baada ya hoja hizi zilizo wazi na zenye nguvu?
81:27Juzuu 30 · uk. 586

إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِلْعَالَمِينَ27

Hayakuwa haya isipokuwa ni mawaidha kutoka kwa Mwenyezi Mungu yanapewa watu wote.
81:28Juzuu 30 · uk. 586

لِمَنْ شَاءَ مِنْكُمْ أَنْ يَسْتَقِيمَ28

Kwa atakaye, kati yenu, kulingana juu ya haki na Imani.
81:29Juzuu 30 · uk. 586

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ29

Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote.

Cheza kutoka mwanzo wa sura