Al-Fil

سورة الفيل

Sura 105 · Makki · 5 aya

105:1Juzuu 30 · uk. 601

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ1

Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu?
105:2Juzuu 30 · uk. 601

أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِي تَضْلِيلٍ2

Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?
105:3Juzuu 30 · uk. 601

وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ3

Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana,
105:4Juzuu 30 · uk. 601

تَرْمِيهِمْ بِحِجَارَةٍ مِنْ سِجِّيلٍ4

ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu.
105:5Juzuu 30 · uk. 601

فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَأْكُولٍ5

Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa.

Cheza kutoka mwanzo wa sura

Abdulbasit Abdussamad - Al-Fil · Tlawati